Watu watatu wamethibitishwa kufa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati watuhumiwa wa kundi la al-Shabab

Watu watatu wamethibitishwa kufa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati watuhumiwa wa kundi la al-Shabab walipowashambulia raia wa Kenya wakisafiri kwa basi kwenye mkoa wa Pwani wa Lamu Alhamisi, polisi wa eneo hilo wamethibitisha.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Lamu, Perminus Kioi, alisema basi hilo lilikuwa kwenye njia ya Mombasa-Lamu wakati watuhumiwa wa wanamgambo wa al-Shabab walipovamia katika eneo la Nyongoro karibu na mji wa Witu katika kaunti ya Lamu.

"Tunaweza kudhibitisha kuwa watu watatu waliuawa na wengine kujeruhiwa. Tumewapeleka polisi katika eneo la tukio na operesheni ya uokoaji inatarajiwa kuanza hivi karibuni," Kioi alimwambia shirika la habari la Xinhua kwa simu.

Alisema kuwa basi hiyo kwa jina Mombasa Rhaha aliteketezwa na wanamgambo hao.

Comments