Wanamgambo 3 wa kundi la kigaidi la Taliban walipoteza maisha yao na wengine wawili kujeruhiwa jana (Jumanne) nchini Afganistan baada ya shambulizi la anga lililofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo

Wanamgambo 3 wa kundi la kigaidi la Taliban walipoteza maisha yao na wengine wawili kujeruhiwa jana (Jumanne) nchini Afganistan baada ya shambulizi la anga lililofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo
kwa maficho yao katika mkoa wa Zabul kusini mwa nchi hiyo , kauli ya wanajeshi nchini humo ilisema leo (Jumatano).
Kwa mujibu wa kauli hiyo, wanajeshi walikamata jumla ya aina 46 tofauti za bomu zilizotengenezwa nyumbani (IED) ambazo wahandisi hao walizivunja katika kipindi cha masaa ishirini na nne yaliyopita.
Vikosi vya usalama vya Afganistani hivi karibuni vimeongeza shughuli zao za usalama dhidi ya wanamgambo wa Taliban ambao wamekuwa wakijaribu kuchukua maeneo ya bara kabla ya msimu wa baridi.

Comments