Na HAKIKA JONATHAN
…SEHEMU YA 01…
Nilikurupuka usingizini, mapigo ya moyo wangu yalienda kasi sana,ndoto niliyoota ilikuwa ya kutisha, sikutamani hata kuelezea. Nilinyanyuka kitandani, nikaisogelea swichi, karibu na mlango, nikawasha taa!
“,Whaaat! wewe ni nani?, ina maana nilikuwa naota ndoto ya kweli! “,niliongea kwa mshangao, binadamu wa kutisha, niliyemuota ndotoni akinikimbiza, alikuwa mbele yangu amesimama,mwanga wa taa kubwa ya umeme ulimfanya aonekane wazi juu mpaka chini,ngozi yake ilikuwa nyeupe kama karatasi,mdomoni alifungwa kitambaa cheupe, kichwani alikuwa na michirizi ya damu.
“,Nimekuja nimekuja nimekuja, nimekuja kuitoa roho yako! “,binadamu yule wa kutisha aliongea, akipiga hatua kunisogelea,ilibidi nifanye kila njia kuiokoa nafsi yangu, nikataka kukimbia, sikuweza, mlango wangu niliufunga kwa funguo kabla ya kulala, isitoshe funguo zilikuwa kitandani, nisingeweza kuzifuata, binadamu yule angenikamata kwa urahisi, aliendelea kutembea taratibu kama roboti kunisogelea, hakutembea kama binadamu wa kawaida, alitembea kwa kujiburuza sakafuni.
“,Mungu wangu, nimekwisha! “,nilitamani ardhi ipasuke niweze kutoka,haikuwezekana.
“,Wewee…e ni nani?, unataka nini kw…angu ……?”,niliuliza huku nikitetemeka,kwa mara ya kwanza nilijikojolea, niliumbuka mwezenu.
“,Naitwaa Tagrisi, mfalme wa ujinini, umenikosea sana, umenikosea, umenikosea, nimekuja kukuua, kukuua! “,nilizidi kuchanganyikiwa,nikalitazama juu mpaka chini, kweli alikuwa jini, alikuwa na kwato nyeusi, nguvu zikaniishia, nikatafakari kosa nililolifanya, sikupata jibu,kwa mbali macho yangu yakaona giza, nikahisi kizunguzungu, nikazimia palepale na kudondoka chini.
…………………………………
02:20pm
Baada ya kuzimia, jini lile lilitoweka,lilitaka kuniuwa mpaka nitakapotambua makosa yangu,makosa ambayo sikuyafahamu. Ghafla fahamu zikanirejea tena, nilikuwa nahema na kupumua kwa kasi, mapigo yangu ya moyo hayakuwa ya kawaida,nikatazamaa juu ya dali sikuona kitu, kulia na kushoto, sikuona kitu, nikatazama chini ya uvungu, sikuona kitu chochote kile, nikaisogelea friji yangu, nikamimina maji kwenye glasi, nikanywa,angalau mwili wangu ukapoa, joto likapungua. Taratibu nikakisogelea kitanda changu, nikalala tena, baada ya dakika tano tu, usingizi mzito ukanichukuwa, nikaanza kuota ndoto nyingine ya kutisha, niliota nikiwa katikati ya msitu, mikono na miguu yangu ilifungwa kwa kamba ngumu ya katani. Jini yule aliyejitambulisha kwa jina la Tagrisi, alikuwa ameshika panga,nyuma yake alikuwa na wafuasi wake, walifanana kwa kila kitu, mavazi yao ya rangi nyeusi, ngozi nyeupe pamoja na michirizi ya damu kichwani.
“,Umenikosea sana, umenikosea sana, lazima ufe, lazima ufe, lazima nyama yako niwapatiee wafuasi wangu, wafuasi wangu ……”,jini aliyejitambulisha mbele yangu kwa jina la Tagrisi aliongea, akanyenyua panga lake kubwa, lililong’aa kutokana na makali yake, alitaka kuninyofoa kiungo kimoja baada ya kingine,akalishusha panga lake kwa kasi ya ajabu aweze kuifyeka shingo yangu.
“,Mamaaaa, nakufaaaa! “,nilipiga kelele, nikakurupuka usingizini kwa mara nyingine tena, licha ya kelele nilizopiga kuwa kubwa, hakuna aliyesikia, mama yangu, baba yangu, pamoja na wadongo zangu wawili wa kike, waliendelea kuuchapa usingizi. Baada ya kukurupuka usingizini kwa wakati mwingine tena, nilijitazama kama nilikuwa nina jeraha lolote, sikuamini kama nilikuwa nimepona kifo, ghafla upepo mkali ukavuma, licha ya kufunga dirisha la chumba changu kwa komeo, lakini lilifunguka, upepo ulikuwa mkali na wa ajabu, radi zikapiga kwa fujo, nikazidi kushangaa,kitendo cha kusikia muungurumo wa radi nyakati za kiangazi ni jambo la ajabu sana, ghafla radi zikatoweka,dirisha likajifunga, likarudi kama lilivyokuwa.
“,Pyuuuuuu, “sauti ambayo sikuielewa ikasikika,Tagrisi alirudi tena, macho yake yalikuwa mekundu, yalizunguka zunguka, hayakutulia sehemu moja, nikashuka kitandani kama umeme,mkononi nilishika funguo, nikaufungua mlango, haukufunguka.
“,Mamaaaa, maaaa, nakufaaaa! “,niliita kwa sauti ya juu, sauti haikutoka.
“,Dadaaaa,Winiii, dada winii, nakufaaaa…!”,nilimuita mdogo wangu kipenzi aje kunisaidia, na yeye hakusikia chochote kile, aliendelea kuuchapa usingizi, pamoja na mdogo wangu mwingine aliyeitwa Bestina.
“,lazimaa ufee, umenikosea, umenikosea, umenikosea, “kiumbe yule wa ajabu alizungumza, akatembea kunisogelea, akijiburuza na kwato zake, sikuwa na cha kufanya, nilimsahau mpaka Mungu, nikajikuta nakaa chini palepale mlangoni, nikajikunja kwa unyonge, nikiwa tayali kwa lolote lile, baada ya sekunde takribani kumi, jini lile lilikuwa mbele yangu, likausogeza mkono wake wa kulia shingoni kwangu, lilitaka kuninyonga kwa kutumia mkono wakee.
“,Pyaaaaa, pyaaaaa …”,lilipigwa na shoti, likautoa mkono wake shingoni kwangu haraka sana, shingo yangu ikabaki na alama za mikono yake iliyojaa damu.
“,umeniumiza, umeniumiza,nitarudi, nitarudi tenaaaa ……”,liliongea na kupotea kama upepo, rozali yangu niliyoivaa shingoni ilimpiga na shoti jini yule, akapotea, nikaibusu,rozali ilikuwa ndiyo mkombozi wangu, ndiyo nikamkumbuka Mungu.
“,Asante Mungu, asante Mungu …”,niliongea, laiti kama ningefanya maombi kabla ya kulala, sizani kama yangenitokea hayo yote, nilifungua mlango, ukafunguka, nikaenda kuwa amsha wazazi wangu niweze kuwasimulia yaliyonikuta.
…………………………………
Raskazoni, Tanga:Masaa sita yaliyopita
Kama ujuavyo siku za wikendi, fukwe za bahari hujaa watu, kila mtu akiwa ameenda kuburudika, wengine walikuwa na wapenzi wao, rafiki zao au wazazi wao. Mimi nilikuwa na rafiki yangu Abdul,wote tulisoma naye kidato cha nne, shule ya sekondari Nguvumali.
“,Hakika! “,Abdul aliniita.
“,Nambie ,acha uogaa wewe, toa jinzi yako na laba uje tuogelee, maji matamu asikwambiee mtu ……”,nilimjibu rafiki yangu Abdul, huku nikiendelea kupiga mbizi kama samaki, nilikuwa fundi wa kuogelea, kiasi kwamba watu wengi walikuwa wamesimama ufukweni wakinitazama, wengine walinihurumia, kwani niliogelea mpaka kina kirefu cha bahari, kisha nikarudi tena.
“,Njoo uonee, nimeokota pete, lazima nikamvishe mpenzi wangu Annety, jumatatu, shuleni …”,Abdul aliongea, niliposikia kuhusu Pete nikashtuka, nikatoka haraka sana ndani ya maji, nilikuwa nimesikia stori nyingi za pete zinazo okotwa ufukweni mwa bahari, kuhusishwa na ushirikina.
“,Usivaaaeee! “,nilipiga kelele, nikamkataza,kisha nikamnyanganya,nilitazama huku na kule, nikaona mawe, nikachukua jiwe moja, pete nikaiweka vizuri juu ya jiwe, nikaiponda ponda, ikasagika kama unga. Kisha nikarudi mahali alipokuwa amesimama rafiki yangu kipenzi, licha ya kutofautiana dini zetu, yeye akiwa muislamu, mimi mkristo, tulipendana sana kama marafiki, urafiki ambao ulihamia mpaka kwa wazazi wetu, wakafahamiana, wakawa marafiki, familia zetu zikageuka kama ndugu wa ukoo mmoja.
“,Usiwe unachukua chukua pete, bangili, cheni au kitu chochote ufukweni, kuna ushuhuda niliwahi kusikia, kijana kama sisi aliokota pete, alipoivaa, akawa amefunga ndoa na malikia wa majini, kuanzia hapo, alifanya tendo la ndoa kila siku na jini hilo,likamtumia kwa muda mrefu mpaka akawa mgumba! “,niliongea, nikamuonya rafiki yangu Abdul.
“,Heeeeee! kumbe ni hivyo, ikawaje? “,Abdul aliniuliza swali, alitaka kujua zaidi kuhusu stori hiyo.
“,Jini lile lilimpatia utajiri na pesa nyingi, likampatia onyo, asije akajaribu kulala na mwanamke mwingine,kwa vile kijana yule alikuwa halipendi, akabahatika kumpenda msichana mmoja, wakafanya naye ngono,hapo ndipo mambo yakaharibika, alioza mwili mzima, ndipo msichana yule akambeba mpaka kanisani kwetu, akasema kila kitu na kutubu dhambi ya uzinzi, mapadri na masista wakafanya maombi, wakamvua pete, akapona na kuwa mzima, mali zake zikatoweka ghafla tu, ndipo alipotoa ushuhuda kanisani …”,nilitoa maelezo marefu, kisha nikashtuka, maji yalikuwa yamefika mahali tulipokuwa tumeketi.
” Maji yameanza kurudi, tuondokeee zetu! “,nilizungumza,upande wa pili tayali askari wa usalama walikuwa wameshaanza kutoa watu ufukweni, kuepusha ajari kutoka na mawimbi ya maji yaliyoanza kusogea majira ya jioni.
“,Sawa rafiki yangu,nimejifunza, kuanzia leo sitaokota chochote kile ufukweni! “,Abdul aliongea, akanishukuru.
“,Kweli kabisa, bila hivyo nitakupoteza, “niliongea, nikavaa, tukatoka ufukweni, tukatembea mpaka eneo la daladala, tukapanda daladala za Nguvumali,tukarudi nyumbani.
…ITAENDELEA…
SITASAHAU
Mtunzi:Hakika Jonathan
…SEHEMU YA 3…
Jpili :7;20am
Wote tulikuwa sebureni, mama na baba walikuwa macho, mimi na wadogo zangu tulikuwa tumelala kwenye sofa. Kwakuwa sikulala vizuri usiku uliopita kwa sababu ya vitisho kutoka kwa kiumbe wa ajabu aliyejitambulisha kwa jina la Tagrisi, usingizi mzito ulinichukua, nikalala fofofo.
Nikiwa nimelala sebureni,nikaota ndoto nyingine tena, ndoto ambayo ilisababisha matatizo makubwa katika maisha yangu, kwa muda mfupi tu.
“,Hakikaa!,Hakikaa!umevunja pete ya ndoa ya binti yangu kipenzi na wa kipekee, umesababisha damu ya mke wangu imwagike! damu ya mke wangu imwagike!, chagua moja, chagua moja, kufa au kuikomboa nafsi yako kwa kumuoa binti yangu …!”,niliota nikiwa ufukweni mwa bahari, pale pale nilipoivunja pete siku moja iliyopita, mbele yangu alikuwa amesimama Tagrisi, mfalme wa ujinini, akiniuliza maswali magumu ambayo sikuwa na majibu ya haraka.
