Leo Katika Historia
Leo Katika Historia
08.01.2020 ~ 11.01.2020
Januari 8 mwaka 1324, Marco Polo , mtoto wa familia moja ya Venisia ya wafanya kazi alifariki akiwa na umri wa miaka 70.
Januari 8 mwaka 1324, Marco Polo alifariki aliwa na umri wa miaka 70, Marco Polo alikuwa msafiri wa kimataifa ambae alikuwa akifahamika kama msafiri mashuhuri . Marco Polo alianza safari zake baada ya baba yake na mjomba wake walipoteuliwa na mfalme Kubilai Khan kumkabidhi barua Papa Gregory wa Tia. Alipata fursa ya kutembelea mataifa mengi katika . Aliporejea Venisia alishiriki katika mapigano dhidi ya wakazi wa Genos na kukamatwa kuwa mfungwa. Ni wakati alipokuwa gerezani ndio aliandika ktabu chake kuhusu safari na maeneo aliotembelea ulimwenguni.
Januari 8 mwaka 1642, Galileo Galilee mwanasayansi wa Italia ambae alikuwa akitambulika kama mmoja mwa waanzilishi wa fizikia na astronomia ambayo ni sayansi ya anga za mbali na sayari alifariki akiwa na umri wa miaka 79. Alihukumiwa kifo na kanisa kwa kusema kuwa dunia inazunguka jua. Alisamehewa baada ya kufuta kauli zake.
Januari 8 mwaka 1916, kikosi cha mwisho cha jeshi la washirika ambacho kilikuwa na lengo la kuendelea kuvamia Uturuki Çanakkale katika vita vya kwanza vya dunia kiliondoka . Siku moja baadae kamanda wa jeshi la tano Otto Liman von Sanders alizungumza karibu na penensula ya Galibolu.
Comments
Post a Comment