Watu 6 ikiwemo Watoto watatu walipoteza maisha yao na wengine wanne kujeruhiwa






Watu 6 ikiwemo Watoto watatu walipoteza maisha yao na wengine wanne kujeruhiwa jana (Jumanne) nchini Uganda, baada ya lori la sukari kugonga jengo kwa nguvu kubwa katika wilaya ya Mayuge mashariki mwa nchi hiyo, msemaji wa maafisa wa polisi wa eneo hilo James Mubi amesema


Kwa mujibu wa James, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa lori hilo kushindwa kuipiga breki. Waliojeruhiwa walikimbizwa kwa hospitali ya karibu kupata matibabu. Kulingana na takwimu ya maafisa wa polisi nchini humo, Uganda inasajili takriban ajali 20,000 kila mwaka, kwa hivyo ni mojawapo ya nchi zilizo na kiwango cha juu cha vifo vya ajali za barabarani.

Polisi walidai viwango vya juu vya ajali za barabarani husababishwa na kuendesha gari bila kujali, makosa ya kibinadamu, kuendesha gari kwa mwendo wa kasi, kuendesha gari baada ya kunywa pombe na kujaza gari kupita kiasi.

Comments