Wachimbaji wadogo wa madini waomba kupewa maeneo yaliyotelekezwa



Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu nchini  wameiomba serikali iwapatie  maeneo yaliyotelekezwa ili waweze kuchimba dhahabu kuondoa mwingiliano kati ya wachimbaji wakubwa pamoja na kupunguza migogoro ya wachimbaji


Wachimbaji hao wametoa ombi hilo kwa waziri wa madini wilayani Chato katika uzinduzi wa soko kuu la dhahabu Chato huku wakiainisha changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo
Waziri wa nishati Dkt.Medard Kalemani amesema umefika wakati kwa wizara ya madini kutoa leseni kwa wachimbaji na wauzaji wa madini kupewa leseni ili waweze kusafirisha madini nje ya nchi ili kudhibiti utoroshwaji wa madini.
Waziri wa madini Mhe.Dotto Biteko amemwagiza afisa madini mkoa wa Geita kutoa leseni mia mbili ndani ya siku saba kwa wachimbaji wadogo mkoa wa Geita ili kuondoa malalamiko.

Comments