Korea Kusini: Waziri wa zamani ashutumiwa kwa makosa ya rushwa

  •  

Waziri wa zamani wa Sheria Cho Kuk ameshtumiwa kwa jumla ya makosa 11 yakiwemo ya rushwa, uzuiaji wa Biashara na kughushi nyaraka na madai mengine yanayohusiana na kashfa dhidi ya familia yake 



Mwendesha Mashtaka amedai ufadhili wa masomo ya Utabibu wa Milioni 6 (Fedha za Korea) alioupata mtoto wa Cho mnano Novemba 2017 hadi Oktoba 2018 ulihusiana na rushwa na kukiuka Kanuni za kupambana na Ufisadi

C8CEDBE7-19B3-473F-BDD5-95E0E9CD3F09.jpeg


Kuhusu uwekezaji wa hisa chini ya majina ya uongo yaliyowekwa na mke wa Cho, upande wa mashtaka umedai kuwa Cho na mkewe walikiuka sheria rasmi ya Maadili ya Umma kwa kuripoti mali zao kwa uongo

Waendesha mashtaka pia wanashuku kwamba Waziri huyo wa zamani na mkewe walihusika na makosa ya kielimu ya watoto wao uvunjivu wa kanuni za fedha

Comments