Idadi ya watu waliopoteza maisha yao nchini Indonesia kutokana na mapromoka ya ardhi yaliyosababishwa na mafuriko katika majimbo ya West Java na Banten, imeongezeka hadi 15, msemaji wa idara inayohusika na juhudi za kukabiliana na majanga nchini humo Agus Wibowo alisema.
Kwa mujibu wa Agus, mafuriko hayo yalivuruga shughuli za biashara, huku uhamishaji wa watu walioathirika unaendelea kwa sasa. Mkuu wa shirika linalohusika na majanga katika jimbo la Banten Kaprawi Hari, aliambia Xinhua kwamba mafuriko ya jana (Jumatano) yaliharibu nyumba, shule, madaraja na vifaa vingine vya miundombinu katika eneo hilo.
Kulingana na idara inayohusika na utabiri wa hali ya hewa nchini humo, msimu wa mvua ulianza mnamo Novemba 2019, na utafikia kilele chake mwezi huu (Januari) hadi Machi wa mwaka huu. Indonesia imekumbwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi ya mara kwa mara katika kipindi cha mvua nzito.

Comments
Post a Comment