Mamia ya waandamanaji, walioshiriki kuomboleza washiriki wa Hashd Shaabi waliouawa katika shambulizi la Marekani nchini Iraq,walivamia ubalozi wa Marekani katik mji mkuu wa Baghdad siku ya Jumanne (jana),afisa wa usalama alisema.
Waandamanaji wengi, wakiwa wamevalia sare za jeshi la Hashd Shaabi, walipiga kelele nje ya ubalozi akiimba itikadi kali za kushutumu mashambulizi ya angani ya vikosi vya Marekani dhidi ya vituo vya Hashd Shaabi.
Maandamano hayo yaigeuka na kuwa vurugu baada ya waandamanaji hao kuteketeza mnara wa walinzi na lango la nje la ubalozi, afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq aliiambia Xinhua kwa sharti la kutokujulikana.
Comments
Post a Comment