Waziri Mkuu wa Finland Sanna Marin, amependekeza Nchi hiyo kuwa na Siku Nne (4) za kufanya kazi ili wananchi wapate muda wa kutosha kufanya mambo mengine na familia zao
-
Pamoja na pendekezo hilo, Marin pia amependekeza muda wa kazi kupunguzwa kutoka Saa Nane (8) hadi Sita (6) kwa siku ili wananchi waweze kufanya shughuli nyingine za Kijamii
-
Alinikuliwa akisema, “Naamini Wananchi wana haki ya kutumia muda wao mwingi na familia zao, wapenzi wao na mambo mengine katika maisha kama vile 'Hobby' na Utamaduni. Hii itakuwa hatua kubwa kwetu katika Maisha ya kazi”
-
Aidha, Waziri wa Elimu wa Nchi hiyo Li Andersson, ameunga mkono hoja ya Marin na kudai kuna umuhimu mkubwa wa kuruhusu Raia kufanya kazi kwa kiasi
-
Hivi sasa Nchi ya Finland ina utaratibu wa kufanya kazi kwa Saa Nane (8) kwa Siku, na Siku Tano (5) kwa Wiki
Comments
Post a Comment