AKWELINA - 1

 

AKWELINA - 1

AKWELINA - 1

 


IMEANDIKWA NA : RUVULY DE FINISHER 

*********************************************************************************

Simulizi : Akwelina

Sehemu Ya Kwanza (1)



""" Mke wangu unajua hii inchi yetu ina mambo mengi mno ambayo tukiyaangalia kwa macho tunaona ya kawaida sana lakini kwa mwenye akili na mwenye mtazamo wa kufikiria mbali lazima atatambua kwamba maisha ya sisi tulio vijijini tena mpakani na nchi jirani tunaishi kama swala ndani ya msitu wenye simba wengi alafu wananjaa Kali mno unafikiri tutapona kweli , hivi mke wangu kwa elimu niliyonayo Mimi unafikiri mimi ni wa kuishi maisha kama haya kweli !! nina elimu kubwa sana mke wangu lakini leo hii tunaishi maisha ya kimaskini zaidi ya masikini wenyewe kula kwetu shida , tupo kwenye nyumba ya nyasi mvua ikinyesha tunalala tumesimama lakini yote kwa yote nakushukuru sana mke wangu kwa mapenzi ya dhati unayonipa pamoja na ugumu wa maisha haya lakini bado upo na Mimi, nakupenda mke wangu nakupenda mno haya mke wangu ingia ndani tukalala.


Yalikuwa ni maneno ya #KAKINGA akimueleza mke wake #MONNA kutokana na ugumu wa maisha waliokuwa nayo pamoja na elimu kubwa aliyojaliwa Kakinga lakini bado maisha kwake yalikuwa ni duni sana Kakinga alimchukua mke wake wakaingia ndani. Usiku ulizidi kusonga mbele masaa yalikatika, ilipofika saa saba usiku Monna alibanwa na haja ndogo ( mkojo ) akamuamsha mume wake ili ampeleke chooni kwakua ulikuwa ni usiku mnene, Monna alijaribu sana kumwamsha mume wake lakini kakinga huwa akilala kuamka ni ngum sana, Monna alizidiwa na mkojo ikabidi achukue taa akatoka nje .


Monna alikwenda hadi chooni akajisaidia , alipomaliza kujisaidia Monna akachukua taa lake akarudi alipokuwa anarudi ndani Monna kabla hajafika ndani alisikia mbwa wao anabweka kuashiria kuna kitu kibaya ambacho hakipo mbali na mazingira ya nyumba yao. Monna alichunguza sana wakati anachunguza ghafla alitokea mama mmoja akiwa ametapaa damu mwili mzima , yule mama alikuwa amebeba mtoto mdogo sana, Mama yule alipomuona Monna alimfuata akamuomba kwa kusema :-


""""" Binti yangu naomba saidia maisha ya mtoto wangu huyu Mimi sio wa kupona tena nakufa hali yangu sio nzuri mchukue Mtoto huyu alafu nenda nae mbali tafadhali nakuomba binti yangu nisaidie .


Monna alikuwa bado ameduwaa kwa mshangao, Yule mama akaondoka chini akapoteza maisha mtoto akaanza kulia baada ya kuondoka chini akiwa katika mikono ya mama yule , Monna alimchukua yule mtoto, Mtoto aliendelea kulia sauti ya mtoto yule ilisafiri kwa kiasi kikubwa ndani ya msitu ule, Monna akiwa anamtuliza mtoto alisikia watu wakisema :-


"" Jamani huyu huku namsikia mtoto analia upande huu """"


Monna alikimbia na mtoto kurudi nyumbani , wale watu walifuata sauti ile wakamkuta mama wa mtoto ameshakufa, wakasikia sauti ya mtoto ikiendelea kulia wakafuata sauti ile, Monna alikimbia hadi nyumbani kwake kwakua hakuwa mbali na nyumba yake aliingia ndani akamziba mtoto mdomo , Muda mchache wale watu wakafika eneo lile wakasema :-


*""" Hajaenda mbali huyu na inataikiwa na yule Mtoto achinjwe hastahili kubaki hai tawanyikeni sehemu zote mtafuteni sawa """*


Wale watu walikubaliana wakaondoka, Monna alimshukuru sana mungu, Monna akamfunua nguo yule mtoto akakuta kuna kitabu kidogo pamoja na kitambaa kilichofungwa, Monna alihisi damu katika mikono yake akaitazama ile damu ilipotokea akaona ile damu imetoka mgongoni mwa mtoto, Monna akamgeuza yule mtoto akaona mtoto ameandikwa neno #AKWELINA katika mgongo wake. Monna alishangaa sana kutokana na kuona mtoto alivyofanyiwa ukatili kama huo kwa sababu mtoto aliandikwa jina lile kwa kitu chenye ncha kali. Monna alimwamsha mume wake akamueleza yote yalimtokea mume wake akasema:-


KAKINGA ?? Mke wangu mbona unatafuta matatizo Wewe Mtoto huyu humfahamu alafu unaona kabisa jina hili lilivyo andikwa kwa kutumia kisu si kisu kabisa hiki sasa huyu mtoto akifa hapa au hao watu wakairudi tena utafanyaje ?


MONNA ?? Mume wangu eeee sasa Mimi ningefanyaje lakini mbona wanilaumu kiasia hicho wakati nimetoa msaada tu .


Kakinga aligombana sana na mke wake usiku kucha. Asubuhi na mapema palipokucha walitokea watu waliovaa nguo za kijeshi katika makazi yale wakawaita watu wote wanaoishi mazingira yale, Monna na Mume wake nao wakaenda katika mkutano huo , baada ya wanaichi kufika alisimama kiongozi wao akasema :-


"""" Wanaichi wa eneo hili mimi mkuu wa majeshi katika inchi hii tunashida kubwa sana na ndio maana tunapita kila sehemu tuawatangazia wanaichi wote kwamba kuna Mtoto amepotea , mtoto huyo nyuma ya mgongo wake ameandikwa jina linalosomeka AKWELINA kwa yeyote aliyemuona Mtoto huyo atapata pesa kiasi cha shilingi bilioni moja. Je kuna yeyote aliyemuona mtoto huyo ?