“,Hapana…a, hapa…ana, kuliko kumuoa jini, bora nife. “,nilizungumza kwa kutetemeka, kama Tagrisi alitisha kiasi kile, bila shaka hata mtoto wake alikuwa na sura mbaya, alikuwa anatisha kama alivyo yeye..
“,Binti yangu ni mrembo kuliko warembo wote duniani, duniani,kubali umuowe, uikomboe nafsi yako, nafsi yako! “,mfalme Tagrisi aliongea, akaniomba kwa mara nyingine tena.
“,Nimesemaa sitakiii, usinilazimishe, sitakiiii kuoa shetanii! “,nilifoka, mfalme Tagrisi akakasirika.Akaninyoshea mkono, mkono wake ukatoa radi, zikaupiga mdomo wangu, nikawa bubu pale pale, sikuweza kuongea tena. Akaninyoshea mkono wake wa kushoto, akanipiga na radi zingine miguuni kwangu, miguu yote ikapooza, sikuwa na uwezo wa kutembea tena, nikadondoka chini.
“,Hiyo ni adhabu yako, nakupa masaa ishirini na manne, utafakari maneno yangu, ukikubali kumuoa binti yangu utapona, ukikataa utakufaa! “,mfalme Tagrisi aliongea, upepo mkali ukavuma ufukweni, mawimbi makubwa yakatokea baharini, mfalme Tagrisi akapotea mbele ya macho yangu kama upepo, akaniacha nikigaa gaa na kuugulia maumivu, sikuwa na uwezo wa kutembea wala kuongea.
“,Pa, pa, bhaa, bhaaa!, bhaaa, bhaaa”,nilimuita mama yangu, nikamuita baba yangu,sauti haikutoka vizuri, maneno niliyotamka hayalueleweka na binadamu yoyote yule ambaye hajasomea elimu ya walemavu.Nikafumbua macho,nikashtuka usingizini, nilikuwa sebureni kwetu.
“,Pa, pa, bhaaa, bhaaa! “,nikajaribu tena kuzungumza, nikashindwa, nikajaribu kusimama ili nitembee, nikashindwa,kweli nilikuwa bubu na miguu yangu ilikuwa imepooza, ndoto niliyoiota ilikuwa ya kweli.
“,Mwanangu, umefanya nini?, nini kimetokea? “,mama aliniuliza maswali,huku akinitazama usoni, nilitamani kumjibu na kumsimulia kila kitu, lakini nilishindwa.
“,kaka! kakaa! kakaa! “,vicheko vya wadogo zangu havikuwepo tena, walishtuka usingizini na kukuta hali yangu ikiwa mbaya, wakaanza kulia kwa huzuni, nilitamani niwajibu lakini nilishindwa, nilibaki tu kuwafuta machozi. Baba yangu alikuwa akitembea huku na kule sebureni, hakujua afanye nini ili kurudisha hali yangu kama zamani.
“,Baba Hakika, tumpeleke kanisani mtoto akafanyiwe maombi, hii hali siyo ya kawaida, bila shaka kuna nguvu za kishirikina zinahusika na swala hili.”,mama alizungumza huku akilia…
“,Hapana, tumpeleke hospitali kwanza! “,baba aliongea, ndiyo ilikuwa sauti ya mwisho kwenye familia, licha ya kanisa la katoriki Parokia ya Majani Mapana kuwa karibu na nyumbani, baba alikataa nisipelekwe kanisani, alininyenyua kwa mikono yake miwili, akanipeleka mpaka ndani ya gari letu dogo aina ya Toyota escudo, akanipakia, kisha akarudi ndani, wote wakajiandaa, wakapanda ndani ya gari, baba akiwa ameshika uskani, alikamata barabara kuu ya kuelekea mikoani, barabara ya Kange akitokea kota za jeshi la kutuliza ghasia FFU, akaanza kuelekea katikati ya jiji la Tanga, hospitali kuu ya mkoa ili niweze kupatiwa matibabu. Nilishuhudia kila kitu lakini sikuwa na uwezo wa kuongea na kueleweka..
………… ………………………
Hospitali ya mkoa :8:20am
Daktari alikuwa ameketi kwenye kiti chake, baba yangu alikuwa ameninyenyua kama mtoto mdogo licha ya ndevu nyingi zilizonijaa kidevuni, mama alikuwa amekaa pamoja na wadogo zangu, macho yetu wote yalimtazama daktari.
“,Hana tatizo lolote,lakini sisi hatuamini ushirikina, nawaomba mumpeleke kwenye nyumba za ibada akafanyiwe maombezi! “,dokta aliongea.
“,Umempima vizuri kweli? “,baba aliuliza.
“,Niamini afande, mtoto wako hana tatizo lolote, ni mzima kabisa, mpelekeni tu akafanyiwe maombi kanisani au msikitini! “,dokta aliongea,kama nilivyokueleza baba yangu alikuwa askari maarufu, alijulikana kila mahali, hata dokta alimfahamu,ilibidi anyoshe maelezo vizuri asije akageuziwa kichapo maana tayali baba alikuwa ameshaanza kukasirika,hakuamini kabisa vipimo vya daktari.
“,Bhaaa,bhaa!bhaa!”,nilimuita baba,baba akanitazama,japo hakuelewa nilimaanisha nini,nilimnyoshea mkono daktari,kisha nikatikisa kichwa,niliashiria daktari alikuwa sahihi,nikaomba kalamu kwa ishara,daktari alikuwa ameshika kalamu,akanipatia,nikajiandika kwenye mkono wangu.
“,Mfalme Tagrisi amefanya haya yote”,maneno niliyoandika kwenye viganja vya mkono wangu vilisomeka hivyo,nikamuonesha baba,mama,pamoja na wadogo zangu,wote wakasoma,wakaelewa tatizo langu.
“,Twendeni kanisani haraka sana,bila shaka ibada inaendelea…”,baba aliongea,familia nzima ikatoka katika chumba cha daktari,baba akiwa amenibeba,akanipakia kwenye gari,safari ya kuelekea kanisani ikaanza.
“,Hatuwezi kuelekea kanisani tukiwa na mavazi haya,inabidi tubadirishe nguo!”,mama aliongea,wote tukajitazama,alikuwa sahihi,mimi nilikuwa bado nimevaa bukta ya kulalia,wengine walikuwa wamevalia mavazi yasiyokuwa ya ibada.
…………………………………
Nguvumali:9:30am
Familia nzima ilikuwa katika mavazi ya kufanyia ibada,baba alikuwa amenivalisha nguo,sikuweza kujivalisha nguo mwenyewe,kadiri muda ulivyozidi kwenda,hali yangu ilizidi kuwa mbaya.Maumivu ya miguu yalikuwa makali sana,nilihisi miguu ikiwaka moto.Baba akanipandisha ndani ya gari,familia nzima ikafuatia,ikaingia ndani ya gari,safari ya kuelekea kanisani iweze kuanza.
“,pa,pa,bhaa,bhaaa!”,nilijaribu kuongea nikashindwa,nikaipiga piga miguu yangu kutuliza maumivu,maumivu yalikuwa makali sana,yasiyoelezeka.Macho yangu yalianza kutoa machozi.
“,Washa gari tuondoke,huoni hali ya mwanao inazidi kuwa mbaya?”,mama alimfokea baba.Kwa mara ya kwanza nilimshuhudia mama yangu akitunisha kifua mbele ya baba yangu,baba hakupenda kupelekeshwa na mwanamke hata siku moja,kama nisingekuwa naumwa,basi mama angeambulia makofi,kama sio mawili basi matatu.
“,Huwezi amini mke wangu,gari imegoma kuwaka!”,baba aliongea,huku akijaribu kuwasha tena gari,ikakataa tena na tena!
“,Heeee!Mungu wangu,mwanangu atakufa!”,mama aliongea,alionesha kabisa kukata tamaa,akaanza kuwaza na kuwazua,akapata jibu,akaandika ujumbe kwenye karatasi,akampatia karatasi mdogo wangu aliyeitwa Wini.
“,Mpatie karatasi hii Padri au sista yoyote yule utakayekutana naye mara tu utakapofika kanisani,kisha subili majibu na uniletee ,tufahamu kama amekubali kuja kutupatia huduma ya maombezi nyumbani kwangu!”,mama aliongea ,mdogo wangu akatoka ndani ya gari,akakimbia haraka sana kuelekea kanisani.
“,Bhaaa,bhaaa,bhaaa!”,niliongea kwa huzuni,nikiipiga piga miguu yangu,machozi yakinitiririka,maumivu yalizidi kuwa makali,nilitamani kufa kuliko kuendelea kuishi,baba alininyenyua na kunirudisha ndani,familia nzima ikarudi ndani na kuketi sebureni,kila mmoja akiongea lake.
Baada ya dakika kumi na tano kupita, mdogo wangu Wini alirudi akiwa anahema sana, bila shaka alikuwa anakimbia wakati wa kwenda kanisani kupeleka ujumbe na wakati wa kurudi nyumbani.
“,Mamaaa! mamaaa! nimelitafuta kanisa sijaliona, uwanja wa kanisa nimekuta kiwanja cha mpira! “,mdogo wangu aliongea kwa mshangao, akatufanya tuzidi kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
“,What! una kichaa au? Kanisa hujaliona,limeenda wapi sasa! “,mama aliuliza swali kwa mshangao.
“,Kweli kabisa mama!sisemi uongo”,mdogo wangu aliongea, mama hakuyaamini maneno yake,akaanza kumsogelea mlangoni alipokuwa amesima ili amchape makofi, aliamini hakufika kanisani kutokana na utundu wake.
“,Bhaa, bhaaa, bhaaa”,nilipiga kelele kumzuia mama yangu, akageuka na kunitazama, nikanyosha mkono wangu, nikawaonyesha maandishi niliyoandika nikiwa hospitalini, “Tagrisi amefanya haya yote “,wote wakapigwa na butwaa, wakatambua ni kwanini hata gari liligoma kuwaka.Familia nzima ikapigwa na butwaa, walishindwa wafanye nini ili waweze kuniokoa, kila njia iliweza kugonga mwamba.
…ITAENDELEA …
SITASAHAU
Mtunzi :Hakika Jonathan
…SEHEMU YA 2…
2:40
Nilitoka ndani ya chumba changu kama kichaa,”,Puuuuu! “,niliteleza kwenye sakafu, nikadondoka chini kama mzigo, nikainuka tena, nikausogelea mlango wa wazazi wangu.
“,Ngo, ngo, ngo, mamaaa! “,niligonga mlango, nikamuita mama yangu kipenzi.
“,Ngi, ngo, ngo, babaaa! “,niligonga mlango kwa mara nyingine tena, nikamuita baba yangu.
“,Kuna nini usiku huu? kuna tatizo?, wadogo zako wanaumwa? “,baba aliitika,akaniuliza maswali mengi sana kwa wakati mmoja.
“,Nakufaaa, njoo unisaidiee, nakufaaa! “,nililalamika,sauti yangu ilipenya vilivyo ikaacha mwangwi mkubwa sebureni, niliongea kwa sauti kubwa sana,mama yangu aliyasikia maneno yangu ya kuomba msaada, wote walikurupuka kitandani, wakawasha taa,wakaufungua mlango, wadogo zangu na wenyewe walikuwa tayali mbele yangu, hawakuogopa, walikuwa ni jasiri licha ya kuzaliwa na jinsi ya kike.
“,Mamaaa,babaaa! nimemuonaa jini, ana kwato! ngozi nyeupe, anatishaa sanaa, alikuwa amekujaa kuniuwaa! “,nililalamika sana, mwili wangu ulitetemeka kwa hofu.
“,Hahaaaaaaa! “,wadogo zangu walinicheka sana,waliamini kwa asilimia mia moja nilikuwa nimeota ndoto, hakuna jini yoyote aliyekuwa amekuja kuniuwa.
“,Nyamanza mwanangu usilie, hiyo ni ndoto tu, hakuna atakayekudhuru, Mimi na baba yako tuko hapa! “,mama yangu alinibembeleza,akanibusu kichwani, akanikumbatia.
