Putin ashuhudia majeshi ya Urusi yakifanya mazoezi ya kivita ya kukata na shoka
Ndege za kivita, meli, ndege zisizobeba binadamu, nyambizi na makombora mazito yajaribiwa katika eneo la bahari nyeusi
10.01.2020 ~ 11.01.2020
Rais wa Urusi, Vladmir Putin ameshuhudia mazoezi ya kijeshi na majaribio ya silaha ya pamoja ya majeshi ya Urusi yaliyofanyika katika bahari nyeusi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya Kremlin, Putin alifuatilia mazoezi ya pamoja yaliyofanywa na kikosi cha jeshi la Urusi katika bahari nyeusi na kile cha kaskazini akiwa katika meza ya kuongozea kombora la Mareshal Ustinov katika meli ya kivita.
Putin aliangalia pia ufyatuaji wa makombora yenye kasi zaidi ya sauti, Kalibr sevir na Kinjal.
Katika mazoezi hayo zilishiriki ndege za kivita aina ya Su-30 na Su-24 pamoja na ndege ya ulipuaji wa kimkakati Tu-95. Zilishiriki pia meli zaidi ya meli za kivita 30, ndege zisizobeba binadamu “drone” zaidi ya 40 na nyambizi
Comments
Post a Comment