Wanajeshi 20 nchini Libya walioungwa mkono na shirika la umoja wa mataifa (UN) walipoteza maisha yao

Wanajeshi 20 nchini Libya walioungwa mkono na shirika la umoja wa mataifa (UN) walipoteza maisha yao siku ya (Alhamisi) baada ya shambulizi kati yao na jeshi la waasi nchini humo katika mji mkuu wa Tripoli kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vikosi vya serikali nchini humo, wanajeshi 12 walikamatwa na waasi hao baada ya shambulizi hilo. Kamanda wa jeshi la waasi hao Khalifa Haftar, ameagiza wanamgambo wake kuendeleza mashambulizi ndani na karibu ya mji huo wa Tripoli, huku akijaribu kuchukua eneo hilo. Maelfu ya watu walipoteza maisha yao na takriban watu 120,000 walihamishwa makwao kutokana na vita hizo.

Comments