Kwa mujibu wa Chaneli ya Runinga ya Iran, huku wakiwaita Wanajeshi wa Marekani kama 'Magaidi wa Amerika' imesema 'Magaidi wa Amerika' 80 wameuawa kwenye shambulio leo
-
Ingawa chaneli hiyo haikuonesha kithibitisho chochote kuhusiana na taarifa hiyo, imeongeza kuwa makombora yote 15 yaliyorushwa katika Kambi za Jeshi za Ain al-Asad na Erbil, yamefika
-
Aidha, imeeleza kuwa vifaa vya kijeshi zikiwemo ndege za Marekani zimeharibiwa vibaya na tayari wameshaorodhesha sehemu nyingine 100 za kushambulia iwapo Marekani itajibu mashambulizi
-
Kambi ya Jeshi ya Kimataifa ya Ain al-Asad inayoongozwa na Marekani inajumuisha muunganiko wa vikosi kadhaa vya Majeshi vinavyopambana na Dola Ya Kiislamu huko Iraq
-
Hata hivyo, Denmark (Wanajeshi 130), Norway (Wanajeshi 70), Poland (Idadi ya Wanajeshi haijatajwa) pamoja na Iraq zimesema kuwa hakuna Wanajeshi wao waliouawa au kujeruhiwa
Comments
Post a Comment