Kiongozi mkuu wa Irani khamenei shambulizi kwenye kambi za Marekni, ni kama tumewapiga makofi.

Kiongozi mkuu wa Irani Ayatollah Ali Khamenei hivi leo (Jumatano) aliambia Marekani kutoa wanajeshi wake  katika eneo hilo, masaa kadhaa baada ya Iran kuzindua mashambulizi ya kombora katika kambi mbili za jeshi la Marekani nchini Iraq.

Khamenei alisema shambulizi la makombora la Irani kwenye kambi za Marekni, ni kama  "waliwapiga makofi" usoni.

Walakini, "operesheni za kijeshi za aina hii hazitoshi," na "kilicho muhimu ni kumaliza uwepo wa ufisadi wa Wamarekani katika mkoa huo," alisema.

Comments