Marekani yawataka Wananchi wake kuondoka nchini Iraq kutokana na vurugu zinazoendelea


  •  T

  • Ubalozi wa Marekani nchini Iraq imewataka raia wake wote wanaoishi Iraq kuondoka nchini humo mapema iwezekanavyo kutokana na kuongezaka kwa mvutano na vurugu nchini Iraq

Jumanne iliyopita Waandamanaji walifanikiwa kuvunja ukuta wa Ubalozi huo na kuwasha moto ndani ya Ubalozi ikiwa ni hasira zilizosababishwa na Marekani kuwaua Wapiganaji 24 wanaoungwa mkono na Iran wikiendi liyopita

Ubalozi huo umesema kutokana na Waandamanaji kuendelea kuzingira Ubalozi, huduma zinasitishwa kwa muda usiojulikana na Raia wa Marekani wanatakiwa kutosogea karibu na Ubalozi na Wananchi wanaotaka kusafiri kwenda huko wasitishe

Aidha, mapema leo Rais Trump ametoa amri ya kumuua Kiongozi wa Kikosi cha Quds cha Iran, Qasem Soleimani akiwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, hatua iliyopingwa Spika Nancy Pelosi

Kiongozi wa Kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema kisasi kikali kitalipizwa kwa waliohusika na kumwaga damu za wenzao huku Waziri wa Mambo ya Nje, Javad Zarif akisema ni Uchochezi wa Kishenzi

Comments