Watu wapatao 7 kutoka familia moja ikiwemo mtoto wa miezi miwili wamepoteza maisha yao jana

Watu wapatao 7 kutoka familia moja ikiwemo mtoto wa miezi miwili wamepoteza maisha yao jana (Jumanne) nchini Brazil baada ya matope kuzika nyumba mbili katika mji wa Recife kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, idara ya wazimamoto katika eneo hilo lilisema.

Kwa mujibu wa wazimamoto hao, hawakuweza kujua sababu ya ajali hiyo kwani matope hayo hayakusababishwa na mvua. Kulingana na majirani wa familia hiyo, mabomba mawili ya maji katika eneo hilo yalikuwa yamepasuka, na kusababisha mafuriko ya maji ambayo vilevile ilisababisha matope hayo.

Comments