Historia ya Jiji Maarufu la Dar es Salaam





Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania . Pia ni jina la Mkoa wa Dar es Salaam . Dar es Salaam ni mji mkongwe na wenye mamilioni ya watu katika nchi ya Tanzania. Dar es Salaam ndio mji wenye vitega uchumi vingi na ndio mji unaoangaliwa na watu wengi.Ni mji mkuu wa ki biashara wa Tanzania wakati Dodoma ni makao makuu ya Tanzania tangu mwaka
1973. Mpango wa kuhamishia
serikalimjini Dodoma bado unaendelea, japokuwa bado ofisi nyingi za serikali, ikiwa ni pamoja na
Ikulu , zipo Dar es Saalaam.
Mji una wakazi wapatao 4,364,541 kwa
hesabu ya sensa iliyofanyika katika mwaka wa 2012.


ASILI YAKE


Jiji hili zamani liliitwa Mzizima .
SultaniSeyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabuﺩﺍﺭ ﺍﻟﺴﻼﻡ ( Dār as-Salām ) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).
Dar es Salaam ilichaguliwa na
wakoloniWajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo mpana wa mto Kurasini . Hivyo kuanzia mwaka 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala.
Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu mwaka
1904 viliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya
Tanzania bara ya leo kuwa eneo lindwa la Tanganyika chini ya
Uingereza

Comments