*UMUHIMU WA KUTUMIA JUISI YA KITUNGUU MAJI NA PARACHICHI*
Tumia juisi ya mchanganyiko wa kitunguu maji (chekundu) na parachichi kuondoa ziada ya tryglicerides kwenye mzunguko wa damu.
Tryglicerides ni aina ya mafuta yanayotengenezwa mwilini kutokana na ubugiaji wa kiasi kikubwa cha vyakula vya wanga na sukari.
Tryglicerides huhifadhiwa mwilini kwenye seli za mafuta na wakati wa njaa hutolewa huko zilikohifadhiwa na kugeuzwa kuwa nishati.
Tryglicerides zinapokuwa nyingi kwenye mzunguko wa damu huweza kusababisha ugonjwa wa moyo unaotokana na mishipa inayoleta damu kwenye moyo kujaa utando nta (plaque).
Mishipa hii inaposiribwa na utandonta hushindwa kufikisha kiasi cha kutosha cha damu kwenye misuli ya moyo. Hali hii hufanya moyo kupata utapiamlo wa oxygen na virutubisho vingine.
Moja ya njia za kujilinda dhidi ya mlundikano wa utandonta kwenye mishipa ya moyo ni kutumia juisi ya parachichi moja na kitunguu maji kimoja chenye ukubwa wa wastani kila siku.
Comments
Post a Comment