Kakinga aliposikia fedha nyingi kama zile aliingiwa na tamaa akajitokeza mbele ya kiongozi yule kisha akasema :-


KAKINGA ?? Kiongozi Mimi...........................




KAKINGA ?? Kiongozi Mimi nina swali naomba kuuliza tafadhali .


KIONGOZI ?? Uliza kijana .


KAKINGA ?? Tunaomba picha ya huyo mtoto ili siku tukimuona iwe rahisi kumtambua na kwanini mtoto huyo ameandikwa jina hilo la AKWELINA katika mgongo wake ?


KIONGOZI ?? Picha zipo tutawaonesha wananchi wote na kuhusu historia ya mtoto huyo sio rahisi kuifahamu wewe mwanaichi wa kawaida kutokana na sheria ya nchi inavyosema sawa kijana ?


KAKINGA ?? Sawa kiongozi .


KIONGOZI ?? Vizuri sana sasa tutawapatia mawasiliano ili siku yeyote au kwa yeyote ataemuona ajitahidi kuwasiliana na sisi tunaomba ushirikiano wenu na yeyote ataebainika kwamba kamficha Mtoto huyo adhabu yake itakuwa kali isiyo na msamaha .


Kakinga akafikiria sana suala hilo akatamani kusema ukweli lakini nafsi yake ikakataa wakati Kakinga yupo katika dimbwi zito la mawazo Wanajeshi waligawa vipeperushi kwa wingi kisha wakaondoka, Monna akamchukua mume wake wakarudi nyumbani, walipofika nyumbani walimkuta mtoto analia sana , Monna alimchukua mtoto yule akajaribu kumnyonyesha kitendo hicho kilimfurahisha sana kakinga akamwambia mke wake (Monna) :-


KAKINGA ?? Mke wangu huwezi kutoa maziwa kwa sababu maziwa huwa yanatengenezwa ukiwa na ujauzito sasa Wewe ujauzito unao ?


MONNA ?? Heeeeeh Mimi nilikuwa sifahamu mume wangu sasa nifanyaje huenda huyu mtoto ananjaa sana , inabidi nikanunue maziwa ya ng'ombe au unasemaje ?


KAKINGA ?? Nenda kanunue mke wangu hilo ni jambo la busara sana lakini kwanini mtoto huyu anatafutwa sana na wanajeshi si hatari hii au aliyekupa mtoto huyu alikuwa ni mtu mbaya ndani ya nchi yetu ? Ninahofu mke wangu kwa sababu wale ni walinzi wa nchi hii huyu mtoto asiwe mtoto wa Raisi ohoo itakuwa hatari .


MONNA ?? Sijui bana na kwanini yule mama aliniambia nimtunze mtoto wake hiyo ndio hofu yangu huenda ni kweli usemayo lakini sina imani na wale wanajeshi Mume wangu naomba tumlee huyu mtoto hayo mengine anajua mungu .


KAKINGA ?? Mmmh haya kamletee maziwa na ununue na dawa uje tumuekee alipoumia .


Monna alichukua pesa akaenda kununua vitu alivyo hitaji baada ya muda Monna alirudi akachemsha maziwa akampatia mtoto, katoto kalikuwa na njaa sana kalikunywa maziwa kwa kasi sana kaliposhiba , Monna akachemsha maji akamuogesha, baada ya kumuogesha Monna alimpatia kakinga yule mtoto ili ampake dawa Sehemu alizoumia, kakinga wakati anampaka dawa mtoto roho ilimuuma sana akasema :-


KAKINGA ?? Mke wangu wanadamu wanaroho mbaya sana yaani mtoto mdogo kama huyu wamempatia majeraha kama haya daah aliyefanya hili tukio mungu anamuona, alafu mke wangu kuanzia leo mtoto huyu ataitwa jina hili hili aliloandikwa mgongoni kwake kwa sababu huenda hili jina linamaana kubwa kwake au unasemaje mke ?


MONNA?? Upo sawa Mume wangu kipenzi nahisi jina hili litalinda kumbukumbu zake siku sijazo .


Baada ya Mwaka mmoja maisha yalikuwa yenye furaha na upendo zaidi kwa kakinga na Monna baada ya kumpata Akwelina katika maisha yao walimpatia malezi bora na upendo zaidi, Monna alimpenda sana Akwelina, Siku baada ya siku watu wa maeneo aliopo mtoto Akwelina walimpenda sana kwakua Akwelina alikuwa binti mzuri sana, Monna hakuwa na kipingamizi kwa yeyote aliyehitaji kuondoka na mtoto, Upendo wa Monna kwa majirani zake ulimfanya asahau kuwa mtoto yule anatafutwa sana na Serikali.


Monna na mume wake kakinga waliendelea kuishi maisha hayo bila wasiwasi wowote, Siku moja majira ya asubuhi Monna alitembelewa na rafiki yake kipenzi ZILPA , Zilpa alimkuta Monna anafua nguo akiwa na mtoto mgongoni kwake, Monna akamkaribisha rafiki yake kipenzi akampatia kiti rafiki yake, Monna akaendelea kufua nguo wakiwa wanazungumza na rafiki yake .


Maongezi yaliendelea kwa muda akwelina akaanza kulia Zilpa akamchukua Akwelina ili amsaidie rafiki yake aweze kufua nguo, Zilpa alipokuwa anamtuliza Akwelina nguo ya juu aliyovaa Akwelina ilipanda juu kidogo, Zilpa alistuka baada ya kuona maneno baadhi yameandikwa mgongoni kwake, Zilpa akatamani kuona maneno aliyoandikwa Akweli Zilpa akazidi kumfunua akakuta jina limeandikwa AKWELINA katika mgongo wa mtoto Zilpa akastuka mno , Monna alipomaliza kufua nguo aliingia ndani kuchukua maji aliporudi nje Monna hakumuona Zilpa pamoja na mtoto Monna alidondosha ndoo ya maji chini aka...




