Wanamgambo 21 wa kundi la kigaidi la Taliban waliuawa na wengine watano kujeruhiwa jana (Alhamisi) usiku nchini Afganistan kutokana na shambulizi la anga lililotekelezwa na jeshi la kitaifa la nchi hiyo, katika mkoa wa Langhman mashariki mwa nchi hiyo, wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imethibitisha leo (Ijumaa).
Kwa mujibu ya wizara hiyo, mmoja wa viongozi wa Taliban Zain-Alabadin, pia aliuawa katika shambulizi hilo, Zain alihusika katika mashambulizi ya kigaidi kwenye mkoa wa Laghman na vilevile mkoa wa jirani wa Nangarhar. Kundi la kigaidi la Taliban, ambalo hutumia maeneo ya mandhari yenye miamba na milima kujificha, hawajatoa maoni yao kwa sasa.
Comments
Post a Comment