MABASI YANAYOSAFIRISHA VIFURUSHI BILA LESENI YA TCRA YAPEWA ONYO


-
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kukagua na kusimamia mabasi yote yanayofanya usafirishaji wa Vipeto, Bahasha na Vifurushi bila kuwa na Leseni kutoka Mamlaka hiyo
-
Amedai kuwa, baadhi ya mabasi yameendelea kufanya hivyo licha ya maagizo yake ya awali na kuitaka TCRA kufuatilia suala hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya mabasi hayo
-
Nditiye ametoa maagizo hayo wakati akifungua Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta, na kuwataka wanaofanya hivyo kuacha mara moja na kufuata taratibu ambazo zimewekwa na Mamlaka
-
Naibu Waziri huyo pia ametoa wito kwa Shirika la Posta kuboresha zaidi huduma zao, kwa kuwa kuna mizigo ambayo ni mali ya serikali hivyo ni lazima isafirishwe na Shirika hilo

Comments