“,Kwanini mnamcheka kaka yenu?, nyie hamuotagi ndoto mbaya?, poteeni hapa mara moja!, Hakika mwanangu usiwe na wasiwasi, atakayekugusa mimi na yeye, rudi chumbani ukalalee! “,baba aliwafokea wadogo zangu mapacha wasiofanana, wote wakiwa na umri wa miaka kumi na minne, wakafunga midomo yao, wakaanza kurudi chumbani kwao, baba alitisha sana, akikufokea sura yake inakunjamana na kuwa kama simba, aliogopeka sana, hakuna asiye mjua jijini Tanga, alikuwa askari hodari wa kutuliza ghasia (FFU), ukitaka ukutane na kichapo cha baba yangu, andamana! fanya fujo kwenye kumbi za starehe, Chichi, Nyumbani hoteli, Kwetu pazuri au Tanga beach resort,atakuchapa kirungu mpaka ahakikishe huna uwezo wa kufanya fujo tena maisha yako yote.
“,Mtoto wenu mtoto wenu,mtoto wenu,amenikosea sana,amenikosea sana,lazima nimuuwe, lazima nimuuwe! “,sauti nzito ilisikika sebureni, wadogo zangu wakaogopa kuelekea chumbani kwao, wakarudi na kujificha nyuma ya baba.
“,Baba umesikia, sio ndoto!anasema lazima aniuwe,lakini mimi sijui kosa langu! “,niliongea kwa huzuni, mama alikuwa bize akisali rozali, baba aliingia chumbani, akatoka na rungu lake, akasimama mbele yetu, wote kwa pamoja tuliangaza huku na kule, hatukuona mtu yoyote yule, zaidi ya taa ambayo iliwaka na kuzima.
“,wewe ni nani? Mwanangu amekukosea nini? ……”,baba yangu aliuliza,rungu lake lilikuwa mkononi mwake, alikuwa tayali kwa ajili ya kuilinda familia yake.
“,Naitwa Tagrisi, mfalme wa ujinini,mtoto wako amevunja pete yetu, amevunja pete yetu, amevunja pete yetu, lazima afe, lazima afe! “,sauti ya kutisha ilisikika tena, maneno yaliyosikika yalitushtua sana.
“,Peteeee? “,wote tulishangaa.
“,Nimekumbuka, nimekwisha! ,niliivunja pete jana baharini, Abdul aliiokota,akataka kuivaa, nikamkataza,nikaivunja vunja na mawe! “,niliongea huku nikilia kwa huzuni, nilikuwa tayali nimelitambua kosa langu, kifo kilininyemelea,niliwaogopa sana majini pengine hata zaidi ya Mungu, licha ya kumfanyia Mungu dhambi nyingi, alitusamehe, hakuwahi kutuadhibu, lakini majini wakikosewa hawana msamaha, wanalipa kisasi, nikazidi kulia kama mtoto mdogo.
“,paaa! paaaa! paaa! “,radi zilipiga sebureni kwetu, baba na mama wakatukumbatia, kila mmoja alisali kadiri awezavyo,radi zikatoweka, taa ikaanza kuwaka bila kuzima zima,hatukujua jini yule alikuwa ametoweka au alikuwa bado nyumbani kwetu, hakuna aliyerudi tena chumbani, wote tukalala pale pale sebureni, mama na baba wakaa macho mpaka asubuhi.
…………………………………
Bahari ya hindi :Siku mbili zilizopita ;
Mtoto pekee wa kike wa mfalme alikuwa amevunja ungo,shamlashamla ziliendelea,majini wa kike na kiume waliimba, wakacheza, wakala na kunywa. Walikuwa na furaha sana, hasa mfalme Tagrisi pamoja na mke wake, malikia Tagrisa.
“,Shangweee, shangweee,leo ni shangwee katika nchi yetu ya ujinini, binti yangu wa kike, wa kwanza na wa mwisho, ameuaga utoto siku ya leo!, amevunja ungo, tunapaswa kufurahi!,sherehe hii itajumuisha na shughuli zote za yeye kuchagua mchumba! “,mfalme Tagrisi alihutubia viumbe wake, wote wakashangilia, wakainama chini na kumsujudia.
“,Mwanangu kipenzi, hii ni nafasi yako, chagua mchumba kati ya vijana hawa wa kiume! “,mfalme Tagrisi aliongea, vijana hamsini kutoka katika familia mbalimbali zenye vyeo vikubwa katika ufalme huu, walisogea mbele. Mfalme akasubili jibu kutoka kwa binti yake aliyeitwa Nagasina.
“,Pete hii ni ndoa yako, ikipotea! umepoteza mume, itunze mpaka kufa kwako,kijana utakayemchagua, ukimvisha pete hii,atakuwa mume wako mpaka dakika ya mwisho ya kufa kwako! “,Tagrisi aliongea tena, akasimama kwenye kiti chake cha ufalme, akamsogelea binti yake Nagasina, akamkabidhi pete. Nagasina hakujibu chochote kile, machozi yalianza kumtiririka usoni na kudondoka chini, umati wote wa ufalme huu ukapigwa na butwaa!.
“,Hataki kuolewa, hataki ndoa! “,kila mmoja aliongea lake katika ufalme huu,walishangazwa sana na kitendo cha binti mfalme kupokea pete ya ndoa kutoka kwa baba yake, akalia machozi ya huzuni.
“,Babaa!, mama!, nisamehe kama nitakuwa nimekosea,sitaki kuolewa na jini mwenzangu, nawapenda sana binadamu, nataka kuolewa na binadamu, nawapendaaa! “,binti mfalme aliongea na kulia kwa huzuni, mama yake akamuonea huruma Nagasina, wote waliohudhiria sherehe hii wakaanza kudondosha chozi, Nagasina alionyesha hisia kali za mapenzi kwa wandamu, lakini miiko haikuruhusu jini na binadamu kuowana.
“,Mume wangu!, tazama chozi la binti yako, mtoto wako pekee wa kike, niko tayali kufa kama ndoa hii ikisababisha matatizo, nakuomba umruhusu aolewe na mwanaume anayemtaka, niko tayali damu yangu imwagike kwa ajili yake! “,malikia Tagrisa alimuomba mume wake, akapiga magoti, akakubali kujitoa kafara kwa ajili ya penzi la mwanaye.
“,Binadamu ni wabaya! sisi na wao ni maadui,tukivunja miiko hii, yatatokea matatizo mke wangu! “,mfalme Tagrisi alimuinua mke wake,kwani alikuwa amepiga magoti chini ya miguu yake, akamweleza kwa hisia kali za uchungu.
“,Lolote baya likitokea, nife ili laana hii isije ikaangamiza ufalme wetu! “,malikia Tagrisa aliongea.
“,Sawa, nimekubali, navunja miiko ya ufalme wetu, binti yangu Nagasina, nakuomba urushe pete yako juu, itamezwa na samaki na kutemwa ufukweni,pete hii vijana pekee ndiyo wanavutiwa nayo, itakaye mvutia na kuivaa, atakuwa mume wako wa ndoa! “,mfalme Tagrisi aliongea, Nagasina akairusha pete juu, samaki wa ajabu akaidaka, akaimeza, akaenda kuitema nchi kavu, ufukwe wa bahari, raskazoni Tanga.
“,Iyeeeeeeee! “,ufalme wote ukashangilia, kila mmoja alikuwa na shauku ya kushuhudia ndoa ya binti mfalme,akaisubili kwa hamu siku inayofuata aweze kumtambua binadamu atakayeokota pete na kufunga ndoa na Nagasina.
…………………………………
Masaa kumi na mbili yaliyopita ;
Hofu ilitanda, vilio vikatawala ufalme wote wa ujinini, kifo cha malikia Tagrisa kilikuwa cha ghafla na cha kustaajabisha.
“,Mamaa! rudi mama!, ilikuwa ni kosa langu mama!, usife mama! “,binti mfalme Nagasina, alilia kwa uchungu.
“,Usilie mwanangu, asipokufa yeye, ufalme wetu utateketea, tumevunja miiko, pete yako imevunjwa vunjwa na binadamu,anatakiwa afe! lakini atarudi, atafufuka tena baada ya miaka mia moja! “,mfalme Tagrisi aliongea, angalau Nagasina akapata faraja, ipo siku atamuona mama yake kwa mara nyingine tena. …
“,Lazima nilipize kisasi kwa aliyevunja pete, bila hivyo, akubali kukuowa kwa lazima! “,mfalme Tagrisi aliongea, akapotea na kuelekea duniani kumtafuta kijana aliyeivunja pete muhimu kwa maisha ya ndoa ya binti yake Nagasina.
…ITAENDELEA …
Je, Nini kitaendelea? Usikose kila hatua ya simulizi hii,
SITASAHAU
Mtunzi:HAKIKA JONATHAN
…SEHEMU YA 4…
Jumapili :10:20
Muda ulizidi kusonga mbele,hali yangu ilizidi kuwa mbaya,mwili wangu ulitetemeka kama mgonjwa wa degedege,kichwa kilianza kuniuma,nikaanza kukata tamaa, nikashindwa kuvumilia mateso.
“,Mwanangu atakufa, mwanangu jamani! “,mama aliongea, huku akitembea huku na kule sebuleni, baba na yeye hakuwa na uelekeo maalumu, hakujua afanye nini ili aweze kunikoa, alitembea na kupishana na mama sebuleni, mkono wake wa kulia ulikipiga piga kichwa chake, alikuwa akitafakari mambo mengi sana bila majibu yoyote yale.
“,Tagrisi nimekubali, nimekubali, siko tayali kufa, nimekubali! “,nilipiga kelele, kelele ambazo kila mmoja aliyekuwa sebuleni aliweza kuzisikia,nilipotamka maneno hayo, upepo mkali ulivuma, radi zikapiga,nikatoweka sebuleni kama upepo.
“,Hakika! Hakika!, umeenda wapi mwanangu? uko wapi? “,mama aliita, akipapasa sofa bila kuamini alichokiona, sikuwepo mahali nilipokuwa nimeketi,nilitoweka katika mazingira ya kutatanisha.
“,Mwanangu! mwanangu, mwananguuu! “,baba aliita tena, alinitafuta kila kona sebuleni, chini ya sofa, nyuma ya sofa, chini ya meza, kabatini, kila mahali ndugu zangu walinitafuta sikuwepo! nilishuhudia kila kitu walichokuwa wanakifanya,lakini wao hawakuniona, nilitamani niwambie lakini nilishindwa,upepo ulizidi kunipeleka nikatoweka kabisa sebuleni kwetu, upepo ukanipeleka mahali nisipopafahamu.
“,Kakaaaa! kakaaa! “,wadogo zangu walilia,machozi ya huzuni yalinitoka, niliwahurumia sana,wasingeniona tena duniani,upepo ulizidi kunipeleka huku nikishuhudia kila kitu ambacho kiliendelea katika nyumba yetu.
…………………………………
Bahari ya hindi :10:30
Upepo ulinipeleka na kunitupa baharini, wasichana warembo ambao sikutambua idadi yao, wakiwa wamevalia nguo za kanzu nyeupe zilizofunika mpaka miguu yao walinipokea,niliwaogopa sana, kwani hawakuwa binadamu wa kawaida, macho yao hayakutulia sehemu moja, yalizunguka zunguka kama panga boi.
“,Tumekuja kukupokea! karibu kwenye ufalme wetu! “,mmoja kati ya mabinti wale aliongea, akanisogelea, akanivalisha kofia kichwani,nikahisi macho yangu kuwa mapya, sikuona tena kilichokuwa kinaendelea nyumbani,nikasahau kila kitu,nikawa binadamu mpya kabisa.
“,Mimi ni nani, hapa ni wapi? “,niliuliza swali, huku nikiyashangaa mavazi yangu ambayo nilikuwa nimevaa, yalikuwa mavazi ya kifahari yenye mapambo ya kila aina, yalinukia manukato yenye harufu nzuri sana.
“,Hahaaaa,hahaaaa, hahaaa, wewe ni shemeji yetu, mchumba wa Nagasina, binti mfalme wa falme hii ya ujinini, hahahaaa! “,mabinti wale warembo walicheka sana, kicheko cha ajabu ambacho kilisindikizwa na mwangwi,kisha walinipatia jibu la swali langu, wakapiga magoti na kunisujudia, nilikuwa mtu mkubwa kwa muda mfupi tu.