Monna alidondosha ndoo ya maji chini akatoka nje ya nyumba yao akatazama pande zote hakumuona Zilpa, Monna alianza kulia akiwa anakimbia hovyo Kilio cha Monna kiliwastua majirani walijitokeza kwa wingi wakashangaa sana kumuona Monna anakimbia ovyo akiwa anamwita Zilpa, Monna alizunguka kijiji kizima toka asubuhi hadi majira ya saa sita mchana bado Monna hakufanikiwa kumuona Zilpa, Monna alirudi nyumbani masikini akiwa amechoka sana Roho ilimuuma sana Monna nguvu zilimuisha kichwa kikamuuma sana, Monna akajivuta taratibu taratibu hadi nyumbani kwake , Monna alipofika nyumbani aliingia ndani akaanza kulia kwa uchungu, Kilio cha Monna kiliendelea hadi majira ya usiku bado Monna alikuwa analia .


Siku hiyo Kakinga alichelewa sana kurudi nyumbani kutokana na shughuli zake kakinga akiwa kazini alifuatwa na rafiki yake , Rafiki huyo alipofika kwa Kakinga akashanga kumuona Kakinga bado anafanya kazi Rafiki wa Kakinga akasema:


RAFIKI: Kakinga ndugu yangu yaani bado unafanya kazi hadi muda huu inamaana huoni giza hili ?


KAKINGA: Naliona lakini siwezi kulaza kazi hii inabidi niimalize kabisa ili kesho nishike kazi nyingine si unajua pesa sina kaka , Nivumilie kidogo nimalize kazi hii alafu tunaondoka nyumbani sawa ?


RAFIKI: Sawa lakini muda umekwenda kaka kumbuka kijiji chetu kimechafuka siku hizi sasa wewe poteza muda hapa ukute mke wako amebakwa kama Maria mtoto wa mwenyekiti alivyobakwa .


KAKINGA: Aaah weee wambake nani mke wangu mimi ?? Haha sio rahisi mke wangu mwenyewe komando wewe unamuonaje ??????


RAFIKI: Haya wewe shauri yako .


KAKINGA: Kuwa na amani bwana mkubwa kazi imeisha hii sasa hivi tunarudi nyumbani ondoa hofu .


Baada ya dakika ishirini kakinga akafanikiwa kumaliza kazi yake akabadili nguo kisha wakarudi nyumbani, Safari haikuwa ndefu sana walipofika mtaa wa nyumbani Rafiki wa Kakinga akamuacha kakinga akaenda nyumbani kwake nae Kakinga akaenda nyumbani kwake. Kakinga alipokaribia eneo la nyumbani akasikia sauti ya Mke wake kipenzi toka ndani ikilalamika kwa kutoa kilio cha hudhuni mno kakinga akastuka mno akatupa vifaa vya kazi chini alikurupuka mbio hadi ndani akamkuta Monna amekaa chini akiwa hovyo hovyo kakinga alimuuliza mke wake akiwa na hofu :-


KAKINGA: Kuna nini mke wangu umegongwa na nyoka au umebakwa ?


Monna hakujibu chochote akazidisha kilio kwa hasira Kakinga akazidi kuchanganyikiwa akauliza tena: Si ninakuuliza wewe umepatwa na nini mbona hunijibu Umebakwa sio ?


MONNA: Hapana mume wangu sijabakwa mimi aaaah .


Kakinga akapua kwa nguvu kisha akaikaa chini akasema: Tatizo nini Mke wangu au unaumwa ?


MONNA: Akwelina wangu jamani kaibiwa Mume wangu ????


KAKINGA: Haaaaah !! ?? Unasemaje Akwelina wangu kaibiwa ? Unajua sijakuelewa na sitaki matani kabisa, Unajua kiasi gani ninavyompenda mtoto wangu hebu acha kuniambia hizo simulizi zako sipendi utani Mke wangu niambie ukweli ?


MONNA: Kweli mume wangu Akwelina kaibiwa na Zilpa asubuhi ya leo nilikuwa nafua wakati huo nilikuwa nimembeba Akwelina Mgongoni Zilpa akaja kunitembelea ndio akaniomba anisaidie kumtuliza Akwelina kwa sababu alikuwa analia sana nikampatia kwa sababu namuamini sikuwa na hofu juu yake nikaingia ndani kuchukua maji nilipotoka nje sikumkuta tena Zilpa pamoja na Akwelina wangu jamani mimi nahisi kufa Mume wangu ??


KAKINGA: Zilpa anatafuta Vita na mimi nisubiri hapa hapa naenda nyumbani kwao Zilpa nahisi hawanifahamu vizuri pumbafu .


Kakinga alichukua Panga akatoka nje akiwa na hasira sana, Monna alijaribu kumziwia kakinga lakini alishindwa, Kakinga alikimbia mno bila kuchoka kutokana na umbali ilimchukua muda mrefu kakinga kufika nyumbani kwao na Zilpa, Japo palikuwa na umbali mrefu kakinga alijitahidi kukimbia bila kuchoka , kakinga alipokaribia nyumba anayoishi Zilpa alishangaa kuona wanajeshi wamezunguka nyumba yote, Kakinga alisimama na kujificha nyuma ya Nyumba nyingine.


Kakinga alijiuliza maswali mengi sana baada ya kuona wanajeshi wametapakaa eneo analoishi Zilpa lakini akakosa majibu, Kakinga akanyemelea ( kutembea taratibu ) kuifuata nyumba anayoishi Zilpa, kakinga alipofika karibu alichungulia akamuona Zilpa anampatia Mtoto yule kiongozi aliyetoa tangazo yule kiongozi akamvua nguo zote Akwelina akamkagua mgongoni alipoona lile jina akachukua begi kubwa akampatia Zilpa, Wakati huo Akwelina alikuwa analia sana kilio cha Akwelina kilimpatia maumivu makali sana kakinga .


