Watu 11 walimeteza maisha yao na wengine 15 kujeruhiwa

Watu 11 walimeteza maisha yao na wengine 15 kujeruhiwa jana (Ijumaa) nchini Zimbabwe baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka barabarani katika mji wa Mutoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, afisa wa eneo hilo Robert Muzeziwa aliambia Xinhua.
Kwa mujibu wa Robert, ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka kwa gurudumu la gari hilo. Waliojeruhiwa walikimbizwa kwenye hospitali ya karibu kupata matibabu.
Ajali mbaya za barabara ni jambo la kawaida nchini Zimbabwe na husababishwa na hali mbaya za barabara na kuendesha bila kujali.

Comments