Mwanasheria
kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bi.Happy Msimbe akitoa huduma kwa Mmoja
wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali
yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine akipata huduma ya kusajili Taasisi
yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka
2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi
linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam kwa kanda ya Mashariki.

Mwanasheria
kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bi. Idda Kombe akitoa huduma kwa Mmoja

Wanasheria
kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO kutoka kulia ni Denis Bashaka, wa pili
kulia ni January kitunsi na wa pili kushoto Faki Shaweji wakifafanua
jambo kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine akipata huduma ya
kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.
3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za
Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki.

Msajili
na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Vickness Mayao
(Kushoto) akimsikiliza kwa makini aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Neema Mwanga wakati wa zoezi la
kusajili Taasisi na Mashirika yaliyosajiliwa chini ya sheria nyingine
kuja chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka

***************
Na Mwandishi Wetu
Wadau
kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini ambao awali
walisajiliwa katika Sheria nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali wameridhishwa na kasi ya uhuishaji wa usajili wa Taasisi na
Mashirika hayo.
Hayo
yamebainika leo jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi linaloendelea la
kuhuisha usajili wa Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo
awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine ikiwemo “Societies Act Cap
337” (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) ; “Trustees’ Incorporation Act
Cap. 318 (RITA); na The Companies Act Cap 212 (Msajili wa
Makampuni-BRELA) ambazo zinatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa
marekebisho na Sheria Na. 3/2019.
Wakizungumza
wakati wa zoezi hilo mmoja wa wadau kutoka Shirika la ‘SOS Village
Children’ Bw. Dhiyant Patel Patel amesema kuwa Shirika lao lilikuwa
limesajiliwa chini ya Sheria ya “Trustees’ Incorporation Act Cap. 318
(RITA) hivyo kuhitajika kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na
Sheria Na. 3/2019.
Bw.
Patel ameongeza kuwa zoezi hilo lina umuhimu na manufaa kwa Taasisi na
Mashirika hayo kwani litawasaidia kuendelea kutekeleza majukumu yao ya
kila siku kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizopo.
“Niwapongeze
Wizara na kwa hatua hii ya kasi ya kuhuisha usajili wa Mashirika
yaliyokuwa nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini sisi
tumeitikia wito na tuko pamoja katika hili” alisisitiza Bw.Patel
Bw.Patel
ametoa wito kwa Mashirika yanayotakiwa kujisajili chini ya Sheria ya

marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo
ili kuondokana na usumbufu mara baada ya Serikali kukamilisha zoezi
hilo.
“Zoezi
hili linaenda vizuri na hatukuamini kwamba tunaweza tukapata huduma hii
kwa muda wa masaa mawili kusajili na kupata cheti husika” alisema.
Naye
Mwakilishi wa Shirika la Bunjiri Community Development Support Bw.
Ernest Mwanzi amesema kuwa Serikali imefanya jambo la muhimu kwa
kuendesha zoezi hili kikanda na kushauri zoezi ili liendelee kufanyika
katika mikoa mbalimbali nchini.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Shirika la Haki Ardhi Bi. Gloria Msaki
ameipongeza Wizara na Ofisi ya Msajili wa NGO kwa kujipanga katika zoezi
la uhuishaji wa Taasisi na Mashirika yaliyosajiliwa katika Sheria
nyingine ambayo yanatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho
na Sheria Na. 3/2019.
Akizungumza
katika zoezi hilo Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bi. Vickness Mayao amesema kuwa utaratibu wa usajili
umerahisishwa sana hasa ule wa Mashirika yalikuwa yamesajiliwa katika
Sheria nyingine.
Ameongeza
kuwa Wadau wameridhishwa na huduma zinazotolewa na Ofisi yake na kusema
wanapata mrejesho mzuri kutoka kwa wadau kupitia fomu za mrejesho wa
zoezi hilo.
Ofisi
ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inaendelea na zoezi la
usajili wa Mashirika yaliyosajiliwa awali chini ya Sheria nyingine kama
vile “Societies Act Cap 337” (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch);
“Trustees’ Incorporation Act Cap. 318 (RITA); na The Companies Act Cap
212 (Msajili wa Makampuni-BRELA) ambazo zinatakiwa kujisajili chini ya
Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama
ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019.
Usajili
huu umeanza katika Kanda ya Mashariki (Dar es salaam, Lindi, Mtwara,
Pwani na Morogoro) na Kituo kitakuwa Ofisi za Wizara ya Afya-Dar es
Salaam kuanzia tarehe 10-19/07/ 2019.

Comments
Post a Comment