HISTORIA YA WADOE






HABARI NA HISTORIA ZA KABILA LA WADOE.

 Kabila la Wadoe limetokana na Wanyamwezi (rejea historia ya neno Unyamwezi) ambao waliingia Bagamoyo kama jeshi la kukodiwa na Wamasenga (wenyeji wa maeneo Bagamoyo) kupigana vita na Wakamba kutoka Kenya, waliovamia maeneo ya Saadani kwaajiri ya kuwinda tembo na makazi.. Wakamba walipo ingia maeneo ya Saadani wakawaamuru wenyeji (wamasenga) wauwe wanyama wote lakni wakimuua tembo wapelekewe.
Wakamba waliitaji tendo kutokana na biashara ya pembe za ndovu. Na kwa kuwa Wakamba walikuwa wababe sana Wamasenga walifanya kama walivyoagizwa.
Ukweli ni kwamba, Wamasenga walifanya hivyo mwanzoni lakini baada ya kuona pembe za ndovu zinafaida hawakupeleka kwa Wakamba.Ndio hapo mwanzo wa uadui ukatokea. Wakamba wakamuua mtoto wa kiongozi wa Wamasenga.

Inasimuliwa kuwa Wamasenga walikasirika sana na hawakujua cha kufanya. Ndipo akatokea rafiki wa kiongozi wa Wamasenga mfanyabiashara wa kinyamwezi akamwambia atamletea jeshi na wakaahidiana baada ya vita hilo jeshi litapewa lundo la nguo zenye urefu kama mvinje.
Safari ya jeshi la kukodiwa kutoka unyamwezini likaanza kuja likiongozwa na Mwene Seseme (seseme halole mwenyewe nichechemee nikaone mwenyewe) wakapita katika milima ya Nguu na wakaweka kambi hapo wakaifanya sehemu hiyo kuwa ya ibada.
Katika safari hiyo mama wa kiongozi Mwene Seseme akafariki ambaye ni dada wa mfalme Pazi wa Wazaramo.
Mwene-seseme akaamuru ile maiti iliwe na Wabungu (ni moja ya ukoo ilio kwenye huo msafara ambao ulikuwa ukila watu) kwa lengo kwamba akimzika atapata shida ya kwenda kuomba kwenye kaburi yake lakini akiliwa na Wabungu, Mbungu mmoja akifa ni sawa amekufa mama yake.Mjomba wa Mwene-Seseme (Pazi) kujakusikia dada yake ameliwa hakuzikwa alikasirika na hakutaka wakatune na Mwene Seseme.

Comments