Fursa ya udhamini wa masomo mwaka 2020-2021 yatolewa Uturuki
Fursa ya udhamini wa masomo kutoka katika taasisi ya waturuki waishio ugenini yatolewa msimu wa mwaka  2020-2021
11.01.2020 ~ 11.01.2020

Fursa ya udhamini wa masomo kutoka katika taasisi ya waturuki waishio ugenini yatolewa msimu wa mwaka  2020-2021.
Kwa wanafunzi kutoka katika pembe nne za dunia wanaotaraji kuendelea na masomo yao nchini Uturuki, fursa mpya ya udhamini wa masomo imetolewa  Januri 10 mwaka  2020.
Taasisi  ya waturuki waishio ugennini YTB imetangaza fursa mpya ya udhamini wa masomo kwa wanafunzi wanoataraji kuendelea na masomo yao Uturuki.
Taasisi hiyo imetangaza kwamba fusra imetolewa rasmi kwa mwanafunzi yeyote anataraji kuendelea na masomo yake nchini Uturuki iwapo atakuwa na vigezo ambavyo vitapelekea kuchaguliwa.
Taasisi ya YTB imefahamisha kwamba wakati wa mahojiano na wanafunzi ambao watakuwa  wamechaguliwa mtihami wa majaribio utahitajika .
Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na udanganyifu katika baadhi ya mataifa.
Nauli ya ndege, kwenda na kurudi hutolewa kwa wanafunzi  ambao wamechaguliwa kudhaminiwa na  taasisi hiyo ya YTB Uturuki.
Mwaka  2019  wanafunzi 146 600 kutoka katika mataifa 167 waliomba udhamini wa masomo nchini Uturuki kupitia taasisi ya YTB.
Kwa maelezo zaidi pitia ukurasa huu   www.turkiyeburslari.gov.tr

Comments