ZAIDI YA BODABODA 100 ZAKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI RUFIJI

 Kamishna wa Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Kitengo cha Usalama Barabarani ACP Abdil Issango akizungumza na baadhi ya madereva wa pikipiki katika operesheni hiyo.
 Kamishna wa Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Kitengo cha Usalama Barabarani ACP Abdil Issango akizungumza na baadhi ya madereva wa pikipiki ,kushoto kwake ni Mkuu wa usalama  barabarani wilaya ya Mkuranga( DTO) Idwin Kulya 


Na.Vero Ignatus,Rufiji

Zaidi ya pikipiki 100 zimekamatwa katika operesheni ambayo inayofahamika kama hatutaki ajali iliyoendeshwa na jeshi la polisi usalama barabarani mkoa wa Kipolisi Rufiji wilaya ya Mkuranga.

Lengo la operesheni hiyo ni kuwakamata madereva wote wa pikipiki wanao kaidi na kukiuka sheria za usalama barabarani na ikiwemo,ulevi,mwendokasi,kupakia mshikaki na kutokuvaa kofia ngumu

Akizunguza  Kamishna Msaidizi wa polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani ACP Abdil Issango katika eneo la Vikindu wilaya ya mkuranga mkoa wa kipolisi wa Rufiji amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu ndani ya wilaya ya mkuranga,kibiti na Rufiji kwaajili ya kuwakamata madereva wa pikipiki ambao hawafuati na kutii kanuni na tarati bu za usalama barabarani 

Amesema zoezi hili linakwenda sambamba na kuwakamata madereva walevi,ambao hawana leseni,pamoja na pikipiki ambazo zinapakia abiria zaidi ya mmoja kwani ni kosa kisheria.

''Ajali nyingi ni bodaboda na kinachowaua ni mwendokasi,ukizingatia barabara zetu hazina miundombinu mizuri kwa kipindi hiki cha mvua,tutakachokifanya ni kuwakamata na kuwalipisha faini''Alisema Issango.

Ametoa wito kwa madereva wote wa vyombo vya moto wazingatie sheria za usalama barabarani kwa ni mwendo kasi unaua na kila dereva anatakiwa aheshimu sheria amauheshimu wa barabrabara haujalishi anatumia chombo gani hii itasaidia kupunguza ajaali kwani ajali nyingine zinasababishwa na miundo mbinu

''Unapolipita gari jingine lazinma uwe na uhakika unapopita inawezekana kule unapopita miundomninu siyo mizuri hivyo unaporudi unaweza ukasababisha ajali''

Katika kipindi hiku cha sikukuu wazazi wametakiwa kuwa makini na watoto pia wasiwaache watoto watangetange bararabarani hovyo kwenye fukwe za bahari,maeneo yaliyotengwa rasmi kwaajili ya kuogelea,kwani watoto wamekuwa wakipotea,nahata baadhi yao kupoteza maisha kwa kukosa uangalizi wa wazazi

Operesheni hiyo iliyoanza mwanzoni mwa mwezi desemba 2019 ni endelevu hivyo basi jeshi la polisi linawataka madereva kuwa makini siyo kwa hofu ya kukamatwa tu bali kuzingatia sheria ili kuepusha ajali.

Comments