MHAMIAJI AJIKATA KOO BAADA YA KUKATALIWA KUINGIA MAREKANI

MHAMIAJI AJIKATA KOO BAADA YA KUKATALIWA KUINGIA MAREKANI
-
Mhamiaji mmoja kutoka nchini Mexico amejichinja baada ya kuzuiwa kuingia Marekani
-
Mwanaume huyo, Raia wa Mexico ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 amejiua mita kadhaa kutoka Daraja la Kimataifa la Pharr – Reynosa, Texas
-
Maafisa wa eneo hilo wamesema, mtu huyo ambaye bado hajatambulika hadi sasa alitoa kisu na kujikata koo baada ya kukataliwa kuingia nchini Marekani

Raia wengi wa Mexico wamekuwa wakikimbilia Marekani wakidai maisha yao yapo hatarini nchini kwao kutokana na uwepo wa makundi ya uhalifu ambayo yamefanya sehemu kubwa ya Mexico kuwa hatarishi
-
Uhamiaji Haramu katika mpaka wa Marekani na Mexico umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa tangu Rais Trump aingie madarakani

Comments