Mbeya: Jeshi la Polisi lamkamata wakala wa bima ya GTM baada ya kukumta mihuri 56 ya kughushi ya idara za serikali na ofisi binafsi
- Get link
- X
- Other Apps
Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 17:00 jioni huko maeneo ya Mtaa wa Sokoine uliopo Kata na Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kupata taarifa na kisha kufanya msako mkali na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa pamoja na vielelezo.
Baadhi ya mihuri na nyaraka alizokutwa nazo mtuhumiwa ni kama ifuatavyo:-
1.Mhuri wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kata ya Ruanda,
2.Mhuri wa Afisa biashara wa Halmashauri ya Mbeya,
3. Access Bank Tawi la Mbeya,
4.Mamlaka ya Mapato Mbeya [TRA]
5. Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini,
Aidha mtuhumiwa alikutwa pia na Kompyuta moja aina ya Accer, Stika za bima, Poss Machine na nyaraka mbalimbali vikiwemo vyeti vya wanafunzi ambao vimeghushiwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
KUPATIKANA NA BANGI.
Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamshikilia AGREY MASHAKA MBOTO [25] Mkazi wa Kilambo Wilayani Kyela akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi kavu kilogramu thelathini [30].
Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 14:45 mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanya msako mkali huko Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bangi hiyo
Comments
Post a Comment