TAMWA imesaidia katika kubadili sheria zinazomkandamiza mwanamke Zanzibar- Bi. Issa

 
Dkt. Mzuri Issa, mkurugenzi wa chama cha waansihi wa habari nchini Tanzania tawi la Zanzibar wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili.si

 
Wakati tulipoanzisha chama cha wandishi wa habari wanawake, TAMWA visiwani Zanzibar nchini Tanzania kulikuwa na matukio mengi ya ukatili wa wanawake ambapo vyombo vya habari wakati huo havikuripoti na mbaya zaidi mtazamo wa jamii ukimwelekezea mwanamke lawama.
Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa TAMWA visiwani Zanzibar Dkt. Mzuri Issa katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akiwa jijini New York Marekani, Bi Issa ametolea mfano wa sheria ambayo ilikuwa ikimkandamiza mtoto wa kike ambapo iwapo amepata ujauzito alikuwa anafungwa jela, na isitoshe hakuruhusiwa kuendelea na shule. TAMWA kwa kubaini ukosefu wa haki iliamua kuchukua hatua
(Sauti ya Bi Issa)
Na je jamii ina mtazamo gani kuhusu vyombo vya habari visiwani Zanziibar?
(Sauti ya Bi Issa)

Comments