Baada ya muda kidogo Wanajeshi waliondoka na Akwelina , Kakinga alishindwa afanya nini, Zilpa alibaki pale nyumbani na begi lake, Baada ya wanajeshi kuondoka Kakinga akamfuata Zilpa akamkuta akiwa na familia yake , Kakinga alianzisha vurugu kali Kaka wa Zilpa wakamchangia Kakinga wakamshinda nguvu wakampiga sana alafu wakambeba wakamtupa mbali na Nyumba yao, Kakinga alirudi nyumbani akiwa amevimba sura na nguo zake zimechanwa chanwa , Kakinga alipofika nyumbani kwake alikaa nje akawa analia kwa hasira Monna akatoka nje haraka baada ya kumsikia mume wake analia, Monna alimkuta kakinga yupo hovyo hovyo Monna akauliza :


MONNA: Umepatwa na nini mume wangu mbona upo hivyo ?


KAKINGA: Zilpa mshenzi sana mke wangu kampeleka Akwelina kwa wale wanajeshi na wamemchukua mtoto wetu masikini ?? .


MONNA: Mungu wangu nakufa mimi masikini Akwelina wangu daaah najuta Mimi Zilpa mungu atakulipa nakuchukia sana mbwa wewe ??


KAKINGA: Sikubali mke wangu, Akwelina wangu hawezi kwenda mbali na Mimi kwa hali yeyote sikubali nakuapia mke wangu sikubali lazima nitamrudisha katika mikono yetu subiri uone Monna ??


Kakinga na monna walikaa nje ya nyumba yao hadi asubuhi. Siku iliyofuata asubuhi wale wanajeshi waliwaita wananchi wote wa eneo lile, kiongozi wao akasimama kisha akasema :


KIONGOZI: Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu nimewapenda sana watu wa eneo hili hususa binti mmoja anayeitwa ZILPA yeye katusaidia kumpata mtoto tuliyekuwa tunamtafuta kwa muda mrefu, leo tutalala katika eneo hili na tutaweka sherehe usiku wa leo ili tufurahi kwa pamoja kwa hiki mlichofanya kwetu nawapongeza sana wananchi wetu .


Baada ya kiongozi kumaliza mazungumzo na wananchi, kiongozi aliwapatia Wanajeshi kazi ya kutafuta sehemu itayofanyika sherehe hiyo majira ya usiku, Wanajeshi hawakupoteza muda wakashirikiana na Wananchi wakatengeneza eneo kubwa sana kwa ajili ya sherehe hiyo. Baada ya masaa kadhaa jua lilizama giza nene likatawala anga, Usiku huo ulikuwa usiku wa furaha kwa wananchi wengi lakini usiku huo ulikuwa mbaya sana kwa Monna na mume wake Kakinga, Kakinga akiwa na mke wake nyumbani kwao alifikiria sana kisha akamwambia Mke wake :


KAKINGA: Mke wangu andaa vitu vyako muhimu vyote usisahau na vile vitu ulivyomkuta navyo Akwelina, naondoka naenda huko kwenye sherehe yao narudi na Akwelina hapa kwa hali yeyote siwezi kukubali .


MONNA: Hapana mume wangu watakuua wale watu hawana huruma kabisa mume wangu tafadhali usiende ukifa mimi nitaishi vipi bila wewe jamani usiende Mume wangu .


KAKINGA: Mungu atanisaidia kwa hilo ninaamini kabisa wale sio watu wazuri kwenye maisha ya yule mtoto.


Kakinga alipata ujasili wa ajabu sana akaondoka moja kwa moja hadi katika sherehe, alipokaribia hema alipokuwepo kiongozi wao akajificha katika majani, kakinga akiwa amejificha alimuona mwanajeshi mmoja anakuja eneo alilokuwepo katika alitetemeka akatulia kimya, yule mwanajeshi alifika akakojoa , kakinga alimvamia yule mwanajeshi akampiga jiwe la kichwa yule mwanajeshi akapoteza fahamu kakinga akavaa mavazi ya yule mwanajeshi kisha akaingia hadi katika chumba cha kiongozi akamuona Akwelina amelala karibu na kiongozi huyo, Kakinga akiwa ndani ghafla akaja mwanajeshi mmoja akamchua kiongozi akatoka nae nje Kakinga akatumia nafasi hiyo hiyo akamchukua Akwelina akachana lile hema kwa upande wa nyuma akatoka nje, Kakinga alipopiga hatua chache akakutana na wanajeshi mbele yake, Kakinga akawapa mgongo wale wanajeshi wakampita ghafla Akwelina akalia kwa sauti wale wanajeshi waka.........



Kakinga alipopiga hatua chache akakutana na wanajeshi wengine kakinga akawapa mgongo wale wanajeshi wakampita ghafla akwelina akalia kwa sauti wale wanajeshi walisimama Mwanajeshi mmoja akamuuliza kakinga :-


MWANAJESHI ?? Simama askari huyo mtoto uliyenae umemtoa wapi na muda kama huu unampeleka wapi ?


KAKINGA ?? Aaah mtoto huyu anaumwa sana ninaenda kumpatia tiba ili kukoa maisha yake hiyo ni amri toka kwa kiongozi.


MWANAJESHI ?? Sawa naomba kitambulisho chako kwa sababu unaomekana unawasiwasi sana.


Yule mwanajeshi akamsogelea kakinga, Kakinga alijiandaa akamshika vizuri akwelina, yule mwanajeshi alipotaka kumshika kakinga, kakinga alitumua mbio wale wanajeshi walipomuona kakinga anakimbia walimfukuza wakiwa wanapiga firimbi kuwajulisha wenzao , mlio wa firimbi ile ulisambaa eneo lote wanajeshi walijigawa taa kubwa liliwashwa lile taa lilimmoreka kakinga taa lile liliwasaidia wanajeshi kumuona kakinga vizuri, wakati kakinga anakimbia wanajeshi wengine walitokeza mbele yake kakinga akasimama wale wanajeshi walimzunguka kakinga, wakamnyoshea silaha wakamwambia apige magoti, kakinga alipiga magoti akiwa chini alimshika akwelina vizuri akatazama mbele yake akaona kuna msitu kakinga alisimama ghafla akamsukuma mwanaheshi mmoja akapata njia kakinga akakimbia tena.