Baada ya kupatiwa majibu ya swali langu, sikuendelea tena kuhoji,binti aliyekuwa amenivalisha kofia aliongoza njia,katika kasri zuri la vioo, kasri ambalo lilipambwa na mapambo ya dhahabu kila mahali. Nilitembea kama mfalme, huku macho yangu yakitazama juu yangu mita ishirini, nikatazam tena mita ishirini kulia n…
SITASAHAU
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
…SEHEMU YA 5…
Kange:
Baba alinyosha barabara kuu ya kwenda mikoani, kuelekea stendi mpya ya Kange,alitumia dakika kumi tu, tayali wazazi wangu walifika mtaa ambao rafiki yangu Abdul alikuwa anaishi na wazazi wake,mbele kidogo na kiwanda kikubwa cha maziwa jijini Tanga, maarufu kama Tanga fresh.
“,What? nikweli au naota? “,baba aliuliza swali, akiwa anapaki gari mahali ambapo kulikuwa na nyumba mzee Saidy, baba yake Abdul.
“,Mbona unashangaa, kuna nini? “,mama alimuuliza baba ambaye alikuwa anatazama mita kadhaa, upande wake wa kulia.
“,Angalia, nyumba ya mzee Saidy haipo, kuna bwawa! “,baba aliongea kwa mshangao,wadogo zangu wote wakatazama mahali ambapo kulikuwa na nyumba ya kina Abdul, baba alikuwa sahihi,hakukuwa na kitu chochote kile zaidi ya bwawa kubwa lililojaa maji, baba alichoka! akachukua kitambaa na kujifuta jasho ambalo lilikuwa linamtiririka mwilini, akatoka ndani ya gari, alikuwa bado haja amini kile alichokuwa anakiona.Familia yote ikatoka ndani ya gari, wakasogea mpaka eneo ambalo kulikuwa na nyumba ya mzee Saidy.
“,Mke wangu, mzee Saidy alikuwa anaishi hapa au tumepafananisha? “,baba aliuliza tena, akiwa anasogelea mpaka eneo la bwawa, akachota maji yake, kweli yalikuwa ni maji.
“,Walikuwa wanaishi hapa mume wangu!, mi naona mauzauza yanazidi kuendelea! “,mama aliongea,akageuka upande wa pili, akamuona kijana mdogo wa kiume,kwa kukadiria, kijana huyu alikuwa na umri kati ya miaka kumi mpaka kumi na miwili, mama akamuita kwa ishara ya mkono, kijana yule akasogea mahali walipokuwa wamesimama wazazi wangu.
“,Ety mtoto! haya maji ya bwawa hili yako hapa tangu lini? nyumba kubwa iliyokuwa hapa na geti jeupe imeenda wapi? “,baba alimuuliza swali kijana mpita njia aliyeitwa na mama,baba aliuliza swali huku akiwa anachota maji kwa mkono wake wa kulia,yakatiririka kupitia viganja vya mkono wake, yakarudi ndani ya bwawa.
“,Hahaaaaa, hahaaaa! ,utakuwa umevuta bangi sio bure! nyumba si hiyo hapo mbele yako! …”,kijana yule alicheka kwa kejeli, akanyosha mkono katikati ya bwawa na kuonesha mahali nyumba ilipokuwepo,hakuwa anadanganya hata kidogo, yeye aliiona nyumba ya kina Abdul, lakini ndugu zangu waliona bwawa kubwa la maji.
” ,Hakuna nyumba hapa! nazani wewe ndiye utakuwa umevuta bangi, siunaona maji haya, siunaona! “,baba aliongea, akiwa amepaniki, akachota maji kwa viganja vyake na kumuonesha kijana yule.
“,Hahahaaa, hahaha, haya siyo maji, ni mchanga, hahaha! “,kijana yule mdogo alicheka sana, baba akaangalia kwenye viganja vyake vya mkono, maji aliyokuwa amechota yaligeuka kuwa mchanga,wote wakashangaa! ghafla hali ya hewa ikabadilika, anga likawa jeusi, wingu la mvua likatanda ghafla, radi zikapiga, upepo mkali ukavuma, walipogeuka na kumtazama yule kijana, alikuwa amebadilika, macho yake yalikuwa kama ya paka, ngozi nyeupe kama karatasi, mdomoni alikuwa amefungwa kitambaa cheupe, kichwani alikuwa na michirizi ya damu, nguo zake zilibadilika, alikuwa amevaa kanzu nyeupe tofauti na mwanzoni alipokuwa amevaa tisheti na jinzi. …
“,Tuondoke! sio salama mahali hapa! “,baba aliongea,wote wakalisogelea gari, baba akafungua milango ya gari kwa rimoti, wote wakaingia ndani ya gari, akawasha gari, likawaka, akaliondoa eneo hili haraka iwezekanavyo, huku akiacha sintofahamu, kwani umati wa watu wengi ulikuwa unawashangaa sana, waliwaona wazazi wangu na ndugu zangu kama vichaa, hawakujua chochote kile ambacho kilikuwa kinaendelea, hawakuona dalili zozote za mnvua, radi wala upepo wowote ule haukuwepo eneo hili, hali ya hewa ilikuwa shwari kabisa.
…………………………………
Bahari ya Hindi:1:20pm
Kansina, kijana hodari wa kiongozi wa cheo cha juu katika ufalme wa ujinini, alikuwa na hasira sana, ndoto zake siku zote aliwaza kumuoa binti mfalme Nagasina, mtoto pekee wa mfalme Tagrisi. Aliamini akimuoa, itakuwa rahisi kwake yeye kukirithi kiti cha ufalme wa ujinini. Siyo yeye tu ambaye alitamani kuingia madarakani, bali hata wazazi wake,walitamani mtoto wao apate nafasi ya kumuoa binti mfalme Nagasina, lakini ndoto zao ziliyeyuka ghafla, Nagasina alipokataa kuolewa na jini mwenzake, akataka kuvunja miiko na kuolewa na binadamu, jambo ambalo lilimgharimu mama yake mzazi kujitoa kafara na kupoteza maisha.
“,Baba, baba, baba, mimi bado nampenda Nagasina, bado nina ndoto ya kuwa mfalme wa ngome yetu, sijakata tamaa!lazima niwatenganishe Nagasina na binadamu aliyemuoa, lazima nimuoe mimi! “,Kansina alipiga magoti mbele ya viti vya wazazi wake, viti vilivyotengenezwa kwa madini ya almasi, Kansina alikuwa na huzuni sana, huzuni ambayo ilisababisha hata wazazi wake wakose furaha.
“,Kansina, Kansina, sipendi kukuona uwe mnyonge! huwezi kuwa mfalme wa ngome hii bila kujitoa sadaka, lazima uwe tayali kuikabili hatari yoyote ile mbele yako, wewe ni shujaa! umepigana vita vingi dhidi ya maadui wa ngome yetu na kushinda vita, acha kulia, acha kulia, acha kulia, nitakusaidia mwanangu, nitakusaidia mwanangu! “,mtunza hazina wa damu na nyama ya binadamu, vitu muhimu kwa ufalme wa ujinini ili waweze kuishi, mzee aliyejulikana kwa jina la Tefrini aliongea,akamnyenyua kijana wake aliyekuwa amepiga magoti mbele yake, akamfuta machozi.
“,Usilie mwanangu, ndoa ya binadamu na jini haijawahi kudumu hata mwezi mmoja! tutakusaidia ili Nagasina awe wako, binadamu hawezi kuwa mfalme wetu! “,mama yake Kansina aliyeitwa Tefrina aliongea.
“,Ina maana mfalme akifa, binadamu, mume wake Nagasina atatutawala? “,Kansina aliwauliza swali wazazi wake, wazazi ambao walikuwa na cheo cha pili kwa ukubwa, baada ya mfalme Tagrisi na malikia Tagrisa, walifuata wao.
“,Ndiyo! lakini haijawahi kutokea na haitatokea binadamu kututawala, tunaomba uanze mipango ya kuelekea duniani ,wapatie msaada wazazi wa mume wake Nagasina ili ndugu yao arudi duniani! “,baba yake Kansina, mzee Tefrini aliongea.
“,Lakini baba, hawezi kurudi duniani bila kuvua kofia ya kijini, asipovua kofia kivuli chake kitarudi lakini mwili halisi utabaki huku! “,Kansina aliongea.
“,Kuhusu kumvua kofia niachie swala hilo mimi mama yako, kesho asubuhi njoo hapa, tutakupatia maelekezo yote uende duniani! “,Tefrina,mama yake Kansina aliongea. Kansina akatabasamu, matumaini yalirejea upya, akawakumbatia wazazi wake, kisha akatoweka mahali alipokufahamu yeye.
…………………………………
Nusu saa iliyopita:
Ndoa kati yangu na Nagasina ilikamilika, bila kujitambua, Nagasina alinichukua mpaka katika chumba cha hanimuni. Chumba ambacho kilikuwa cha ajabu sana, godoro lilizungukwa na maua mekundu yaliyonukia vizuri, vipepeo wazuri waliluka luka kwenye maua hayo na kukipendezesha chumba hiki. …
“,Hakika! wewe ni wangu, watajaribu kukurudisha, lakini hawataweza! “,Nagasina aliongea, huku akinipaka mafuta mgongoni, nilimpenda sana msichana huyu, fikra zangu zote zilitekwa na penzi lake.
“,Wanirudishe wanipeleke wapi?, nani anataka kunirudisha? “,nilimuuliza swali Nagasina, huku tabasamu likinitoka usoni, sikutaka kabisa mtu yoyote yule anitenganishe na Nagasina. …
“,Huu sio wakati sahihi kukueleza, naruhusiwa kukueleza mpaka nitakapopata ujauzito wako”,Nagasina aliongea,nikamkumbatia,wote tukajitupa kitandani,sikuona shida yoyote ile kuzaa na msichana mrembo kiasi kile.
“,Pa,paaa,pa,pa!”,radi zilipiga mara nne mfululizo,Nagasina akajitoa katika mwili wangu akiwa na hasira sana.
“,Kuna nini mpenzi wangu?”,niliuliza swali,huku nikiwa nimechukia sana,pepo la ngono lilikuwa limeshaniteka,nilikuwa najiaandaa kuvunja amri ya sita na binti mfalme wa ujinini aliyeitwa Nagasina.
“,Kuna watu wanatuongelea mabaya,hawapendi mimi na wewe kuwa pamoja,nisubili nikachukue kinga,nitarudi baada ya muda mfupi”,Nagasina aliongea akiwa amekasirika,macho yake mazuri yaligeuka na kuwa ya paka,akainama chini ,akaongea maneno ambayo sikuyaelewa,akapotea mbele ya macho yangu,niliona jambo la kawaida,sikuogopa chochote kile kutokana na kofia niliyokuwa nimevalishwa kichwani,kofia iliyofanana kama kofia za kifalme.
…ITAENDELEA…
SITOSAHAU
Mtunzi:Hakika Jonathan
…SEHEMU YA 6…
Nguvumali :2:00
Wazazi wangu pamoja na wadogo zangu walikosa furaha,tangu asubuhi walikuwa hawajatia chochote kinywani, walikosa hamu ya kula wala kunywa. Walinizoea sana,walizoea vituko vyangu, familia hata siku moja haikukosa furaha kama nikiwepo, kwa muda mfupi tu, pengo langu lilionekana. …
“,Tupumzike, tutafakari vizuri!, siku ya leo ikipita bila mtoto wetu kurudi,itabidi tuwambie ukweli majirani, watusaidie kumtafuta! “,baba aliongea kwa huzuni.
“,Ndiyo mume wangu, sijui mwanangu huko aliko ni mzima au amekufa? eeee Mungu nilindie mwanangu. “,mama aliongea kwa huzuni, akanyenyuka mahali alipokuwa ameketi kwenye sofa, akaelekea jikoni kuandaa chakula, akiwa haamni kile kilichotokea,mtoto pekee wa kiume katika uzao wake alikuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha.
