JENERALI WA IRANI AUAWA NA VIKOSI VYA MAREKANI



Jenerali wa kikosi maalum cha Quds Force kinachoungwa mkono na jeshi la Mapinduzi la Irani, Qasem Soleimani ameuawa na vikosi vya Marekani katika shambulio la anga “kwa maelekezo ya rais”.

Kiongozi wa Irani, Ayatollah Ali  Khamenei amesema kisasi kitalipwa kwa waliohusika na “uhalifu huo.”

Tukio hilo linazidisha hali ya hofu ya vita inayozidi kukua kati ya Iran na Marekani.


Comments