Coronavirus: Uzazi wakati wa janga la corona



CoronaHaki

Janga la corona limevuruga mipango mingi ikiwemo ya mama wajawazito ambao walikuwa na mipango mingi ya kukaribisha watoto wao wapya na huku katika mataifa mengine tayari wameanza kupata huduma ya afya wakiwa nyumbani au kujifungulia nyumbani.
Katika maeneo mbalimbali duniani kwa sasa imekuwa ni jambo gumu kwa familia kutenganishwa haswa pale utamaduni wetu huwa unakusanyisha watu ili kuonyesha upendo.
Wakati huu umekuwa wa tofauti kwa wanawake wanaojifungua kwa kuwa imekuwa si rahisi kwa watu kuwatembelea kwenda kumuona mtoto mpya nyumbani au hospitalini.
Sheria za kuona wagonjwa hospitalini zimebadilika kwa kuzuia idadi ya watu na hata mama anapojifungua bado, wageni ni ngumu kwenda kumuona mtoto mpya au kumpa hongera mama kwa kujifungua salama.
Kizazi cha sasa ni kile ambacho hakikubali watu wawe karibu 'social distance generation' ambapo wazazi wanahitajika kujitenga wawezavyo ili kuepuka maambukizi kwa watoto.
Kwenye mitandao ya kijamii watu wamekuwa wakikejeli kuhusu majina ambayo yanaweza kupewa watoto wa kizazi hiki, maana katika jamii nyingine za Afrika mtoto huwa anapewa jina kulingana na msimu fulani, muda ndio maana unaweza kusikia mtu anaitwa Chausiku na sababu ikawa alizaliwa usiku, mwingine utasikia anaitwa Hajambo, Shida, Furaha na mengineyo.
Ni vivyo hivyo mijadala mtandaoni wamekuwa wakihoji kama watoto wa sasa majina yao yatakuwa na uhusiano wowote na corona au vitu ambavyo jamii imekuwa ikisisitizwa kutumia kama 'sanitizer' au 'mask' (Barakoa).

Katika mtandao wa Tweeter, wazazi wa mtoto mpya waliandika kuwa wamejitenga na familia kwa muda wa siku 14 kwa kuwa wakati huu ni wa kizazi cha 'social distancing", na watu zaidi ya laki saba walipenda picha yao.Lakini hayo ni miongoni mwa mabadiliko mengi ambayo yameletwa na mlipuko wa virusi vya corona.Kwa baadhi ya wanawake, sasa wanapaswa kujifungua wenyewe bila kusindikizwa na wenza wao.

coronaHakiGETTY IMAGES

Na wale ambao huwa wanachagua kujifungua kwa upasuaji nafasi hiyo haipo tena labda kwa wale ambao wana matatizo ya kujifungua kawaida ila wanalazimika kujifungua kwa operesheni.
Maeneo mengine wakiamini kuwa kujifungulia nyumbani ni salama zaidi ya kwenda hospitalini na hivyo kufanya utaratibu huo. Umekuwa ni wakati wa hofu kubwa kwa wazazi wapya , maana awali ilikuwa lazima mzazi uwe makini katika kumkinga mtoto na magonjwa lakini sasa mlipuko wa corona unafanya hali iwe ya wasiwasi zaidi.
Awali mama anayekaribia kujifungua alikuwa anaweza kupata wakati wa kujiandaa kwa mahitaji ya watoto kwa kufanya manunuzi au kuangalia mahitaji gani anahitaji kabla ya kujifungua lakini hali imebadilika kwa sasa.
Awali kulikuwa na sherehe ambazo mama mtarajiwa alikuwa akizifanya kabla ya kujifungua, kwa kualika marafiki na kupokea zawadi lakini sasa sherehe hizo hazipo tena.

Nikki akiwa na mwanayeHakiNIKKI DENNETT-THORPE
ImageNikki akiwa na mwanaye

Mzazi mmoja kwa jina Nikki alipata maambukizi ya corona na wahudumu wa afya walimshauri kuwa asijifungue kwa upasuaji bali wasubiri ili ajifungue kawaida.
Lakini hofu yake kuwa ilikuwa mtoto wake kuja duniani na kukutana na janga la corona huku mama na baba yake akiwa amevalia barakoa.
Nikki na mume wake walitengwa kwa muda wa siku 14, wakiwa pamoja na mtoto wao Stanley ambaye hajafahamika hata kwa wanafamilia.

Comments