Wale wanajeshi walipiga risasi hovyo kakinga akajificha katika mti mkubwa uliokuwepo ndani ya msitu huo, baada ya muda wale wanajeshi waliacha kupiga risasi wakaingia msituni kumtafuta kakinga, Kakinga alipoona wale wanajeshi wameacha kupiga risasi anaendelea kukimbia kakinga alipita njia ya karibu ili awahi kufika nyumbani kwake. Wale wanajeshi walimtafuta kakinga msitu mzima lakini hawakumpata wakarudi kwa kiongozi , kiongozi aliwauliza :-


KIONGOZI ?? Mtoto yupo wapi ?


??WANAJESHI:-

“”** Tunastahili adhabu ya kifo mkuu yule kijana hatujamuona **””


KIONGOZI ?? Pumbafu kabisa askari zaidi ya elfu moja mnashindwa kumkamata mtu mmoja tena mwananchi wa kawaida shenzi kabisa nifuateni .


Kiongozi wa wanajeshi alichukua bastola yake akatoka nje akawafukuza wananchi wote waliokuja katika sherehe, alafu akachukua usafiri wakaondoka moja kwa moja hadi kwa zilpa walimkuta zilpa ametoka kuoga kiongozi alikuwa na hasira sana akasema :-


KIONGOZI ?? Wewe binti umemtuma mtu aje kumchukua mtoto sio ?


ZILPA ?? Nimemtuma mtu aje kumchukua mtoto !! Mbona sielewi Mimi sijafanya hivyo kiongozi wangu na siwezi kufanya hivyo kwani kuna nini jamani ?


KIONGOZI ?? Kuna kijana wa kiume amekuja akamchukua Mtoto na akatoweka nae .


ZILPA ?? Nahisi atakuwa ni KAKINGA .


KIONGOZI ?? KAKINGA ndio nani ?


ZILPA ?? Yule ndio alikuwa amemficha huyo Mtoto muda mrefu .


KIONGOZI ?? Nipeleke anapoishi sasa hivi .


Kiongozi alimchukua zilpa wakaondoka kuelekea nyumbani kwa kakinga. Kakinga baada ya kukimbia sana alifika nyumbani akamwita mke wake Monna , Monna alipotoka nje hakuamini kumuona akwelina amerudi katika mikono yake, Monna alimkumbatia akwelina akambusu sana kwa furaha machozi yalimtoka monna , kakinga akasema :-


KAKINGA ?? Mke wangu hakuna muda wa kupoteza jiandae tuondoke utaendelea kumbusu huko mbele maisha yetu nimeyaharibu kwa kumuokoa akwelina tuondoke mke wangu haraka.


Monna aliingia ndani akachukua kanga akamfunga akwelina mgongoni kwake akachukua vitu muhimu vyote akasahau vile vitu alivyomkuta navyo akwelina, Kakinga alimkumbusha monna , Monna akarudi ndani akachukua mfuko mweusi pamoja na kile kitabu kidogo walichomkuta nacho akwelina. Kakinga alimchukua mke wake wakaondoka walipofika mbali kiasi waliona mwanga wa mataa makali eneo la nyumba yao wakasimama kwakua walikuwa kwenye mlima mdogo walimuona zilpa akiwa na wanajeshi Wengi. Wale wanajeshi walifika wakavunja mlango ndani hawakumkuta mtu kiongozi akasema :-


KIONGOZI ?? Ndani hakuna mtu ee sawa na wamekimbia wameacha mifugo tu sasa choma moto nyumba yote hii, choma na mifugo yao .


Wale wanajeshi walimwaga mafuta eneo lote wakachoma moto, Kakinga na mke wake Monna wakiwa mbali kidogo walistuka baada ya kuona nyumba yao inawaka moto , roho iliwauma sana lakini walikuwa hawana uwezo wa kufanya chochote, Monna alimtazama sana mume wake alimuona kakinga ana huzuni Monna akamwambia mume wake :-


MONNA ?? Usijali mume wangu haya ni mapito tu na mungu ndio anayepanga twende mjini, huko mjini anaishi mama yangu mdogo tutamuomba hifadhi mume wangu sawa .


KAKINGA ?? Sawa mke wangu lakini ipo siku haya manyanyaso yataisha.


Monna alimshika mkono mume wake wakaondoka kuelekea stendi ya mabasi, walifika stendi wakapata usafiri, Safari ilikuwa ndefu sana. Yalipofika majira ya asubuhi walifika mjini walimshukuru mungu kufika salama , Wakachukua mizigo yao safari ikaendelea kwenda kwa mama yake mdogo na monna. Hapakuwa mbali sana muda mfupi walifika Monna akapiga hodi mlinzi akaja akamfungulia mlango Monna na kakinga wakaingia ndani , Wakamuomba mlinzi akamwite mama yake mdogo , Kakinga na Monna walipokuwa wanamsubiri mlinzi aje na mama yao mdogo, Ghafla geti liligongwa kakinga akasogea ili amfungulie huyo mtu anayegonga mlango kwakua mlinzi hakuwepo kakinga alipofungua mlango alistuka sana kumuona mtu anaegonga mlango ni yule kiongozi wa wanajeshi kakinga ali……




Ghafla geti liligongwa kakinga akasogea ili amfungulie huyo mtu anayegonga mlango kwakua mlinzi hakuwepo kakinga alipofungua mlango alistuka sana kumuona mtu anaegonga mlango ni yule kiongozi wa wanajeshi kakinga aligeuka na kutazama pembeni akaacha mlango wazi yule kiongozi akapitiliza moja kwa moja hadi ndani, kakinga akamfuata Mke wake haraka haraka akiwa na wasiwasi akamwambia :


KAKINGA: Mke wangu hii sio sehemu salama kwetu tuondoke sasa hivi .


Monna akamshangaa sana Mume wake alafu akamjibu: Kwanini mume wangu mbona unanitisha ?


KAKINGA: Sikutishi mke wangu umemuona yule mwanaume aliyeingia ndani dakika chache zilizopita ?


MONNA: Hapana sijamuangalia usoni vizuri kwani ni nani ?


KAKINGA : Mke wangu mtu yule ni yule kiongozi wa wanajeshi wanaomtafuta sana Akwelina .


