Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Watoto nchini Uingereza, Dkt. Naomi Wright
akielekeza namna ya kumhudumia mtoto aliyezaliwa matumbo yakiwa nje.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt.
Zaituni Bokhari akielezea kwa vitendo namna ya kutumia mfuko safi wa
plastiki ili kuzuia upotevu wa maji maji na joto la mwili kwa mtoto
aliyezaliwa utumbo ukiwa nje kabla ya kumpeleka katika hospitali yenye
wataalam bobezi.
Wataalam wa Afya wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa hospitalini hapa leo.
Daktari wa Watoto MNH, Dkt. Neema Bayyo akionyesha jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje.
Dkt. Zaituni Bokhari akishirikiana na Dkt. Neema kuhifadhi matumbo yaliyotoka nje kwa kutumia mfuko maalum (Silo bag).
Dkt.
Bokhari na Dkt. Wright wakielekeza namna mama anavyotakiwa kumbeba
mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje mara baada ya kupatiwa huduma ya
kwanza.
Wataalam
wa Afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo wamejengewa
uwezo ili kuwasaidia kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa
nje.
Ambapo takwimu za Hospitali ya Taifa Muhimbili
zinaonyesha kuwa asilimia 100 ya watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje
hupoteza maisha kutokana na ukosefu wa elimu kwa watoa huduma za afya ya
namna wanavyoweza kutoa huduma ya kwanza kabla ya kumfikisha mtoto
katika hospitali zenye wataalam bobezi.
Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Zaituni Bokhari wakati wakutoa mafunzo hayo
kwa njia ya vitendo yanayolenga kuwafikia watoa huduma za afya katika
hospitali mbalimbali za rufaa ndani na nje ya Dar es Salaam.
“Tunatumaini kuwa mafunzo haya yatasaidia kupunguza vifo vya watoto
wanaozaliwa utumbo ukiwa nje ambapo hadi sasa tayari madaktari na
wauguzi wa MNH-Upanga na Mloganzila wamekwisha kupatiwa mafunzo na
kuanzia kesho tutaanza kuzifikia hospitali mbalimbali za rufaa ndani na
nje ya Dar es Salaam ili kuwapatia mafunzo haya,” amesema Dkt. Bokhari.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto nchini Uingereza,
Dkt. Naomi Wright ametaja nchi nne ambazo zimechaguliwa kwa ajili ya
kutoa huduma kwa watoto hao kuwa ni Tanzania, Ghana, Zambia na Malawi.
“Sababu hasa ya Tanzania kupatiwa mafunzo haya ni kutokana na ongezeko
la vifo vya watoto wanaozaliwa matumbo yakiwa nje ambapo kwa nchi
zilizoko kusini wa jangwa la Sahara ni zaidi ya asilimia 98%,” amesema
Dkt. Wright.
Baadhi
ya mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na jinsi ya kumhudumia mtoto
aliyezaliwa utumbo ukiwa nje, njia sahihi za kutoa huduma kwa mtoto huyo
kwa kutumia mifuko safi ya plastiki na hatua za kufuata wakati wa
kujiandaa kumtoa mtoto katika hospitali aliyopokelewa hadi kumfikisha
katika hospitali yenye wataalam bobezi.






Comments
Post a Comment