wa Algeria Abdelmadjid Tebboune hivi jana aliongoza mkutano wa baraza kuu la usalama kujadili maendeleo ya usalama nchini
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune hivi jana (Alhamisi) aliongoza mkutano wa baraza kuu la usalama kujadili maendeleo ya usalama nchini humo, na vilevile katika maeneo ya kaskazini mwa Afrika ikiwemo Libya na Mali, shirika la habari nchini humo APS liliripoti.
Kwa mujibu wa taarifa wa Rais Abdelmadjid, hatua zimechukuliwa ili kudhibiti usalama mpakani, na vilevile kutoa msukumo mpya kwa jukumu la Algeria katika kiwango cha mataifa. Taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi juu ya hatua hizo.
Rais Abdelmadjid aliitisha mkutano wa mara kwa mara wa baraza la usalama.Huu ni mkutano wa kwanza mkubwa rais wa nchi hiyo ameongoza tangu kifo cha hivi karibuni cha mkuu wa jeshi Ahmed Gaid Salah.
Comments
Post a Comment