Leo Katika Historia
Leo Katika Historia
02.01.2020 ~ 10.01.2020
Januari 2 mwaka 1951, Uturuki ilikuwa mwanachama wa muda wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Uturuli ilikuwa mwanachama wa muda wa baraza la usalama wa Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1954 na mwaka 1961, mwanachama wa muda katika ya mwaka 2009 na mwaka 2010 baada ya kupata kura nyingi.
Januari 2 mwaka 1975, vituo vya habari ambvyo ni matawi ya shiriki la TRT la Uturuki vilitambulishwa baada ya kuanza kupeperusha taarifa zikiwa 3, TRT1, TRT2 na TRT3.
Januari 2 mwaka 1971, ajali iliotokea katika historia ya kabumbu ambayo ilipewa jina la "janga la Ibrox" ilitokea katika mchuano kati ya klabu mbili hasimu za Skotlend Glasgow Rangers na Celtic. Mashabiki 66 walifariki na wengine zaidi ya 200 walijeruhiwa katika mkanyagano uliotokea muda mchache kabla ya mpambano kumalizika.
Januari 2 mwaka 2016, mzozo kati ya Iran na Saudia kwa mara nyingine ulianza. Mzozo huo uliibuka baada ya kuhukumiwa kifo kiongozi wa kishia Ayatullah Nimr al-Bakri ambae alikuwa na umri wa miaka 57, kiongozi huyo alishtakiwa na kutuhumiwa ugaidi. Ubalozi wa Saudia mjini Tehran ulichomwa moto.
Comments
Post a Comment