Waziri Mkuu nchini Libya anayeungwa mkono na shirika la umoja wa mataifa Fayez Serraj ametoa wito kwa nchi za Merikani, Uingereza, Italia, Algeria na Uturuki kuanzisha mikataba ya ushirikiano wa usalama kwa lengo la kulinda mji mkuu wa Tripoli

Waziri Mkuu nchini Libya anayeungwa mkono na shirika la umoja wa mataifa Fayez Serraj hivi jana (Alhamisi) ametoa wito kwa nchi za Merikani, Uingereza, Italia, Algeria na Uturuki kuanzisha mikataba ya ushirikiano wa usalama kwa lengo la kulinda mji mkuu wa Tripoli kutokana na mashambulizi ya magaidi.

Kwa mujibu wa Serraj, magaidi hao haswa al-Qaeda na ISIS, wanaendeleza mashambulizi katika maeneo ya ndani na ya karibu na Tripoli tangu mwezi wa Aprili. Maelfu wa watu waliuawa na takriban watu 120,000 walihamishwa makwao kutokana na vita hizo.
Khalifa Haftar, mmoja wa kamanda wa magaidi hao, alisema jana (Alhamisi) kuwa ameagiza wanamgambo wake kuendeleza hatua yao ya mwisho ya mashambulizi katika mji mkuu huo

Comments