Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake, kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na kugombana na mkeweAngelina Sanga (24) ambapo inadaiwa alimpiga na hivyo umsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake.
Kamanda anasema mara baada ya ugomvi huo, Angelina alisafirishwa hadi hospitali ya Ikonda iliyopo wilayani Makete ambapo baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo uchunguzi wa kitabibu ulibaini kuwa dada huyo alionekana amevunjika mkono na sehemu mbali mbali za mwili wake zilionekana zimeshambuliwa vibaya.
Amesema mwanaume huyo anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi huku taratibu za kisheria zikiendelea
Comments
Post a Comment