Kesi ya uhujumu Uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari wa kujitegemea Erick Kabendera imepangwa kusikilizwa hapo kesho katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu majira ya saa tatu asubuhi.
Kabendera anatarajiwa kupandishwa kizimbani huku akiwa anaomboleza msiba wa mama yake aliyefariki siku ya tarehe 31, 2019 akiwa na umri wa miaka 80.
Mama wa Kabendera,Verdiana Mujahwunzi aliyefariki Katika hospitali ya Amana akikokuwa akipatiwa matibabu.
Erick Kabendera anashikiliwa tangu mwezi Julai alipokamatwa na Jeshi la Polisi huku mama yake Mara ya mwisho alisema kuwa anamtegemea mwanaye Kabendera Katika matibabu na baada ya kukamatwa matibabu yake yamekuwa magumu.
Na Katika Kesi hiyo ambayo imetajwa kwa zaidi ya Mara 7 Katika Mahakama ya Kisutu huku upelelezi ukitajwa kuwa bado haujakamilika.
Kabendera anashitakiwa kwa Makosa matatu ya kukwepa kulipa Kodi, Kujihusisha na genge la uhalifu na kutakatisha Fedha Makosa ambayo hayana Dhamana.
#FreeErickKabendera
#JusticeForKabendera
Comments
Post a Comment