Katika maisha yoyote ya ndoa au mahusiano zipo changamoto mbalimbali zinazo sababisha ndoa au mahusiano mengi kufa. Hata hivyo kufa kwa ndoa nyingi na mahusiano hayo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu wengi wamekuwa hawavitilii maanani .
Katika makala hii ya leo ningependa kushiriki pamoja katika kukuletea mambo mbalimbali yanayoweza kufanya ndoa au mahusiano yako yadumu . Mambo hayo ni pamoja na ;
- Hofu ya Mungu . Hakuna ndoa yoyote ile iliyoweza kuwa imara na kudumu ikiwa hakuna hofu ya Mungu baina ya wanandoa . Kama ni kijana mwenye lengo la kuingia kwenye ndoa yakupasa kujilidhisha juu ya mchumba uliyenaye kama ni kweli ana hofu ya Mungu . Starehe ya muda mfupi isikufanye ukajisahau na kuingia kwenye ndoa kwa kukurupuka .
- Mapenzi ya kweli baina ya wapenzi . Ili uweze kudumu katika ndoa au mahusiano yoyote yale , yakupasa kuwa na mapenzi ya dhati kati ya wewe na mwenzi wako . Kutokuwa na mapenzi ya kweli katika mahusiano hudharisha udanganyifu mkubwa na usaliti . Mwisho wa udanganyifu huu ni kupungua kwa mapenzi na hatimaye kuvunjika kwa ndoa au uchumba.
- Uvumilivu kwa mwenzi wako . Moja ya kitu kikubwa sanaa ambacho wengi wetu tunaokuwa katika mahusiano au ndoa ni pamoja na kukosa uvumilivu. Hakuna mahusiano yoyote yanayoweza kudumu pasipo kuwepo na uvumilivu baina yenu . Tumekuwa wepesi kuchukua maamuzi zinapotokea sababu kadha wa kadha hususani kutokuelewana . Ukijaribu kuchunguza yote hayo utagundua kuwa yamepelekewa na wenzi kutokuwa na uvumilivu katika mahusiano yao .
-
Uwezo
wa kujishusha . Jambo hili haswa kwa kiasi kikubwa lipo kwa sisi
wanaume . Imefikia hatua tunakuwa tumekosea wenzi wetu lakini hatuna
kasumba ya kujishusha . Moja ya nguzo imara inayoweza kusaidia kwa kiasi
kikubwa kudumisha mahusiano yenu ni pamoja na kila mmoja wenu kuthamini
uwepo wa mwenzake na kujishusha pale anapoona kuwa amekosea . Kufanya
hivyo kutaepuka kutumia muda mrefu kutatua ugomvi usio kuwa na msingi .
- Hali ya kuishi kwa kuthaminiana . Utu ni kitu muhimu zaidi katika mahusiano . Endapo mahusiano yenu au ndoa yenu itapoteza hali ya utu basi itavuruga mfumo mzima na mwenendo wenu . Katika mapenzi kila mmoja anawajibu wa kujali na kuthamini utu wa mwenzake .
- Hali ya kujengeana misingi imara ya mapenzi mapema . Mahusiano yoyote hudumu ikiwa wapenzi hao wamejengeana misingi iliyoimara katika mahusiano yao. Misingi hiyo iambatane sambamba na kuelezana ukweli pindi unapoona mwenzako haendi sawa . Kuwekana wazi mapema juu ya tabia mnazoona kwenu ni chukizo .
- Kujengeana mipango thabiti juu ya matumizi ya pesa . Hakuna mahusiano yaliyoweza kustawi ikiwa yanaendeshwa pasipo kuwa na mipango thabiti juu ya pesa mnayoingiza . Wanaume wengi huchukia na hata wengine kutokusema wazi pale wanapoona wanawake wao wamezidisha matumizi zaidi ya kipato chao . Mnapokuwa katika mahusiano au ndoa ni wajibu wa kilammoja wenu kuheshimu kipato mnachokipa ikiwa ni pamoja na kuweka mipango madhubuti juu ya namna ya kuziendesha .
Comments
Post a Comment