ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUJIFANYA DAKTARI NA KUTIBU WANANCHI

ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUJIFANYA DAKTARI NA KUTIBU WANANCHI

Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji linamshikilia Ismail Onyango (42) kwa kujifanya daktari na kutoa huduma kwa wananchi bila kuwa na cheti chochote cha Taaluma ya Udaktari, Uuguzi wala Utabibu
-
Onyango ambaye amekamatwa baada ya Raia wema kutoa taarifa kwa Kamati wa Ulinzi na Usalama Wilayani Rufiji, amekutwa na vifaa vya hospitali vikiwemo mikasi, mabomba ya sindano na kipimo cha kisukari
-
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Juma Njwayo, mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi na uchunguzi unaendelea ili kubaini watu wengine ambao amekuwa akishirikiana nao
-
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, Onyango aliwalenga zaidi wanawake na amekuwa akitoa huduma za utoaji mimba

Comments