HABARI NA HISTORIA YA VITA KATI YA MTEMI MIRAMBO, WANYIRAMBA NA WARUNDI




HABARI NA HISTORIA YA VITA KATI YA MTEMI MIRAMBO, WANYIRAMBA NA WARUNDI


Mara baada ya Mtemi Mirambo kuwapiga Waarabu wa Tabora , Mtemi Mirambo aliamua kupigana na Mtemi Kiyungi. Mtemi Kiyungi alikuwa Mtemi wa Unyanyembe. Masimulizi juu ya vita hivi yalisimuliwa na Mwan’ilonda wa ardhi ya Ndono karibu na maeneo ya Tabora. Alisimulia kuwa, Mtemi Mirambo alikwenda na jeshi lake na kuvamia ngome ya Mtemi Kiyungi iliyokuwa ukifahamika kwa jina la Ishunula.
Kwanza alianza kwa kushambulia Kijiji ambacho mjukuu wake Mtemi Kiyungi, alipokuwa anaishi. Alivamia kjiji hiko na kukishambulia kisha kuchukua mateka na mali nyingi. Pamioja na kuchukua baadhi ya mateka na mali, ukweli ni kwamba mapigano yalikuwa makubwa sana. Na ilifikia wakati Mirambo na jeshi lake walizidiwa nguvu. Hivyo waliamua kurudi kambini bila kufika Unyanyembe kwa Mtemi Kiyungi ili kuvamia ngome yake ya Ishunula. Kwenye miaka ya 1876, Mtemi Kiyungi alifariki. Na mara baada ya kifo cha Mtemi Kiyungi, ngome ya Unyanyembe ikawa chini ya mwanae aliyejulikana kwa jina la Mtemi Isike( Silanda).
Lakini mara baada ya Mtemi Isike kuchukua ardhi ya Unyanyembe, hali haikuwa shwari. Kwani Mtemi Nungu ( Nyungu Ya Mawe) binamu wa Mtemi Kiyungi alitoka Kiwele na kuja kumshambulia Mtemi Isike kwa lengo la kumtoa kwenye uongozi. Kwa kuwa Mtemi Nungu ya Mawe alikuwa na urafiki mkubwa sana na Mtemi Mirambo, waliamua kuungana na kumshambulia Mtemi Isike. Na ukweli ni kwamba Mtemi Mirambo alikuwa akitamani sana Mtemi Nungu ya Mawe kuwa Mtemi katika ardhi ya Unyanyembe kuliko mpwa wake Isike. Mtemi Mirambo akiwa na wanajeshi wake waliovaa Vifundo miguu vyenye kengele, waliweka kambi karibu na maeneo ya Itetemya na hapa ndipo walipoanzia kuvamia ardhi ya Unyanyembe.
Wanyanyembe ambao walikuwa wakisaidiwa na Waarabu wa tabora, walifanikiwa kupambana na wanajeshi wa Mtemi Mirambo na Nungu ya Mawe ili wasiweze kukamata ngome ya Mtemi Isike. Vita ilikuwa kali sana, na ndio maana vita hivi viliitwa Bulugu wa miyimba, wakiwa na maana ya Vita Ya Vifundo vya Kengele (vilivyofungwa miguuni mwa wanajeshi wa Mirambo

Comments