“,Kila wakati mauzauza! hii Tanga jamani,mwaka huu hautaisha bila mimi kuhama, bora nimwache peke yake mume wangu, watoto wangu wawe salama,akipata likizo atakuja kuniona! “,mama aliendelea kuongea,baba akimtazama alivyokuwa anatoweka mbele ya macho yake, alisikia kila kitu, akatikisa kichwa, akajilaza kwenye sofa na kuuchapa usingizi.
…………………………………
Bahari ya hindi;
Machale yalimcheza Nagasina, radi zilizokuwa zinapiga kila wakati akiwa pamoja nami zilimtisha sana, alitambua chanzo cha radi hizo,akamfuata baba yake haraka sana ili aweze kumweleza swala hilo.
“,Nagasina, Nagasina, binti mfalme wa ngome hii tukufu ya ujinini, mbona unahuzuni? “,mfalme Tagrisi alinyanyuka kwenye kiti chake cha kifalme, akamsogelea binti yake aliyekuwa akihuzunika, alionekana kupatwa na matatizo mahali alikotoka.
“,Kuna ndugu zetu hawapendi mimi niwe na furaha, hawataki niwe pamoja na mume wangu kimapenzi, wananisema vibaya,alimanusura nishambuliwe na radi! “,Nagasina alimweleza baba yake ukweli bila kuficha kitu chochote.
“,Nilijua tu, jambo hilo lazima litokee, vijana hamsini kutoka familia za viongozi wa ufalme huu, walitaka kukuchumbia ili iwe rahisi wao kujitwalia kiti cha ufalme,lakini kiti hiki atakipata kijana ambaye amechaguliwa na kupendwa na binti yangu …”,mfalme Tagrisi aliongea, akimfuta machozi binti yake kwa kutumia kanzu yake iliyonukia manukato yenye harufu nzuri sana.
“,Sasa baba unanisaidiaje! mimi bado nina umri mdogo sana, sina nguvu za kupambana na majini wanaonizidi umri, wananguvu kunishinda, wataniuwaa! “,Nagasina aliongea, baba yake akamuelewa, akanyosha mikono yake, ishara ya kuomba kitu fulani, akaongea maneno ambayo aliyaelewa yeye mwenyewe,hayakuwa maneno ya kiswahili wala kiarabu. Alipomaliza kutamka maneno hayo,chupa mbili ndogo zikatokea katika viganja vyake, akatabasamu.
“,Chupa hili jeupe lina poda, nyunyizia poda hii kuzunguka kitanda chenu, na chupa hii ni mafuta ya kujipaka, jipakeni wewe na mume wako kila wakati mpaka chupa litakapoisha! “,mfalme Tagrisi alimpatia maelekezo binti yake Nagasina, Nagasina akapokea chupa alizopewa, akapiga magoti, akaibusu kanzu ya baba yake, kisha akasimama.
“,Sawa baba, nimekuelewa, nitafanya hivyo, asante sana “,Nagasina aliongea.
“,Sawa binti yangu kipenzi, jambo la muhimu kabisa, hakikisha mkufu wa mume wako hautoki shingoni mwake, itakuwa rahisi maadui kuivunja ndoa yenu “,Mfalme Tagrisi aliongea kwa msisitizo, kisha akarudi kwenye kiti chake cha kifalme na kuketi. Nagasina akatikisa kichwa kukubaliana na maneno ya baba yake, kisha akapotea na kurudi mahali alipokuwa ameniacha.
…………………………………
Kichwa changu kilijawa na hasira, nilitamani nimtambue adui yangu aliyetaka kunitenganisha mimi na Nagasina, nilikaa kitandani nikiwa mpweke, kila muda nilisonya, nikakipiga kitanda kwa hasira. Dakika takribani kumi na tano ambazo Nagasina aliniacha kitandani na kufuata kinga dhidi ya maadui zetu, niliziona kama masaa mawili. Ghafla upepo mkali ukavuma, harufu nzuri ya manukato ya Nagasina ikapenya katika tundu za pua yangu, nilipogeuka upande wa pili wa kitanda, Nagasina alikuwa amesimama kwa pozi zuri la kimahaba, mkononi alikuwa ameshika chupa mbili za mafuta, sikutambua alifika muda gani mahali hapa, nikashuka kwenye kitanda, nikamsogelea na kumubusu shavuni, akanikumbatia kwa furaha.
“,Nimetoka kwa baba, kanipatia ulinzi, kasema tujipake mafuta haya kila siku mpaka yatakapoisha, hili chupa lina poda, nitaizungushia kwenye kitanda au mahali popote tutakapokuwepo!,tukifanya hivyo, hakuna adui yoyote atakutoa wewe katika mikono yangu”,Nagasina aliongea na kunibusu tena na tena, kisha akachukua chupa ya poda na kuzungushia sakafuni, kuzunguka kitanda chetu, alipomaliza akapanda tena kitandani, akanivua shati na mimi nikamvua kanzu yake, kila mmoja akampaka mwenzake mafuta ya kinga kwa mahaba yasiyoelezeka, mtoto wa watu nilikuwa nimetekwa na penzi la binti mfalme wa kijini, muda wote nilimuwaza yeye, nilikuwa kama tahira, sikujielewa kabisa.
…………………………………
Tefrina hakuwa na muda wa kupoteza, alianza kazi haraka sana ya kuvunja penzi langu na Nagasina,hakupenda kuona kijana wake Kansina anakosa furaha. Alitambua chumba ambacho mimi na Nagasina tulikuwepo kwa ajili ya hanimuni, akaja ili aweze kujaribu kunivua kofia niliyokuwa nimevalishwa, kofia ambayo ilifuta kumbukumbu zangu zote kichwani mwangu. Hakujua kuwa tayali tulikuwa tumepatiwa ulinzi na mfalme Tagrisi, baba yake Nagasina.
“,Nenda kama nyoka, binti yule ni mdogo, hana nguvu yoyote, mng’ate kwa siri, atapoteza fahamu, kisha kamilisha kazi, mvue kofia mume wake haraka sana! “,Tefrini,mtunza hazina wa nyama na damu katika ufalme huu wa ujinini aliongea, mke wake akakubalina naye, akatoweka na kuelekea katika chumba ambacho mimi na Nagasina tulikuwepo. Dakika mbili zilipita,tatu zikapita, dakika ya nne na yenyewe ikapita, dakika ya tano akarejea tena akiwa amebabuka mwilini.
“,Heeee! mke wangu kulikoni?, hivyo vidonda umevitoa wapi?,mbona umewahi kurudi, umekamilisha kazi”,Tefrini, baba yake Kansina, alimuuliza swali mke wake,alionekana kuwa na wasiwasi sana baada ya kumuona mke wake akiwa na vidonda mwilini,bila shaka alishambuliwa na kiumbe mwenzao mwenye nguvu kuwashinda…
“,Nilifika katika chumba chao,nilipotaka tu kuingia nilipigwa na shoti,naumia mume wangu,nisaidieee!”,Tefrina,mama yake Kansina aliongea kwa uchungu.
“,Hilo ni zindiko,wamepatiwa ulinzi na mfalme Tagrisi,tunapaswa kujua ulinzi waliopatiwa ni wa aina gani,bila hivyo,hatutaweza kumsaidia mtoto wetu kumpata Nagasina,polee mke wangu,muda sio mrefu utarudi katika hali yako ya kawaida,dawa ya kukuponya ni hii fimbo yangu,usiwe na wasiwasi…”,Tefrini aliongea kwa huzuni,akachukua fimbo yake,akamnyoshea mke wake huku akimtamkia maneno ya ajabu aliyoyaelewa yeye mwenyewe,miale ya mwanga ilitoka kwenye fimbo hiyo na kumpiga mwilini mke wake,mama yake Kansina,majeraha yake yakapona palepale.
…ITAENDELEA…
SITOSAHAU
Mtunzi :Hakika Jonathan
.…SEHEMU YA 7…
Jpili; 4;00pm
Huzuni ilitawala nyumbani kwetu, familia nzima ilikuwa kimya,chakula kilipikwa lakini walishindwa kukila, hawakujua nilikuwa mzima au nimekufa. Jambo ambalo liliwafanya wazazi wangu pamoja na wadogo zangu wakose furaha.
“,Ngo, ngo, ngo, hodiii! ngo, ngo, ngo, Hakikaaa! “,ghafla sauti ilisikika, kuna mtu alikuwa anapiga hodi,famili nzima ikasimama, waliitambua vizuri sauti ya mtu aliyekuwa anabisha hodi.
“,Abdul, Abdul, karibu sana mwanangu,”mama alienda kufungua mlango, kama alivyotegemea, aliyekuwa anabisha hodi alikuwa ni rafiki yangu kipenzi Abdul.
“,Kuna tatizo gani? mbona mnaonekana hamna furaha?, Hakika yuko wapi? jana aliniambia atakuja nyumbani kunitembelea, mpaka sasa hajafika, nimeamua nije mwenyewe kumtembelea. “,Abdul aliongea huku akitabasamu,hakujua chochote kile ambacho kilikuwa kimetokea.
“,Abdul amepotea katika mazingira ya kutatanisha, jana mlienda baharini, ukaokota pete ya ajabu, akakunyanganya na kuivunja vunja, ilikuwa ni pete ya majini, ndiyo iliyosababisha matatizo haya yote “,baba aliongea, uso wa Abdul ukabadilika ghafla, tabasamu likatoweka usoni mwake.
“,Unasemaje baba?, mbona sielewi? “,Abdul aliongea kwa mshangao..
“,Jana mlipoenda baharini, aliivunja pete ya majini, hivyo basi, aliambiwa achague kufa au kumuoa mtoto wa kijini,tangu jana usiku ni mauzauza humu ndani, leo asubuhi kaugua ghafla,hospitali tumeenda, lakini hawajaona ugonjwa,turiporudi nyumbani, alipotea ghafla humu ndani,mpaka sasa hajaonekana, tulipokuja kwenu kuomba ushauri, tuliona mauzauza, nyumba haikuwepo, kulikuwa na bwawa la maji!,”baba alimpatia maelezo marefu Abdul, Abdul akazidi kuchanganyikiwa.
“,Kwahyo Hakika haijulikani amepotelea wapi?, ngoja nikawaambie wazazi wangu waje ili tukamtafute “,Abdul aliongea, kisha akatoka haraka haraka na kuelekea nyumbani kwao kuwajulisha wazazi wake kuhusu matatizo yaliyoikuta familia yetu.
“,Sawa mwanangu, fanya haraka tunawasubili, kuwa makini njiani usiumie! “,baba aliongea, Abdul alikuwa ameshatoweka mbele yake, aliondoka akiwa anakimbia,hali ambayo ilimfanya baba awe na wasiwasi.
…………………………………
Bahari ya Hindi:4;15
Tefrini na mke wake Tefrina, walimuita kijana wao Kansina, kuna jambo la muhimu walitaka kumfahamisha. Kansina alikuwa ana furaha sana, alitaka kujua nini kilikuwa kinaendelea ,wazazi wake walimuahidi watalishughulikia swala la kuvunja ndoa yangu na Nagasina, ili aweze kumuowa na kuwa mrithi wa kiti cha mfalme Tagrisi.
“,Mwanangu,mwanangu, mwanangu Kansina, mama yako alikueleza ataenda kumvua kofia mume wake Nagasina, ili kesho uende duniani kuwapatia maelekezo ndugu zake wajue namna ya kumuokoa binadamu mwenzao, lakini imeshindikana! kesho hautaweza tena kuelekea duniani”,Tefrini, baba yake Kansina aliongea.
“,Kwanini baba!,mbona mnanifanyia hivi,hamtaki nimuoe Nagasina?,hamtaki niwe mrithi wa kiti cha ufalme?”,Kansina aliuliza maswali mengi sana,furaha aliyokuwa nayo ilitoweka ghafla kama upepo,hasira zikampanda kichwani,aliwaona wazazi wake kama wasaliti,alifikili wazazi wake hawapendi yeye amuowe Nagasina na kuwa mfalme.
“,Usikasirike mwanangu!,tunapenda sana umuowe Nagasina na kuwa mfalme miaka ijayo,lakini mama yako ameshindwa kumvua kofia binadamu,mume wake Nagasina,wamepatiwa ulinzi,hivyo basi mama yako amejeruhiwa vibaya sana alipojaribu kufanya hivyo,kama siyo hii fimbo yangu yenye nguvu,mama yako angekuwa ameshapoteza maisha yake,mpaka miaka mia moja ijayo ili aweze kufufuka tena”,Tefrini,baba yake Kansina aliongea,lakini kijana wake wa kipekee hakuamini maneno yake,alikuwa amejaa ghadhabu na hasira isiyo kifani.
