Ukraine yataka fidia na kuombwa radhi rasmi

Ukraine yataka fidia na kuombwa radhi rasmi
Kufuatia Iran kukiri kuidungua ndege ya abiria ya Ukraine kimakosa, Rais wa Ukraine Vladmir Zelenskiy ameitaka nchi hiyo kuomba radhi rasmi pamoja na kulipa fidia
11.01.2020 ~ 11.01.2020
Vladimir Zelenskiy ,Rais wa Ukraine ameitaka Iran ikubali makosa kikamilifu kufuatia kuidungua kimakosa ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ukraine.
Zelensky kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amesema alitegemea Iran itaomba radhi rasmi na kuongeza,
“ Ukraine inasisitiza wakiri makosa kikamilifu, wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria, miili ya marehemu irudishwe, fidia zilipwe na tunategemea watatutaka radhi rasmi”.
Zelenskiy alisisitiza uchunguzi inabidi ufanyike haraka na bila ya kuingiliwa tena kwa uwazi.

Comments