MONNA: Mungu wangu sasa tunafanyaje mume wangu jamani ?


KAKINGA: Hebu nifuafe huku .


Kakinga alimchukua Mke wake monna wakatoka nje ya geti wakasogea mbali na nyumba ile, Kakinga na monna walikaa nje pale kwa masaa matatu wakamuona yule kiongozi anatoka nje na mama mdogo walipofika nje kiongozi alimuaga mama mdogo alafu akaondoka, Kakinga na monna walipomuona yule kiongozi kaondoka walirudi getini wakagonga geti tena Mlinzi alipowaona kwa mara ya pili akawaambia:


MLINZI: Ninyi mbona siwaelewa au ninyi ni majini? si nimewaambia mnisubiri hapa nikamwite madame Mimi naingia ndani ninyi mkaondoka narudi nje sijawakuta nahofu sana na ujio wenu au mnataka kuiba niite askari ?


MONNA: Hapana kaka sisi hatupo hivyo unavyofikiria mtoto alikuwa anataka maji ndio tukaenda kununua dukani na huyo madam ni mama yangu mdogo tafadhali tunaomba kuonana nae .


Mlinzi aliguna kisha akawazunguka kwa muda mrefu kisha akasema:


MLINZI: Sasa siwaruhusu kuingia ndani subirini hapa hapa nje ya geti nikamwite Madame siwaamini tena.


Mlinzi alifunga mlango akaingia ndani akamwita madame, Madame alitoka nje akamwambia mlinzi afungue geti baada ya Mlinzi kufungua geti Madame hakuamini kumuona Monna mbele yake madame alifurahi sana Kumuona Monna akasema: Njoo mwanangu jamani miaka mingi imepita Monna umekuwa msichana mkubwa sasa ingia ndani Mama njooo ??


Monna kwa furaha aliingia ndani akamkumbatia Mama yake mdogo kwa shauku na bashasha madame akampokea Monna kwa furaha pia, Madame akamuona Kakinga akamuuliza Monna: Huyo kijana ni nani Msichana wangu ?


MONNA: Huyu ni Mume wangu Mama anaitwa Kakinga na huyu ni mtoto wetu wa kwanza .


MADAME: Anhaa karibu sana Mkwe wangu karibu nyumbani mimi ndio Mama yake mdogo na Monna kwahiyo ondoa wasiwasi jione upo kama nyumbani kwako Baba alafu usiniogope buana mimi ni mzungu wa roho kwahiyo kuwa huru.


KAKINGA: Ahsante sana Mama yangu nimefurahi sana kukufahamu.


Baada ya mazungumzo hayo Madame alimchukua Monna na Kakinga wakaingia ndani walipofika ndani Madame akawapatia chakula kizuri sana kisha akawaonesha chumba chao cha kulala alafu akaingia chumbani kwake , Monna na Kakinga walipomaliza kula waliingia chumbani kwao wakalala .


Baada ya mwezi mmoja kupita maisha ya monna na kakinga ndani ya nyumba ya Madame yalikuwa maisha mazuri sana siku baada ya siku monna na kakinga walizidi kupendeza na kunawili. Siku moja majira ya mchana Kakinga alikuwa anazungumza na mke wake monna kakinga akamuuliza :


KAKINGA : Mke wangu hivi Mama yako mdogo anafanya kazi gani kwa sababu kila siku usiku anatoka alafu anarudi asubuhi sijawahi kumuona anaenda kazini hata Siku moja lakini anafedha nyingi mno sasa fedha hizi yeye anazitoa wapi ?


MONNA: Mmmmh mume wangu umeanza kupekuwa pekuwa vitu visivyokuhusu yanakuhusu hayo ni maisha yake tumeyakuta na tuyaache kama yalivyo sawa mume wangu ?


KAKINGA: Sawa lakini mmh ninawasiwasi sana na Mama yako mdogo sijui ni kwanini lakini acha nikae kimya kama utakavyo Monna.


MONNA: Ni bora tu ukae kimya Mume wangu asije akatusikia akatufukuza bure pia jiulize tukifukuzwa tutakwenda wapi ?


KAKINGA: Sawa Mke wangu .


Monna alikuwa hapendi Mume wake azungumze kitu kibaya chochote kuhusu mama yake mdogo kwa sababu Monna alikuwa anamuamini sana pia alikuwa anampenda mno mama yake mdogo, Wakati Kakinga akiwa anazungumza na Monna Madame alitoka nje akamwita Monna , Monna akamfuata Madame alipofika Madame akamwambia: Leo nahitaji kutoka kidogo na Mume wako kama inawezekana Mtoto wangu .


MONNA: Kwanini isiwezekane Mama yangu yule ni Mtoto wako pia na hukuhitajika kuniomba ungemchukua tu Mama yangu .


MADAME: Ahsante Mtoto wangu naomba mueleze Mume wako suala hili nahitaji tutoke sasa hivi sawa ?


MONNA: Sawa Mama yangu kipenzi.


Monna akamfuata Mume wake akamueleza ombi la Mama yake mdogo Kakinga hakupinga ombi la Mama ikabidi akubali , Kakinga akajiandaa kisha wakaondoka, Safari ilikuwa ndefu sana wakafanikiwa kufika eneo moja lililokuwa linatoa harufu mbaya sana Madame akamwambia Kakinga: Pole kwa harufu mbaya Mkwe vumilia kidogo wala hatukawii eneo hili .


KAKINGA: Aaah Usijali Mkwe tupo pamoja lakini tumefuata nini hapa ?


MADAME: Kuna picha nitaletewa hapa kwahiyo ilinilazimu niwe na kijana wa kiume kama walivyotaka wao hiyo ndiyo sababu ya kukuchukua wewe Mkwe .


KAKINGA: Watu gani hao Mkwe ?


Madame aligeuka akamtazama sana Kakinga alafu akasema: Mbona unaniuliza maswali mengi una hofu na Mimi Mkwe ?


KAKINGA: Hapana hapana Mama yangu nilikuwa nauliza tu .