“,Kama mmeshindwa,mimi naenda mwenyewe,hamuwezi kunisaliti!”,Kansina aliongea kwa hasira,akatoka mbele ya viti vya wazazi wake,akajigeuza nyoka asionekane kwa urahisi,akatoweka kuelekea mahali ambapo mimi na Nagasina tulikuwepo.
“,Kansina!,Kansina!,Kansina usiende,utakufa!huko ni hatari!”,Tefrina,mama yake Kansina alimlilia mwanaye,kijana wake hakuwa na nguvu za kutosha kuhimili nguvu za zindiko ambalo mimi na Nagasina tulifanyiwa ili kutulinda,mafuta tuliyokuwa tumejipaka,pamoja na poda tuliyoizungusha mahali tulipokuwepo vilikuwa na nguvu ya ajabu.
“,Muache akafe! hawezi kutuita sisi ni wasaliti?, hajui ni kiasi gani tunampenda, muache akafe ajifunze! “,Tefrini, baba yake Kansina aliongea kwa hasira, alikuwa amekasilika sana.
“,Baba Kansina, ni maneno gani hayo unaongea, unamuona kabisa mtoto anaenda huko na hana nguvu za kutosha,kijana wetu bado mdogo, atakufa mume wangu! “,Tefrina,mama yake Kansina aliongea huku akilia kwa uchungu.
“,Wewe ndiyo chanzo, umemdekeza sana mtoto, amekosa mpaka heshima kwa wazazi wake, tumemzuia anatuita sisi wasaliti, muache akafe ili ajifunze kuwa sisi ni wazazi wake, tumeona mengi mpaka kufikia hapa tulipo “,baba yake Kansina aliongea, mama yake Kansina akajikuta akiyafuta machozi yake,jambo ambalo mume wake aliliongea lilikuwa na ukweli ndani yake.
…………………………………
Bahari ya Hindi:
“,Paaa, pa, pa! “,radi tatu zilipiga, mara hii radi hizi zilizitoa mpaka cheche za moto, tulishtuka kutoka usingizini, tulikuwa tumejilaza kitandani kimahaba, Nagasina alikuwa amejilaza kifuani kwangu, baada ya shughuli kubwa ya kufanya tendo la ndoa kwa mara ya kwanza, baada ya ndoa yetu kukamilika masaa kadhaa yaliyopita. Alikurupuka kitandani, shuka akalitupa kule, alikuwa na hofu isiyo elezeka, kwa upande wangu sikuogopa kitu chochote kile, kila jambo nililiona la kawaida, sikuwa na akili timamu, nilikuwa kama zuzu, kofia niliyovalishwa kichwani ilinipumbaza.
“,Hii radi siyo ya kawaida!, kuna hatari mahali hapa! “,Nagasina aliongea, macho yake yakiangaza kila kona ya chumba ,alipotazama chini, alitambua chanzo cha radi zilizopigwa,nyoka mdogo wa kijani alikuwa amekauka mwili mzima, aligusa poda iliyokuwa imenyunyiziwa kuzunguka kitanda chetu,akapigwa na radi, akafa palepale. Nagasina akamnyoshea vidole vyake viwili vya mkono wa kulia, umbo la nyoka yule likabadilika, akawa na umbo lake halisi, Nagasina akamtambua.
“,Kansina, kansina, kila siku nakueleza sikupendii! ona sasa umekufa kifo cha kikatili, “Nagasina aliongea kwa huzuni, alimuhurumia sana Kansina, mwili wake ulizidi kubadilika na kuwa wa kutisha, akamnyoshea tena vidole vyake viwili vya mkono wa kulia,mwili wa Kansina ukapotea kama upepo, akafuatia Nagasina, akapotea, sikujua walielekea wapi, nikajilaza tena kitandani kumsubili mpaka atakaporudi.
…………………………………
5:30pm
Filimbi ya dharula ilipigwa, viumbe wote wa ufalme wa ujinini walikusanyika mbele ya viti vitatu vya kifalme, huku pembeni kukiwa na mwili ambao ulikuwa umefunikwa kwa kitambaa chekundu.
“,Tumepatwa na msiba, Kansina amepoteza maisha alipojaribu kutaka kumdhuru mume wake na binti yangu Nagasina, ni majonzi mazito kumpoteza mwenzetu lakini ni fundisho kwa wengine, ndoa ya binti yangu iheshimiwe! “,mfalme Tagrisi aliongea, mwili wa Kansina ukakabidhiwa kwa wazazi wake, kila mmoja akatawanyika, wakiamini Kansina atafufuka tena baada ya miaka mia moja kupita.
…………………………………
“,Miaka mia moja ni mingi mno, lazima tulipize kisasi, tutafanya kila njia mpaka huyu binadamu arudi kwao, lazima tuwakomoe! “,Tefrini na mke wake Tefrina, waliomboleza kifo cha kijana wao Kansina kwa huzuni, huku wakiuhifadhi mwili wa kijana wao katika chumba maalumu kusubili miaka mia moja iweze kupita, aweze kufufuka tena. Waliahidi kulipiza kisasi kwenye familia ya mfalme wao Tagrisi, waliamini mimi kurudi duniani, itakuwa pigo kubwa kwa binti yao Nagasina.
…ITAENDELEA …
SITOSAHAU
Mtunzi:Hakika Jonathan
*SEHEMU YA 8++
Hali ya tahaluki ili ikumba familia ya mzee Saidy, taarifa ambayo mzee Saidy pamoja na mke wake waliipokea kutoka kwa mtoto wao iliwastaajabisha kupita kiasi na hawakumuamini hata kidogo mtoto wao pekee wa kiume.
“, Ndio baba, Hakika kapotea katika mazingira ya kutatanisha, kama nilivyowambia, chanzo ni pete ya ajabu tuliyoiokota jana baharini na yeye akaivunja ili nisiivae na kupata matatizo! “.Abdul alizungumza….
“, Kwahiyo amepotelea wapi?, mbona unanichanganya we mtoto! “,. Mzee Saidy aliongea huku akimtazama usoni kijana wake.
“, Yaaani mimi ndo sjaelewa kabisaa, naona wabwabwanya bwabwanya tu maneno, waeleza hivi waeleza vilee, wageuka huku wageuka kule, hata sikuelewi mwanangu! “.Mama yake Abdul aliongea kwa Kiswahili cha kitanga, uso wake ulijaa hofu na mshangao sana.
“, Najua hamuwezi niamini, tena wameniambia walitaka waje nyumbani kuwaeleza lakini walikutana na mauzauza,nyumba yetu haikuonekana bali walikuta bwawa kubwa la maji,wakaamua kurudi nyumbani “. Abdul aliendelea kueleza na kujikuta akizidi kuwachanganya wazazi wake.
“, Kama wamekutuma uje kutuita,ngoja twende huko nazani watatuelezea vizuri na tutawaelewa! “.Baba yake Abdul aliongea, akavaa kanzu yake, akavaa kofia yake, wote wakatoka nje haraka haraka na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwetu mtaa wa Majani mapana.
***
“,Hapa Tanga hayo mambo yalikuapo zamani sio siku hizi, kwahiyo sina uhakika kama kweli mnayotueleza ni sahihi, hata kama ni sahihi hatuna cha kuwasaidia zaidi ya swala zetu na dua zetu “,.Ilikua ni sauti ya jirani yetu maarufu kama mzee Busha,umaarufu aliojipatia kutokana na kufungasha mzigo mzito katikati ya mapaja yake, alitembea kwa taabu sana lakini hakuonekana kukosa furaha, muda wote alicheka na wenzake kwenye vijiwe vya kahawa bila kujidharau na kujiona tofauti na wenzake.
“, Hayo maneno mimi siwezi kuyaamini, labda mmetoa kafara mtoto wenu ili mume wako apandishwe cheo kazi…….. “,
“,Puuuh, puuuh,”. Sauti za ngumi zilisikika na kufanya eneo lote kutimka vumbi, baba alishindwa kuvumilia kejeli zile kutoka kwa jirani yetu ambaye siku zote alikuwa na maneno mengi, aliongea sana bila kuifikiria, hakutambua kuwa baba alikuwa amechanganyikiwa na mawazo ya kumpoteza mtoto wake kipenzi katika mazingira ya kutatanisha, Kabla hajamalizia sentesi yake alipokea malipo ya kejeli zake kwa kupigwa kichapo kikali bila kutegemea.
“, Nisamehe, nisamehe sana, sitarudia tena! “, jirani yule alipiga kelele za maumivu huku akijutia maneno aliyoyatamka.
“, Mshenzi kabisaa, nitakutoa roho yako mimi! .Baba aliongea kwa hasira,mama akiwa anamvuta mkono wake kuelekea ndani,akafunga na mlango ili baba asiendelee kusababisha balaa mtaani,alitambua kabisa kitendo cha mimi kapotea katika mazingira ya kutatanisha basi kungepelekea baba kuwa na hasira muda wote…
**
Majani mapana:7:30pm
Mzee Saidy, mke wake pamoja na mtoto wao, rafiki yangu kipenzi Abdul waliendelea kutapatapa kuitafuta nyumba yetu bila mafanikio. Walizunguka huku, wakarudi kule,wakarudi tena palepale ambapo waliamini ndiyo mahali ambapo nyumba yetu ilipatikana.
“, Ndio hapa,hapa ndipo nyumba yao ilikuepo, lakini nashangaa kwanini hakuna nyumba yoyote, uwanja ni mweupeee!,nyasi zimeota kama vile hakukua na chochote mahali hapa! “.Mama yake Abdul aliongea kwa mshangao,akizidi kuangaza eneo lote bila mafanikio, uwanja ulikua ni mweupe na hakukua na nyumba yoyote ile…
“,Hapa kuna kitu, sio bure!. Haya mauzauza yananipa tafsiri ya yale ambayo kijana wetu alitueleza, hapa kuna ushirikina sio bure, kuna mambo hayako sawa hata kidogo!. Turudini nyumbani, nitajua namna ya kufanya.! ….”.Baba yake Abdul aliongea,alionekana kutafakari jambo, akatabasamu, bila shaka alipata jibu ya maswali mengi kuhusiana na mauzauza yaliyokua yanatokea. Wote kwa pamoja wakaongozana na kurudi nyumbani kwao, mtaa wa Kange, jijini Tanga.
**
Bahari ya hindi:8:20pm
Tefrini pamoja na mke wake, waliendelea Kujadili namna ya kulipiza kisasi,kila wazo lililowajia kichwani waliliona halifai. Vichwa viliwauma, licha ya nguvu walizonazo lakini wasingeweza kupambana na mfalme Tagrisi ili kuniokoa,hawakua na nguvu kumshinda.
“,Nimepata jibu,nimepata jibu, nimeshatambua namna ya kufanya, hapa lazima yule binadamu arudi kwao, lazima tugawane maumivu. Mimi nimempoteza Kansina,lazima na binti yao Nagasina aumie kwa kumpoteza mume wake”. Tefrini aliongea kwa uchungu mkubwa, sura yake ilikunjamana na kuzidi kutisha, maneno aliyoyaongea hayakua ya utani hata kidogo,alidhamiria kabisa kulipiza kisasi.
“, Nieleze mume wangu, ni mbinu gani hiyo? , maana ninahisi uchungu sana kuona Nagasina anafurahia maisha, wakati mtoto wetu kupoteza maisha, naumia mume wangu, naumia! “.Tefrina, mke wake Tefrini alizungumza kwa uchungu na kupelekea machozi kumchuruzika, sura yake ikabadilika na kuwa ya kutisha, radi zikapiga mara tatu mfululizo na kupelekea giza kutanda eneo lote la bahari kwa sekunde takribani mbili, kisha hali ikawa shwari.
