HAKI ZA BINADAMU
Na Wakili Manace Ndoroma
Haki za Binadamu ni nini?
Hizi ni haki ambazo mtu anazipata mara tu anapozaliwa, na anaendelea kuwa nazo
hadi kifo chake. Kwa maneno mengine, kitendo cha kuzaliwa ukiwa mwanadamu na si
kiumbe kingine kinakupa moja kwa moja haki fulanifulani ambazo viumbe vingine
havina. Kwa hiyo, haki za binadamu zipo tu, hata kama hazijaandikwa popote, tofauti na
haki za kisheria ambazo huanza pale sheria husika inapotungwa, na hufika tamati pale
ambapo sheria husika imefutwa.
Mifano michache ya haki za binadamu ni pamoja na haki ya kuishi, haki ya kuwa na
makazi, haki ya kutoadhibiwa bila kusikilizwa, haki ya mtu kwenda anakotaka, haki ya
kutodhalilishwa na kutwezwa kwa utu, haki ya kumiliki mali, nk.
Kutokana na umuhimu wake, katika nchi mbalimbali haki za binadamu zimewekewa
mifumo maalum ya kuzilinda na kuhakikisha hazivunjwi hovyovhovyo. Katika nchi ya
Tanzania kwa mfano, ipo Tume ya Haki za Binadamu na Utwala Bora ambayo iliundwa
mwaka 2001 kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila mtu, awe kiongozi ama raia
anaheshimu haki hizo.
Aidha, Haki za Binadamu zimeingizwa rasmi katika Katiba ya Jamhuri ya Mungano wa
Tanzania. Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wameeleza kwa ufasaha kwamba Katiba
imeingiza vifungu hivyo kwa mkono wa kulia na kuviondoa kwa mkono wa kushoto.
Maana yake ni kwamba katika Katiba hiyo hiyo zipo ibara zinazomhakikishia kila mtu
kulindiwa uhai, heshima na utu wake, lakini katika vifungu hivyohivyo, au vingine katika
katiba hiyo hiyo vinaweka masharti magumu kwa mtu kuweza kufaidi haki hizo
Haki za Binadamu zinatambuliwa ulimwenguni kote. Kilichoisukuma Jumuiya ya
Kimataifa kuhakikisha kunakuwa na mifumo thabiti ya Ulinzi wa Haki za Binadamu ni
mateso na uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu uliofanyika wakati wa vita vya pili vya
Dunia vilivyoanza tarehe 1 Septemba, mwaka 1939 na kumalizika tarehe 2 Septemba,
mwaka 1945. Ni vita vilivyoshuhudia unyama wa hali ya juu unaoweza kufanywa na
mwanadamu dhidi ya mwanadamu mwingine, hususan yule aliye dhaifu kimamlaka,
kinguvu, kiuchumi, kisiasa, nk.
Kwa hiyo, mnamo mwaka 1948 mataifa yapatayo 50 chini ya mwavuli wa Umoja wa
Mataifa yalikutana na kutengeneza orodha ya mambo ambayo yalikuja kufahamaika
kama Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu. Kuanzia wakati huo, kila nchi
ikaendelea kuzilinda haki hizo kwa ama kuzitungia sheria, au kuziingiza katika Katiba za
nchi zao. Mpaka sasa, Tamko hilo limefasiliwa katika lugha zaidi ya 360 duniani kote.
Hata hivyo, miaka mingi kabla ya vita vya pili vya Dunia vilivyoisukuma jumuiya ya
kimataifa kukaa pamoja na kutengeneza tamko la haki za binadamu, tayari katika nchi
ya Uingereza na maeneo mengine kulikuwa kumeshafanyika juhudi kadhaa za
kutambua, kuheshimu na kulinda haki za binadamu tangu karne ya 13
Kwa ujumla, haki za binadamu ni kitu ambacho kila mtu anapaswa kuwa na ufahamu
wa asili wa kujua kama zimevunjwa ama hazijavunjwa. Hata kwa hisia tu. Kwa mfano,
katika hali ya kawaida tunatarajia kwamba ukimwona askari polisi anampiga
mtuhumiwa badala ya kumfumga pingu na kumpeleka kituoni kwa mahojiano ya kina
utafahamu mara moja kwamba jambo hilo si sawa. Vilevile, ukiona mtu amenyimwa
ajira kwa sababu tu ya kabila lake, rangi ya ngozi ama sura yake utafahamu kwamba
jambo hilo si sawa na linafaa kurekebishwa haraka sana.
Pia, haki za binadamu zinaweza kutumika kama kipimo cha ustaarabu ambacho jami
husika imekifikia. Mara nyingi, jamii ambazo hazijastarabika zinaongoza kwa uvunjaji
wa haki hizo, bila kujali kama wahusika ni wasomi ama la.
Haki za binadamu zinahusu usawa, heshima, staha, utu na utashi. Kila mtu anayeamini
anastahili kuheshimiwa anapaswa pia kuheshimu wengine. Halikadhali, kila mtu
anapaswa kulinda uhai na maslahi halali ya watu wengine.
Kutokana na maelezo hapo juu, kila mtu mwenye akili timamu anaweza kujua ni jambo
lipi lenye hadhi ya kuitwa Haki za Binadamu. Kwa ufupi ni kwamba namna rahisi ya
kujua haki za binadamu ni zipi ni kwa kuangalia yale mambo ambayo mwanadamu
anastahili kutendewa kwa sababu tu amezaliwa akiwa binadamu, tofauti na wanyama
wengine.
Tukutane toleo lijalo

Comments
Post a Comment