Muda huo huo akatokeza Kijana mmoja akampatia Picha Madame kisha akaondoka , Madame akaitazama picha hiyo akastuka mno alafu akairudisha picha ndani ya Bahasha wakarudi Nyumbani, Walipofika Nyumbani Madame akambeba Akwelina akamtazama kwa muda mrefu kisha akamrudisha kwa Monna Madame akaingia ndani, Kitendo hicho kilimshangaza sana Kakinga akatamani kuzungumza na Monna lakini akasita akaacha .


Usiku ulipoingia majira ya saa saba Kakinga alibanwa na haja ndogo ( mkojo ) kakinga aliamka akaenda chooni wakati anakwenda chooni alimuona Mama mdogo sebuleni anatazama TV alafu ameshika picha mkononi kwake Kakinga aliendelea na safari yake baada ya hatua chache Kakinga alimsikia mama mdogo anapokea simu akasema :-


MADAM: Ndio mkuu yule kijana uliyenipatia picha yake yupo kwangu leo amefikisha mwezi na siku kadhaa akiwa katika nyumba yangu sasa muda huu atakuwa ameshalala chukua watu sita alafu njooni mimi nipo macho nawasubiri msikawie fanyeni haraka sawa .


Kakinga alistuka baada ya kusikia maneno hayo akarudi chumbani kwake taratibu alipofika alimuamsha Monna akamueleza yote aliyosikia toka kwa Mama mdogo ( madame ) Monna alitaka kupinga alichokisikia kakinga akamuomba Monna watoke nje ya nyumba hiyo , Monna alikubali kwa shingo upande kakinga alimshika mkono Monna akatoka nae kwa mwendo wa taratibu mno, kakinga na Monna walipokaribia mlango taa ziliwaka ghafla wakamuona Mama mdogo yupo mbele yao ameshika bastola Monna hak......................................................



Monna hakuamini macho yake monna alihitaji kumsogelea mama mdogo, mama mdogo akanyanyua bastola juu kisha akasema :-


MADAM ?? Usijaribu kunyanyua hatua nyingine najua utashangaa sana mtoto wangu lakini sihitaji kuiponza damu ya mtoto wa dada yangu cha maana muda huu naomba nipatie huyo mtoto hilo tu linaweza kusaidia maisha yenu .


MONNA ?? Lakini mama mdogo mtoto wangu kakukosea nini na kwanini unamtaka ukiwa umeshika silaha huyu ni Mjukuu wako mama yangu muda wowote ukimtaka unampata lakini sio kwa shari kama hivyo ulivyo .


MADAM ?? Nisikilize Monna huyo mtoto sio wako na kwa kukuhakikishia hilo huyo mtoto ana jina katika mgongo wake ameandikwa AKWELINA kweli au siokweli ?


KAKINGA ?? Mama sio kweli hayo unayosema huyu mtoto ni wangu tangu nipo nae toka anazaliwa hadi leo lakini sijamuona ana jina hilo mgongoni ngoja nimlete kwako ili umchunguze Mjukuu wako kama hautuamini.


Kakinga alimchukua mtoto kutoka katika mikono ya Monna , Monna alikataa kakinga asimchukue mtoto, kakinga akambonyeza monna katika kidole cha mguu Monna akampatia kakinga mtoto, kakinga alimsogelea mama mdogo bila hofu yeyote, kitendo kile kilimjengea imani mama mdogo akashusha bastola chini akajiandaa kumpokea mtoto katika wakati anampatia mtoto mama mdogo mtoto alimkwapua ( kumnyanganya ) mama mdogo ile bastola alafu akamnyoshea mama mdogo Kakinga akamwambia Monna :-


KAKINGA ?? Mke wangu mchukue ingia ndani chukua mizigo yetu tu tuliyokuja nayo alafu mchukue na mtoto.


MADAM ?? Monna ukimchukua mtoto Mimi nitakuwa sio mama yako tena nitageuka na kuwa adui yako nitakutafuta dunia nzima na nikikupata kichwa chako halali yangu. alafu wewe kijana huwezi kutoka katika himaya yangu hii na kama ulikuwa hujui nyumba yangu yote imejaa walinzi utapita wapi hahaha rudisha bastola yangu haraka .


KAKINGA ?? Monna nimekwambia mchukue mtoto harakaaaaa .


Monna aliingia ndani akachukua mizigo yao muhimu akatoka nje akamchukua akwelina toka katika mikono ya mama mdogo , kakinga alimchukua mama mdogo akamtanguliza mbele wakatoka nje, walipofika nje waliwakuta wanajeshi wengi kakinga hakuogopa akamtumia mama mdogo kama ngao, Kakinga aliendelea kutoka nje zaidi akafanikiwa kutoka nje ya geti la mama mdogo. Kakinga alipotoka nje ya geti akafunga lile geti alafu akaitupa mbali ile bastola kakinga akamsukuma mama mdogo akashika mkono wa mke wake Monna wakakimbia, mama mdogo alifungua lile geti haraka wanajeshi wakatoka wakawaona kakinga na Monna wameshafika mbali, Mama mdogo na wale wanajeshi waliwafuata wakiwa wanapiga risasi hovyo. Milio ya risasi ilizidi kuwapatia wasiwasi kakinga na Monna walikimbia zaidi, Baada ya muda mrefu Monna alichoka sana akashindwa kuendelea kukimbia, kakinga akaona gari limebeba takataka dereva wa gari lile alikuwa pembeni anakojoa, Kakinga akatumia nafasi hiyo akapanda kwenye gari lile akampandisha na mke wake Monna, Monna wakati anapanda alidondosha mzigo mmoja ikabidi kakinga ashuke akaufuata ule mzigo, Mzigo ule ulikuwa mbali kidogo kakinga alifika akauchukua ule mzigo ghafla akasikia gari linaondoka, kakinga alistuka akaanza kulikimbiza lile gari, Kakinga alijitahidi kukimbia kadri ya uwezo wake, lakini akachoka gari likamuacha.