“, Kuna nguvu ya ajabu iliumba ulimwengu, kuna nguvu ya ajabu iliumba binadamu na viumbe vyote vilivyomo duniani, nguvu hiyo hata sisi tunaiogopa na hatuwezi kuishinda daima. Hivyo basi, tukiwasaidia binadamu kufika mahali ambapo wanaweza kusaidiwa na nguvu hiyo, au tukiwasaidia wazazi wa mume wake Nagasina kujitambua basi lazima kijana wao atarudi duniani, kwa sasa akili zao zimefumbwa wanajiona hawawezi kabisa kumsaidia mtoto wao, kumbe wanaweza kabisaa! “. Tefrini alizungumza huku akitabasamu.
“, Nafahamu kabisa kuhusu nguvu hiyo, lakini je, unataka tufanye nini mume wangu? “.Tefrina aliongea na kuzidi kumuuliza maswali mengi mume wake.
“,Namaanisha hivi,wazazi wa mke wake Nagasina wakifika msikitini, kanisani au wakijitambua na kufanya ibada wao wenyewe Kuomba msaada kwa nguvu hiyo basi mtoto wao atarudi duniani, hahahaha, hahaaaa. “.Yalikuwa ni maneno ya Tefrini yaliyosindikizwa na kicheko kilochopelekea hali ya hewa kubadilika,bahari ilichafuka,upepo mkali ulivuma na kuzua hali ya sintofahamu baharini.
“, Ha ha ha ha.”Wote walicheka kwa pamoja, wakakumbatiana na kupotea mahali walipokuwa, walihisi jambo baya lingeweza kutokea na kukwamisha malengo yao.
***
Kitendo cha bahari kuchafuka kilipelekea viumbe wote wa ujinini kuwa na mshangao, walijiuliza maswali mengi bila majibu,siku zote radi zilipiga na mawimbi ya bahari kuchafuka kama wakiwa na huzuni sana au furaha iliyopitiliza, lakini walishindwa kubaini nani alikuwa na furaha au huzuni kati yao, wote walijiona wakiwa na hali ya kawaida.
“, Baba kuna nini?, bahari imechafuka, tumeshindwa kutambua nani miongoni mwetu aliyesababisha bahari kuchafuka, bila shaka aliyesababisha ana nguvu kubwa sana ndiyo maana tumeshindwa kumtambua kama siyo wewe basi ni wasaidizi wako wenye vyeo vya juu sana, fanya haraka baba, bahari imechafuka mawimbi yataharibu himaya yetu! “.Nagasina aliongea, mfalme Tagrisi alichukua fimbo yake, akapiga piga kioo cha meza yake taratibu katika hali ambayo isingeweza kukivunja kioo kile cha ajabu, kisha akasubili jibu, kimya kikazidi, meza haikuonesha jambo lolote lile.
“, Piga filimbi haraka sana, viumbe wote wa himaya yangu wakusanyike mahali hapa! “,.Mfalme Tagrisi alizungumza kwa hasira. Nagasina akafanya kama alivyoagizwa.
DAKIKA TANO BAADAE
” Viumbe wote wapo, isipokuwa viongozi wetu wa ngazi za juu, Tefrini pamoja na mke wake, bila shaka wao ndiyo wamesababisha machafuko haya ya baharini kutokana na hasira na uchungu wa kumpoteza kijana wao mpendwa Kansina. Jambo ambalo linaniumiza, wametoroka, wameelekea duniani bila taarifa,wakirudi watauawa kwa mikono yangu, wasiporudi ndani ya dakika kumi zijazo nitawafuata huko walikoelekea ili nikawazuie kwani jambo wanalotaka kulifanya ni hatari kwa maisha ya binti yangu pamoja na himaya yetu.”Mfalme Tagrisi aliongea, maneno yaliyomchanganya Nagasina pamoja na viumbe wote wa baharini. Kwa upande wangu sikufahamu chochote kile, nilimkumbatia Nagasina na kumfuta machozi kwa mahaba mazito.
“, Hakika, wanafiki wanataka kututenganisha mimi na wewe, wanatuonea wivu… “. Nagasina aliongea kwa huzuni, maneno ambayo yalizipandisha hasira zangu, nilikuwa nimefutwa kumbukumbu zangu, sikujitambua kabisa.
“, Hata wafanye nini, mimi ni wako daima, kamwe hawataweza “.Niliongea maneno mazito yenye upendo, maneno yaliyosindikizwa na mabusu mengi mfululizo.
**ITAENDELEA *
je, Mzee Saidy, baba yake Abdul atafanya nini ili kuzuia mauzauza na Kuweza kujua siri ya yeye na familia yake kushindwa kukutanishwa na familia yetu, je Tefrini na Tefrina wameelekea duniani kufanya nini?, usikose sehemu ijayo
SITOSAHAU
Mtunzi:Hakika Jonathan
**SEHEMU YA 9*
kange:8:40pm
Mzee Saidy pamoja na familia yake, tayali walikuwa wamefika nyumbani kwao. Kila mmoja alikuwa katika mavazi yake ya swala,huku akiwa amepiga magoti kwenye mkeka wake. Mikononi walishika kitabu cha Quran, swala ilianza, kila mmoja alilitaja jina langu zaidi ya mara nne pamoja na maneno kadhaa ya kiarabu.
“, Tumemalza swala yetu, kilichobakia ni kesho asubuhi kurudi nyumbani kwao na wote kwa pamoja kuelekea baharini mahali pete ilipovunjwa “, Mzee Saidy aliongea kwa tabasamu zuri usoni mwake.
“, Lakini je……? “,
‘”, Shiiiiiih, nishaelewa wataka kusema nini, usjali, ondoa wasiwasi kabisa, kesho lazima rafiki yako atapatikana,kesho hata shule usiende, tutaenda pamoja kumtafuta rafiki yako! “, Mzee Saidy alizungumza kumuondoa hofu mwanae.
“, Ndio mwanangu, swala ndio kila kitu mwanangu, rafiki yako atapatikana usjali “, mama yake Abdul hakusita kumtoa hofu mwanae aliyeonekana kudondosha chozi, huku huzuni ikiupamba uso wake kutokana na sintofahamu ya kupotea kwa rafiki yake.
“, Inshallah”, Abdul aliitikia, akakunja mkeka wake, akainuka na kuondoka zake chumbani kwake.
***
Majani mapana:9:08
Familia nzima iliketi kwa mara nyingine tena, kila mmoja alitafakari namna ya kuianza siku ya jtatu kwa kutembelea sehemu mbalimbali kunitafuta, mama alisema twende kanisani, baba yangu na wadogo zangu wakampinga, kila mmoja aliamini mauzauza yange endelea, kama vile awali kanisa hali kuonekana mdogo wangu alipotumwa kumuita padre wa kanisa letu Parokia ya Majani Mapana.
“, Mimi nimewambia hakuna njia nyingine ya Hakika kupatikana kama sio kutanguliza maombi mbele, halafu mbona tangu Abdul apeleke taarifa kwa wazazi wake mpaka sasa hajarudisha jibu,au ndio ule msemo wa wahenga urafiki kwenye raha tu na sio shida? “, mama yangu kipenzi alizungumza kwa sauti ya upole iliyojaa huruma.
“, Ha ha ha ha, ha ha ha ha “, kicheko kizito cha kutisha kilisikika, nyumba yetu ikatikisika,baba akawakumbatia mama pamoja na wadogo zangu kuwalinda huku akiangaza kila kona ndani ya nyumba yetu, batini, kulia na kushoto, nyuma na mbele.
“, Mko sahihi, mko sahihi, maombi pekee ndiyo yatakayo wakomboa, Hakika amefunga ndoa na mtoto wa mfalme wetu wa ujinini, kavalishwa kofia ya ajabu ambayo imefuta kumbukumbu zake zote,fanyeni ibada maana huyo mnayemuomba atawasaidia na ana nguvu kutushinda, Mzee Saidy hajawasaliti, kaja na familia yake hawajaiona nyumba yenu kama nyie mlivyo ikosa nyumba yao, lakini kesho wakija hapa watafika bila kipingamizi chochote kwasababu wamefanya ibada…… “, sauti nzito ya kutisha iliendelea kutoa maelezo mazito yaliyomfumbua kila mmoja katika familia yetu isipokuwa mimi.
“, Wewe ni nani?, na kwanini umeamua kutusaidia? , “baba aliuliza swali.
“, Naitwa Tefrini,natokea ufalme wa ujinini na nina cheo kikubwa huko, lakini nimehatarisha cheo changu na maisha yangu ili niwasaidie nyinyi na kuusaidia ufalme wetu, mtoto wenu ni binadamu, binadamu katusababishia matatizo kila kukicha katika ufalme we….. “,
“, Toka nyumbani kwangu shetani wewe!, huna nafasi katika familia yangu,”mama alijichomoa mikononi mwa baba,alitamka maneno ya ujasiri huku rozali yake akiinyosha na kuielekeza dalini, mahali ambapo sauti ya kutisha ilikuwa ikitokea. Mwanga mweupe wa rozali uliangaza eneo lote la dalini na kusababisha sauti kutoweka ghafla.
Familia yote ilianza ibada, maana mauzauza sasa yalikuwa yamezidi kipimo, hakuna kimbilio lililokuwa limebakia zaidi ya kumtegemea Mungu. Wadogo zangu, mama pamoja na baba ghafla roho ya ujasiri ilijaa ndani ya nafsi zao, hawakuogopa tena!, kila mmoja aliamini wakati wa mimi kupatikana ulikuwa umewadia.
**
Raskazoni Tanga :10:00
Ufukwe wa bahari ya hindi ulikuwa kimya,licha ya giza nene lililopekea eneo hili kutisha sana, lakini kulikuwa na viumbe wawili ambao hawakuwa binadamu wa kawaida, sura zao zilikuwa nyeupe pee,midomo yao ilifungwa vitambaa kuficha meno makubwa yasiweze kuonekana,kila walipotembea walisindikizwa na mikia mirefu kama ya ng’ombe iliyoburutwa na kuacha alama kwenye mchanga mweupe wa ufukweni.
“, Pole mume wangu, siku zote binadamu ni adui zetu, hata uwafanyie wema kiasi gani hawana shukrani, ona sasa walivyokujeruhi “, Tefrina aliongea kwa upole akiwa amemshika vizuri mume wake aliyejeruhiwa kwa mionzi mikali ya rozali kutoka kwa mama yangu.
“, Wako sahihi kabisa, wako sahihi, wana uchungu wa kumpoteza mtoto wao kama ambavyo tunaumia sisi kumpoteza mtoto wetu Kansina, kwahiyo usiwalaumu sana lakini tushukuru lengo letu limefanikiwa”, Tefrini alimwelezea mke wake, kisha wakasimama baada ya kutembea ufukweni kwa dakika takribani tano.
“, Tuachane na hayo! eneo lenyewe ndio hili, na mawe yenyewe yaliyotumika kuvunja pete ndo hayo hapo “, Tefrina alimfahamisha mume wake,mume wake hakuonekana kushangaa, alichukua fimbo yake yenye nguvu zake zote ili ajaribu kuuvuruga uhusiano wangu na Nagasina.
“,Mnataka kufanya nini?,yani mnanisaliti hata mimi mfalme wenu?”, ilikuwa ni sauti nzito iliyoandamana na ngurumo pamoja na radi. Tefrini na Tefrina walitambua kabisa kama mfalme wao Tagrisi angewatafuta muda wowote ule, kwahiyo walikuwa wamejiandaa kwa mapambano.Waligeuka upande ambao sauti ilitokea, walikuwa sahihi kabisa, alikuwa ni mfalme Tagrisi akiliongoza jeshi la takribani askari mia moja.
“, Uliiondoa furaha yetu, na sisi lazima tuiondoe furaha yako, lazima tuiondoe furaha yako, lazima tuiondoe furaha yako kwa kumrudisha binadamu, mume wa binti yako duniani! “,walimjibu mfalme wao, huku Tefrini akiwa ameinyosha fimbo yake tayali kwa mashambulizi.
” Haya kamateni hao wapuuzi,nasema kamateni hao wasaliti! , wasaliti kama nyie zawadi yao ni kifo tu!”,. Tagrisi aliongea kwa hasira, hasira zilizopelekea mawimbi makubwa ya bahari, yakisindikizwa na upepo mkali uliovuma kutoka baharini kuelekea nchi kavu.
