TUJIKUdMBUSHE.. "WAALIMU WENZANGU, HIVI MNAWAFUNDISHA NINI HAWA VIJANA

 TUJIKUdMBUSHE..


"WAALIMU WENZANGU, HIVI MNAWAFUNDISHA NINI HAWA VIJANA?!"

PROFESA LIPUMBA

MWAKA 1995. KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU, CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM)



Moja ya maeneo ambayo Prof. Lipumba alifika kufanya kampeni katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 ilikuwa ni katika chuo cha usimamizi wa fedha, IFM

Ukumbi ulijaa hadi kufurika. Uadui ulioonyeshwa na hadhara iliyokuwepo ulikuwa wa juu na wa wazi mno kiasi kwamba ungeweza kuuhisi kwenye hewa. Huu uadui ulikuwa ni wa nini?!

Profesa Lipumba alipokaribishwa tu kuzungumza angani kuliinuka msitu wa mikono, wote wakitaka kuuliza maswali! 

Profesa Lipumba aliwapuuza akajaribu kuendelea kuzungumza. Minong'ono iliyokuwa ikizizima chini kwa chini sasa ililipuka na kuwa kelele. Nilimwandikia Profesa Lipumba ujumbe kwenye karatasi na kumsihi apokee maswali ya hao waliotaka kuuliza, au shughuli nzima ingeharibika. 

Baada ya kuusoma ujumbe wangu Profesa Lipumba alisita katika hotuba yake, akamnyooshea mmoja wa wale walionyoosha mikono juu huku akionekana kuchachawa sana, na kumwambia:

"Haya Uliza"

Alisimama yule kijana huku uso ukiwa umewiva kwa ghadhabu.

"Unataka kutuambia nini wewe! Wewe ulikuwa mshauri wa raisi. Ulimshauri rais vibaya mpaka nchi ikaingia kwenye hyperinflation. Leo unakuja hapa eti unataka urais!"

Alisema yule kijana. 

Profesa Lipumba alinyamaza mpaka akajiridhisha kuwa yule kijana alikuwa amemaliza. Ukumbi mzima ulikuwa unalipuka kwa shangwe! Profesa Lipumba aliangalia huku na kule, akaiinamia kisemeo (microphone) na kuuliza:

"Waalimu wenzangu, hivi mnawafundisha nini hawa vijana?! Kijana wa IFM leo hajui tofauti kati ya hyperinflation na inflation ya kawaida?!"

Ukumbi mzima ulipoa ukatulia kama umemwagiwa maji. 

Profesa Lipumba alianza kutiririka vitu ambavyo nadhani katika historia ya chuo hicho walikuwa hawajawahi kuvisikia.

Ghafla watu, walimu na wanafunzi walitoa notebooks wakaanza kuandika kwa kiu kubwa, yale aliyokuwa akiyasema Profesa Lipumba. 

Profesa Lipumba aliongea kwa saa nzima. Alipomaliza ukumbi ulilipuka kwa shangwe! Kila mmoja sasa alitaka kumpa mkono Profesa na kupiga naye picha! Wote walisahau kwamba walimkaribisha kwa uadui wa wazi.

Huyo ndiye Profesa Lipumba! Mzalendo ambaye wachumia tumbo wana hofu naye kubwa! In sha Allah Watanzania watakuelewa tu!

Comments