-
Watumishi watano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wamefariki dunia baada ya treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge katika eneo lililopo kati ya Stesheni ya Mwakinyumbi na Gendagenda
-
Taarifa iliyotolewa na TRC imesema watumishi wanne walifariki katika eneo hilo na mmoja alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Magunga iliyopo Korogwe mkoani Tanga. Mtumishi mmoja amejeruhiwa na anaendelea na matibabu
-
Waliofariki ni Ramadhani Gumbo (Meneja Usafirishaji Kanda ya Tanga), Mhandisi Fabiola Moshi (Meneja Ukarabati wa Mabehewa ya Abiria kanda ya Dar), Joseph Komba (Meneja Msaidizi Usafirishaji Kanda ya Dar), Philibert M. Kajuna (Mtaalamu wa Usalama wa Reli) na George Urio (Dereva wa Kiberenge)
-
Shirika hilo kwa kushirikiana na Taasisi nyingine zitafanya uchunguzi wa pamoja kubaini chanzo cha ajali hiyo
Comments
Post a Comment