Wavuvi 17 wametekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram kusini mwa nchi ya Cameroon siku ya Jumapili (jana), msemaji wa serikali katika eneo hilo alisema leo.
Kulingana na wakaazi wa eneo hilo, wavuvi hao walikuwa wanaendelea na shughuli zao za uvuvi kwenye ziwa Chad wakati Boko Haram waliwazingira na kuwateka nyara na kutoweka nao bila mtu yeyote kujua walipelekwa, huku jeshi la Cameroon likifanya msako wa kuwaokoa wavuvi hao. Kundi hilo limekuwa likilenga maeno hayo haswa msimu huu wa krismasi kulingana na taarifa za vyombo vya usalama. Mwanzoni mwa mwezi huu wa Disemba, Boko Haram iliwateka nyara raia 18 na kisha kuwauwa katika eneo hilo.
Comments
Post a Comment