Wachimbaji kumi na watatu wameokolewa baada ya kukwama chini ya vifusi kwa zaidi ya masaa 80
katika mgodi mmoja katika mkoa wa Sichuan kusini magharibi mwa China,viongozi wa eneo hilo walisema hivi leo (Jumatano).
Uokoaji huo ulianza saa 3:26 mchana siku ya Jumamosi katika mgodi wa Shanmushu mjini Yibin,kulingana na mamlaka ya usimamizi wa dharura ya eneo hilo.
Timu kumi na tatu za uokoaji zilizo na waokoaji 251 zilibadilishana katika shughuli hiyo ya utafutaji.
Comments
Post a Comment