Unataka kuishi umri mrefu ?, soma walichobaini watafiti wa Marekani
Makala iliyoandikwa katika jarida la "New England Medicine" imeelezea siri za umri mrefu
Watafiti nchini Marekani wamebaini kwamba kutokula kwa masaa 16-18 au kufunga kula kila baada ya muda fulani katika wiki hurefusha maisha na kuzuia magonjwa.
Katika makala iliyoandikwa katika jarida la “New England Medicine”, imebainishwa kwamba kula ndani ya masaa 6-8 katika siku na masaa yaliyobaki 16-18 kukaa mbali na chakula hukinga mwili kutokana na magonjwa tofauti, ikiwa ni pamoja na kupunguza shinikizo la damu na kurefusha maisha.
Katika makala hiyo imesisitizwa kwamba kufunga kula ni moja ya njia zinazowezapendekezwa katika tiba ya kiribatumbo, kisukari na magonjwa ya moyo, katika hilo inapendekezwa kufunga siku 2 kwa wiki au “kula kiasi kidogo kila siku”
Utafiti uliofanywa kwa kutumia binadamu na wanyama umeonyesha kwamba kufunga kila baada ya muda maalumu huweza michakato katika mwili “metabolism” kuhuishwa upya kitu ambacho hufanya afya ya chembe hai za mwili "cell" kuboreka.
Comments
Post a Comment