Monna alibaki analia baada ya kumuona mume wake kakinga gari limemuacha. Kakinga alijuta sana kwa kile alichofanya kakinga ikabidi atembee kwa mguu , lile gari lilitembea kwa muda mrefu sana likafika Sehemu ya kutupa uchafu likasimama Monna bila kuchelewa alishuka chini akasogea mbali na lile gari. Monna alitazama huku na kule akashindwa kutambua yupo sehemu gani, Yule dereva alimwaga taka alipomaliza akaondoka. Monna alitazama upande wa kulia aliona bonde dogo akaingia ndani ya bonde hilo akamfunika mtoto vizuri alafu akalala. Kakinga akiwa njiani aliona gari lingine limebeba uchafu kakinga aliomba msaada aliomba msaada akapanda ndani ya gari lile. Monna akiwa amepitiwa na usingizi walikuja wanaume wanne hadi katika lile bonde wakamkuta binti akiwa amebeba mtoto amelala mmoja akasema :-

“””” Nani huyu kalala katika chumba chetu alafu ni binti mzuri sasa huyu leo ni zawadi yetu, alafu amekuja muda mzuri kuna baridi kweli “”””


Monna akiwa amelala alistuka amekamatwa na watu asiowajua, Mmoja kati ya wale watu alimchukua mtoto akaenda kumuweka mbali akarudi wakamshika Monna wakamlaza chini wakamvua nguo, Kiongozi wao akasimama akafungua zipu ya suruali yake alafu aka……





Monna akiwa amelala alistuka amekamatwa na watu asiowajua, Wanaume hao wakamnyanganya mtoto Monna alafu wakamuweka chini kisha wakamshika Monna wakamlaza chini wakamvua nguo, Kiongozi wao akasimama akafungua zipu ya suruali yake alafu akajiandaa kumuingilia Monna , Kiongozi wa vijana hao kabla hajamfikia Monna walisikia mngurumo wa gari, wakamziba mdomo Monna wakaingia nae ndani ya Pango wakamthibiti Monna vizuri, Gari lililofika eneo hilo lilikuwa limembeba Kakinga , Kakinga aliposhuka toka kwenye gari alianza kumwita Monna kwa sauti ya juu sana , Kakinga aliita kwa hisia na machungu makali lakini kimya kilizidi kutawala eneo hilo .


Kakinga alizidi kumwita Monna bila kuchoka kakinga alizunguka eneo kubwa katika eneo hilo la kutupia uchafu ( Jalalani ) bila mafanikio, wakati huo Monna alikuwa anamuona na anamsikia mume wake lakini hakuweza kumjibu kutokana na kuzibwa mdomo, Muda ulizidi kwenda Dereva aliyemsaidia kakinga alimfuata Kakinga akamwambia:


DEREVA: Tuondoke Kaka muda unazidi kwenda alafu hili gari sio langu kwahiyo nataka kurudisha gari ofisini vinginevyo nitapigwa faini .


KAKINGA: Kaka nivumilie kidogo nahisi mke wangu hayupo mbali na eneo hili naomba nivumilie kidogo??


DEREVA: Ndugu yangu kwa hali yeyote hakuna binadamu anaeweza akawa eneo hili labda mbwa na viumbe wengine wanaotembea usiku lakini si binadamu hebu angalia tumezunguka eneo kubwa tu lakini hakuna hata dalili ya kuwepo huyo Mke wako, Mimi naondoka Kaka niambie nikuache huku au tunarudi wote tulipotoka ?


Kakinga alifikiria sana kisha akamjibu Dereva: Wewe waweza kuondoka kaka lakini siwezi kuondoka eneo hili nahisi mke wangu yupo eneo hili, nashukuru kwa msaada wako kaka mungu akulipe.


Dereva alipanda kwenye Gari lake akawasha na kuondoka akamuacha Kakinga eneo hilo la kutupa takataka, baada ya Dereva kuondoka Kakinga nae akasogea upande wa pili wa eneo hilo, Vijana waliomkamata Monna walifurahi mno kiongozi wao akasema: Wajinga hawa badala ya kutupa takataka na kuondoka wanaanza kupotezeana muda tu pumbafu kabisa sasa vijana wangu Muda ndio huu kazi iendelee nitafaidi leo ????


Monna alipomuona Mume wake anaondoka aliishiwa nguvu Dereva aliyemsaidia akiwa anatoka eneo hilo alisikia sauti ya Mtoto akilia ikabidi asimame kisha akazima gari ili aisikie sauti hiyo ya Mtoto anaelia , Sauti ikasikika kwa mara ya pili Dereva akashuka chini akawasha taa na kuanza kuifuata sauti ya mtoto huyo. Baada ya kutafuta sana Dereva akafanikiwa kumuokota mtoto mdogo Dereva akarudi eneo alilomuacha Kakinga cha ajabu hakumuona Dereva akamwita Kakinga kwa bahati nzuri Kakinga hakuwa mbali na eneo hilo, Kakinga aliposikia anaitwa alimfuata Dereva alipofika Dereva akampatia Mtoto aliyemuokota alafu akasemwambia:


DEREVA: Huyo mtoto nimemuokota hapo nyuma sasa sijui kama unamfahamu ? Kwa maana uliniambia unamtafuta mke wako pamoja na mtoto mdogo .


Kakinga alimpokea mtoto haraka haraka akamtazama akamuona Akwelina, Kakinga hakuamini kama amempata mtoto Kakinga alimbusu akwelina na kumkumbatia alafu akasema : Ndio ndugu yangu mtoto huyu ni wangu na alikuwa na mama yake sasa sijui mke wangu ameuwawa masikini ??


Kakinga alishindwa kujiziwia baada ya kuhisi Monna huenda atakuwa ameshapoteza maisha , kakinga alipiga magoti akalia sana kwa uchungu, Monna alikuwa anamuona mume wake anavyoteseka kumtafuta roho ilimuuma sana Monna , Monna alipowaona vijana hao wameshangaa akatumia nafasi hiyo akarudisha kichwa chake nyuma ghafla kwakua vijana hao walikuwa wamezubaa Mkono wa aliyemziba mdomo Monna ukatoka Monna akaita kwa sauti ya juu mno :


" KAKINGAAAAAAAAAA "



ITAENDELEA

Comments