Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu 'apingwa' kwenye uongozi wa chama

Kupingwa kwa uongozi wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ndani ya chama chake cha Likud kunaonekana kama ni majaribu makubwa katika uwepo wake madarakani.

Netanyahu anakabiliana na mpinzani wa muda mrefu Gideon Saar katika uchaguzi wa ndani ya chama chake cha Likud.
Japo Netanyahu anatarajiwa kushinda, uchaguzi huo unawadia wakati ambapo anakumbana na changamoto chungu nzima.
Netanyahau anakabiliwa na mashtaka ya rushwa huku akisubiri uchaguzi mkuu wa tatu wa taifa ndani ya kipindi cha mwaka mwaka mmoja baada ya matokeo katika uchaguzi mara mbili wa awali kushindwa kumpa ushindi wa moja kwa.
Mwanahabari wa BBC mji wa Jerusalem Barbara Plett Usher, anasema kuwa Netanyahu amekuwa akifanya kampeni kwa juhudi zake zote hata ingawa anatarajiwa kupata ushindi kwasababu anachotafuta ni ushindi mkubwa - la sivyo itaonekana kana kwamba nguvu yake katika chama imeanza kudhoofika.
Waziri Mkuu wa Netanyahau bado ana uugwaji mkono mkubwa katika chama cha Likud lakini hii ndio changamoto kubwa ambayo amewahi kukumbana nayo katika kipindi cha miaka 10 madarakani na kunaonesha mgawanyiko uliopo katika chamacha Likud, amesema mwanahabari wa BBC.
Kulikuwa na hali ya kutatanisha kidogo wakati wa mkutano wa kampeni kusini mwa mji wa Ashkelon Jumatano usiku, pale Netanyahu alipoondolewa juu ya jukwaa na walinzi wake baada ya kulia kwa king'ora cha tahadhari ya kutokea kwa shambulio la anga la roketi iliyokuwa imerushwa kutoka Gaza.
Netanyahu
Image caption
Hii ni mara ya pili Netanyahu, ambaye anajiweka kama mtu pekee anayeweka kuleta uthabiti wa kiusalma Israel, amelazimika kutafuta sehemu ya kujihifadhi wakati wa kampeni baada ya kutokea kwa kisa kama hicho Septemba.
Mpinzani wake chamani, Bwana Saar, awali alikuwa waziri katika baraza la mawaziri la Netanyahu na pia ni mtu maarufu na mwenye ushawishi mkubwa kwenye chama cha Likud.
Bwana Saar alionywa kwamba kumpinga Netanyahu kutafanya iwe vigumu kwa chama cha Likud kupata ushindi katika uchaguzi utakaofanyika Machi na huenda kukafanya chama hicho kuwa kwenye upinzani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009.
Matokeo ya kura ya maoni ya hivi karibuni yanaonesha kuwa chama cha Likud kitakuwa na wakati mgumu kukabiliana na chama kikuu cha upinzani cha Blue and White party.
Huu utakuwa uchaguzi wa tatu tangu April mwaka huu, baada ya Netanyahu kushindwa mara mbili kuunda muungano utakaomwezesha kuwa na viti vingi bungeni ili kuendesha serikali.
Pia swali limeibuka la ikiwa ataruhusiwa kuwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ujao au atalazimika kujiuzulu wakati kesi inayomkabili itakapoanza kusikilizwa, jambo ambalo linatarajiwa kuwa mahakama ya juu huenda ikafanya uamuzi huo wiki ijayo.
Netanyahu amekanusha madai ya ufisadi dhidi yake na kudai kwamba kesi hiyo ni njama ya kisiasa.

Comments