IRAN: TULITUNGUA NDEGE YA ABIRIA YA UKRAINE KWA BAHATI MBAYA
-
Kiongozi wa Jeshi la Iran amesema kutokana na makosa ya Kibinadamu Jeshi lake liliitungua ndege hiyo iliyoanguka karibu na Mji Mkuu, Tehran na kuua Watu wote 176 waliokuwemo ndani
-
Taarifa iliyosomwa na Chaneli ya Runiga ya nchi hiyo imesema, “Siku ya huzuni. Ripoti ya awali ya ndani ya uchunguzi uliofanywa na Jeshi inaonesha, makosa ya Kibinadamu katika muda wa vurugu zilizosababishwa na Marekani yameleta janga.”
-
Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, kupitia Mtandao wa Kijamii wa Twitter ameandika, “Ni Majuto yetu makubwa, tunaomba msamaha na kutoa rambirambi kwa watu wetu, kwa familia za wahathiriwa wote na kwa Mataifa mengine.”
-
Iran ilikuwa ikipingana vikali kwa siku kadhaa na madai ya kutunguliwa kwa ndege hiyo na moja ya makombora yake ambapo Marekani na Canada kupitia Vyanzo Vyao vya Kijasusi zilidai kuwa wanaamini Iran iliitungua ndege hiyo
-
Raia waliofariki kwenye ndege hiyo iliyoanguka dakika 3 baada ya kuruka ni pamoja na Raia wa Iran 82, Canada 63, Ukraine 11, Sweden 10, Afghanstan 4, Ujerumani 3 na Uingereza 3

Comments
Post a Comment