***
Bahari ya hindi :10:40pm
Baada ya familia ya rafiki yangu Abdul kufanya swala, pamoja na wazazi wangu kusali na Kuomba ili waweze kutambua mahali nilipo, fikra zangu zilianza kurudi taratibu, huku nikiwa sjielewi elewi.
“, Mdogo wangu Bestina, hapa ni wapi?, mwenzako Wini yuko wapi? ,.
“, Haaaa! mimi siyo mdogo wako, mimi mke wako! weeh vipi, nini kimekupata?, ahaaa, nimepata jibu, nisubili kidogo nikaongee na baba “,. Nagasina aliongea na kuzidi kunichanganya, hakuwa mdogo wangu kama nilivyodhani, alikuwa ni mke wangu, Nagasina alitambua kuna kitu kilisababisha kumbukumbu zangu kuanza kurudi, alitoweka haraka sana kumpatia taarifa baba yake, akiwa hatambui kuwa baba yake, mfalme Tagrisi alikuwa duniani kuwazuia Tefrini na Tefrina kukamilisha visasi vyao na kufanikisha mimi kurudi Duniani.
**ITAENDELEA ***
JE, TEFRINI NA TEFRINA WATAUAWA?, JE, WAZAZI WANGU NA FAMILIA YA MZEE SAIDY WATAFANIKIWA KUNIPATA, USIKOSE SEHEMU YA MWISHO YA HADITHI HII FUPI YA KUSISIMUA.
SITOSAHAU
Mtunzi:Hakika Jonathan
SEHEMU YA 10
Bahari ya hindi:
“Shiit! Baba ameenda duniani, nitafanya nini sasa, Hakika kumbukumbu yake imeanza kurudi, nitamweleza nini, bila shaka hatanipenda tena, atanichukia akitambua ukweli kwamba mimi ni jini,” Nagasina aliendelea kuwaza na kujiuliza maswali mengi yasiyokua na majibu. Alitapa tapa huku na kule akitafakari namna ya kufanya kuzuia kumbukumbu zangu zisirudi, lakini hakuweza, alikuwa na uwezo mdogo kutokana na umri mdogo aliokuwa nao,akabaki ameduwaa tu akimsubili baba yake aweze kurejea.
*
Nagasina tangu aondoke na kuniacha chumbani peke yangu, kumbukumbu zangu ziliendelea kurudi taratibu, nilijiuliza maswali mengi sana yasiyokua na majibu huku moyo wangu ukiwa umejawa hofu na woga uliopelekea mapigo yangu ya moyo kwenda kasi sana.
“, Hapa ni wapi, mbona panatisha kiasi hiki?, inakuaje samaki wanaogelea bila kuingia humu ndani?, ina maana niko chini ya maji?, na yule mwanamke anayeniambia mimi mume wake ameelekea wapi? “, yalikuwa ni maswali mengi kichwani yasiyokua na majibu, niliangaza huku na kule angalau nione mlango wa kutokea, sikuona hata tundu moja!. Jambo ambalo lilizidi kunishangaza sana.
“, Humu nimeingiaje sasa kama hakuna mlango wala tundu lolote lile zaidi ya vioo tu, Mungu wangu! Haya ndio mavazi gani niliyovaa? , au naota mbona sijielewi? “, nilijitazama mara mbili mbili huku nikijishangaa, muda wote nilikuwa sijatambua jinsi nikivyokuwa nimevaa tofauti na binadamu wa kawaida, nilivaa kanzu yenye rangi mchanganyiko, nyeupe nyeusi na nyekundu. Kichwani nilikuwa nimevaa kofia ya kifalme, kofia nzuri sana na ya ajabu. Nikajaribu kuitoa kichwani kwangu niishangae vizuri, nikashindwa!, nikajaribu tena kuivua tena kwa nguvu za mikono yangu miwili, nikashindwa!.
“, Heee! Kofia gani hii!, na mavazi gani haya!. Nitakua naota sio bureeee…… “,niliongea nikiwa nimekata tamaa, nika kaa chini kusubili lolote lile litakalo tokea.
**
Raskazoni Tanga:11:30pm
Askari wa mfalme Tagrisi walimvamia Tefrini pamoja na mke wake, lakini walijikuta wakiteketezwa na kufa pale pale, Tefrini aliionyosha fimbo yake iliyotoa miale ya moto na kuwaunguza askari wote,wakapiga kelele za maumivu. Tagrisi alikasilika sana baada ya kubaki peke yake,akajiandaa kwa mapambano, alijimini kutokana na nguvu nyingi alizonazo kutokana na umri wake mrefu uliomuwezesha kuwashinda maadui zake pamoja na maadui wa himaya yake.
“, Mwisho wako umefika mpuuzi wewe! “, Tagrisi alifoka kwa hasira , sura yake ikabadilika na kuwa ya kutisha, mkia wake ukachomoza na kucheza cheza kwa madoido tayali kwa mapambano.
“, Mimi siyo muoga kama wengine, nitakufa kishujaa pamoja na mke wangu! “, Tefrini aliongea, akiwa amemkinga mke wake asije akadhurika.Aliinua fimbo yake kumnyoshea mfalme Tagrisi,lakini jitihada zake ziligonga mwamba. Fimbo yake ilikuwa na nguvu hafifu mbele ya mfalme Tagrisi, hali iliyopelekea fimbo ya Tefrini kuyeyuka kama mshumaa ndani ya jiko la moto mkali. Kilichofuata ni pigo zito kutoka kwa Tagrisi, aliikunja ngumi yake na kurusha shambulio la moto lililomfanya Tefrini kujikuna kila sehemu za mwili wake huku mwili wake ukimeguka kiungo kimoja baada ya kingine.
“, Mume wangu, usife mume wangu, nakupenda! “, Tefrina, mke wake Tefrini alilia kwa uchungu huku akishuhudia mume wake akipoteza maisha, viungo vyake vikameguka vyote na kupotelea kwenye mchanga.
“, Mume wangu, mume wangu! “, Tefrina aliita huku akifukua mchanga kwa kutumia mkia wake, lakini alichelewa, mume wake alikuwa ameshapoteza maisha na mabaki yake kujichanganya na mchanga.
“, Usilie, utajiumiza bure, sina mke kwa sasa, na wewe huna mume kwa sasa! Kubali uwe mke wangu, bila hivyo nitakuua…. “,.Tagrisi aliongea akiwa amejiandaa kumteketeza Tefrina kama akikataa kuolewa na yeye.
“, Nimekubali! “, Tefrina aliitikia.
“, Umekubali kweli? “, Tagrisi akauliza tena.
“, Ndio Nimekubali, “Tefrina aliitikia huku akijilazimisha kutabasamu, alimpenda sana mume wake lakini hakuwa tayali kufa, aliogopa sana kufa japo baada ya miaka mia moja angefufuka tena. Tagrisi akamkumbatia Tefrina, wakapotea kama upepo na kurudi chini ya bahari.
**
Dakika kumi baadae :
“, Umesema kumbukumbu yake imeanza kurudi?”, Tagrisi alimuuliza mwanae Nagasina, huku mimi nikiwashangaa sana,sikuwafahamu walikuwa ni kina nani kwa wakati huo. Japo nilikili msichana huyu waliyedai ni mke wangu alikua ni mzuri sana. Tagrisi alinishika kichwani, akatamka maneno kadhaa, nikasahau kwa mara nyingine tena kuhusu nyumbani. Hofu na woga vikatoweka….
“, Mke wangu, mbona hauna furaha? “, nilimuuliza mke wangu Nagasina baada ya kumuona analia, machoni alikuwa ana wasiwasi,nilipotazama mbele yangu, baba yake alikuwa mbele yangu amesimama akinitazama.Nikatambua kuna kitu hakikuwa sawa.
“, Kuna binadamu walitaka kukuchukua, hawataki mimi na wewe tuwe pamoja. “Nagasina aliongea kwa upole akiwa amenikumbatia.
“, Usjali mimi ni wako daima! “. Niliongea na kumfuta machozi Nagasina, nilijiona nilikuwa mahali sahihi kabisa, kumbukumbu zangu zilikuwa zimefumbwa kwa mara nyingine tena.
**
Jtatu asubuhi:7:00
“, Hodii “,
“Ngo ngo ngo, Hodii!”, ilikuwa ni sauti ya mlango wa nyumba yetu kugongwa, “, Karibuu”, mama aliitikia na kwenda kufungua,hakuwa mbali na mlango, kwasababu familia nzima ilikuwa sebuleni wakiwa wamejiandaa kuelekea Raskazoni, ufukweni mwa bahari, mahali ambapo niliivunja pete ya ajabu iliyosababisha matatizo makubwa sana.
“, Ooooh, mama Abdul, karibu sana, shemeji karibuni ndani! “, mama alimkaribisha mama Abdul pamoja na mume wake mzee Saidy waliokuwa wameongozana na mtoto wao, ambaye ni rafiki yangu kipenzi, tulisoma pamoja na kucheza pamoja, wengi walimfahamu kama Abdul Saidy lakini mimi nilimwita Neymar kutokana na kipaji chake cha kucheza mpira, yeye aliniita Eric Shigongo kutokana na kipaji changu cha kutunga hadithi na kuhamasisha watu kutimiza malengo yao.
“Poleni na matatizo,Abdul ameshatueleza kila kitu, hakuna muda wa kupoteza,twendeni ufukweni mahali pete ilipovunjwa hapo ndipo tunaweza kuyamaliza haya matatizo. “baba yake Abdul aliongea, familia nzima ikanyanyuka na kuanza safari kuelekea ufukweni mwa bahari, Raskazoni Tanga.
**
Raskazoni :7:20am
“Ndiyo hapa, hapa ndipo alipoivunja pete ya ajabu, na haya ndiyo mawe yaliyotumika kuivunja pete! “, rafiki yangu Abdul aliwafahamisha wazazi wake pamoja na ndugu zangu.
“Na hii michirizi ni ya nini eneo hili?, inaonekana kuna watu walikuwa wanacheza mahali hapa” mama yake Abdul alijaribu kudadisi.
“Hapa ni ufukweni, wanakuja watu wa kila aina, tufanye kilichotuleta kisha tuondokeee, mengine hayatuhusu kwa sasa! “, baba aliongea maneno yasiyo ya kistarabu siunajua maafande, yaani kila kitu kijeshi! hakuna muda wa kupoteza. Mzee Saidy walitoa mikeka, vitabu vyao vya Qur’an na kuanza kufanya swala, na wazazi wangu wakatoa Biblia zao na kuanza kufanya sala, kila familia ilifanya maombi kulingana na imani yake.
“Amen! “, sote tuliitikia.
“, Amen “, niliitikia nikiwa mbele yao, fahamu zangu zilikuwa zimerudi, nilikuwa vile nilivyokuwa kipindi napotea, mavazi yalikuwa ni yale yale. Siku tambua nilifika vipi mahali pale, lakini nilitambua nini kilichokuwa kimenikuta kutokana na maombi.
“, Mama nilikuwa nimemuoa jini, nilikuwa sijitambui, lakini asanteni kwa sala zenu nimekua mzima tena! “, wote walishangazwa sana, walitabasamu na kunikumbatia kwa furaha. Walinisimulia kila kitu kilicho endelea baada ya mimi kupotea, jinsi walivyosumbuka kunitafuta, mauzauza waliyo kutana nayo na mimi nikawasimulia yale niliyokumbana nayo himaya ya ujinini na kuwafanya watokwe na machozi ya furaha, hawakuamini kama walinipata tena!
***
Bahari ya hindi :
“, Baba, Hakika ametoweka! sijui kaelekea wapi, kapotea ghafla!”, Nagasina alimuuliza baba yake kwa mshangao.
“Hakika amerudishwa duniani na ndugu zake, na hautaweza kuolewa na binadamu tena!, nitakutafutia mchumba wa hapa hapa, kama unaitakia mema himaya hii naomba ukubali mwanangu, bila hivyo ni hatari kwa himaya yetu, siunaona damu nyingi imemwagika mpaka sasa, haiwezekani tena wewe kuolewa na binadamu, nasema haiwezekani! “,.Mfalme Tagrisi alimwelezea ukweli binti yake bila kumficha, japo Nagasina aliumia sana, lakini hakuwa na jinsi, ilibidi anisahau na afute ndoto zake za yeye kuolewa na binadamu.
**MWISHO *
Comments
Post a Comment