HABARI YA MTEMI MIRAMBO NA MTEMI KASONGERA WA MPIMBWE NA WAMISHIONARI WAWILI
Mara baada ya Mtemi Mirambo kupigana na Wafipa, hali ya utulivu yaani maisha bila vita yalitawala katika ardhi ya Ulyanhulu.Lakini Mnamo mwaka 1880 mtemi Mirambo alisikia kuwa kusini mwa mto Ugala kuna Mtemi anaitwa Takuma. Ukweli ni kwamba Mtemi Mirambo alitamani sana kupigana na Mtemi Takuma.
Hivyo aliamua kukusanya jeshi lake lililokuwa na watu zaidi ya 7000, na kwenda kwenye ardhi ya Mto Ugala. Na mara baada ya kifika maeneo hayo, Mtemi Mirambo na jeshi lake walikuta watu wote wamejificha kwenye misitu na wengine maporini. baada kuona Hivyo, Mtemi Mirambo aliamua kubadilisha mpango wake.
Na ndipo alipomwambia ,Mtemi Simba wa Konongo kuwa, watamshambulia Mtemi Kasongera aliyekuwa akitawala maeneo ya Mpibwe kaskazini mwa bonde la Rukwa. Kutokana na mpango huo, jeshi la Mtemi Simba liiliamua kujiunga na jeshi la Mtemi Mirambo na kuunda jeshi kubwa na imara.
Wakati Mtemi Mirambo na Mtemi Simba wakipanga mipango hiyo. Walipokea ugeni kutoka kwa Mfalme Leopard II wa Uberigiji, uliokuwa ukihusisha Waingereza wawili. Wageni hao walikuwa bwana Carter na Cadenhead. Walikuwa njiani wakitokea kituo cha umoja wa Uberigiji kilichokuwa huko Karema. Malengo yao yalikuwa ni kufika Pwani kwa ajili ya kupokea tembo waliokuwa wakitokea India.
Tembo hao inasemekana waliletwa Afrika kwa ajili ya usafiri kwa wakati ule. Na wazo la kufanya tembo hao kuwa sehemu ya Usafiri ni bwana Carter. Bwana Carter na mwenzie walifika maeneo ya Mpimbwe mnamo mwaka 1880, kwenye mwezi wa sita, kipindi hiko majeshi ya Mirambo na Simba yalikuwa tayari yameshafika kwenye maeneo hayo.
Mtemi Kasongera aliwaomba wazungu hao waweke kambi kwenye eneo lake na wamsaidia kupambana , lakini bwana Carter alikataa. Bwana Carter alidai kuwa ugomvi wao hauhusiani na safari yao, na Hivyo wanapaswa kuondoka eneo hilo kabla ya vita kutokea.
Na ndipo Mtemi Kasongera aliposema kuwa, endepo wageni hao watakaa kuweka kambi kwenye eneo lake, atajua kuwa walikuwa wakimuunga mkono Mtemi Mirambo. Na ndipo bwana carter alipowauliza wapagazi wake juu ya ombi la Mtemi Kasongera, ndipo walipomjibu kuwa, wakubali. Kwani kinyume na hapo watauliwa. Kwa shingo upande bwana Carter na mwenzie walikubali kutia kambi kwenye ardhi ya Mpimbwe.
na ndio ukawa mwanzo wa Kuamzishwa kwa Kituo cha Kimishionari maeneo ya Mpimbwe. Na hivyo Mtemi Mirambo hakuwa na mpango wa kuvamia tena

Comments
Post a Comment